Ogopeni sana watu wanaosema wao hawana upande wowote katika siasa za nchi hii na wakati huo huo wanapiga kura

Nimeisikiliza clip ya akina Kubenea wakijadili jinsi ya kummliza Boniface Jacob, wanadai akishaondoka Boniface Jacob itakuwa kazi rahisi kumng'oa Mbowe kwenye uenyekiti
Aisee ni hatari sana ,kama wangefanikisha adhimu yao bila shaka ingesingiziwa serikali kwamba imehusika .
 
Nyie endeleeni na siasa mkuu sie tunajua kucheza na matukio huku.
Katika pilika pilika za kumtafuta MO porini si ndo tumegumia hili gari la pombe limepinduka.!!!?KAZI NA DAWA

Kwa kusema gari la pombe una maanisha pombe huyu huyu ninaye mjua au kilaji?
 
CHADEMA walishajua watanzania ni watu wa aina gani na wakaingiza sokoni bidhaa inayokubalika na matokeo yake mliyaona.

Watanzania wangekuwa wanajali sana ufisadi, Kikwete mwaka 2010 asingepata hata asilimia 30 ya kura na watu kama kina Chenge mwaka 2015 wasingerudi Bungeni.

CHADEMA wamehubiri sana ufisadi lakini kila uchaguzi CCM inapata wabunge wengi na hata leo hii tunarudia uchaguzi kwasababu za kipuuzi kabisa ambazo chanzo chake ni CCM lakini bado watu wanawapigia kura wagombea wa CCM waliojiuzulu na kugombea tena.

Tatizo sio CHADEMA bali tatizo ni watanzania wenyewe na ushahidi ni kura alizopata Lowassa ambazo hakuna mgombea wa uraisi kutoka CHADEMA aliewahi kuzipata.

CHADEMA waliangalia watanzania wanapenda bidhaa gani na wao wakaiingiza sokoni na hakika iliuzika tena sana.

Cha muhimu ilikuwa ni kuitoa CCM madarakani kwa kutumia silaha yoyote ile then mambo mengine yangefuata baadae.
Na matokeo ya ujio wa Lowassa na mafuriko yake tunaona sasa aftermath of 'political flood'.
Yamejenga kutoaminiana ndani ya chama chenu kiasi kwamba mnapotaka kupanga mikakati yenu ya siri ya ushindi hamjui nani yupo pamoja nanyi (chama). na hamjui juma lijalo nani atakuwa upande wa adui yenu.

Mlipata viti vingi na sasa kimoja baada ya kingine vinaondoka na kuacha ufa unao kibomoa chama.
Muda umetupa majibu sahihi nani alikuwa sahihi kuhusu ujio wa Lowassa.
Subiri 2019-2020 tutaona mengi zaidi.

Muda wakurekebisha makosa upo watu wapokee maoni na watulize vichwa tu.
Chama kiwe na nguvu kuliko viongozi wa chama ndio, namaanisha maoni ya wanachama wa kawaida yasikilizwe zaidi kuliko ya viongozi, viongozi watumike kuratibu wanachama na namna ya kupata maoni yao sahihi na mazuri.

Viongozi wasijenge zile fikra kwamba wao ndio wana akili sana au wanajua sana kuliko wanachama wao. Wanachama wanawakilisha maoni ya wananchi wengi sana pamoja na ya wale ambao si wanachama lakini wananataka mabadiliko chanya.
 
Na matokeo ya ujio wa Lowassa na mafuriko yake tunaona sasa aftermath of 'political flood.

Hata CCM wanalalamika siri za chama kuvuja.

Nikwambie tu, hii mbinu ya kununua wanasiasa inawaharibia zaidi CCM na maneno kwamba upinzani unakufa ni propaganda tu za watu walioshindwa ku-deliver.

Kama wanaamini CHADEMA wamepata pigo, waambie habari ya Tume Huru kama watakuelewa.

CHADEMA ni chama kilichokua,kujijenga, kukomaa na kusambaa kiasi kwamba huwezi tena kukiua kwa kutumia mamluki au propaganda nyepesinyepesi.Hayo yangewezekana wakati chama hiki bado ni kichanga lakini sio leo hii.
 
salary slip, watu wa aina hiyo kule kwetu tunawaita 'watu mfu' kwa maana hawajui kwanini wapo duniani. Niliwahi kusikia kuwa kuna wakati mwingine huwa wanasahau hata jinsia zao!
 
Hata CCM wanalalamika siri za chama kuvuja.

Nikwambie tu, hii mbinu ya kununua wanasiasa inawaharibia zaidi CCM na maneno kwamba upinzani unakufa ni propaganda tu za watu walioshindwa ku-deliver.

Kama wanaamini CHADEMA wamepata pigo, waambie habari ya Tume Huru kama watakuelewa.
Ni kweli lakini angalau wenzenu wanavuna wananchama wenu na huku wanapandikiza migogoro kwenu.
Pili wao wamezoea kuvujishwa kwa siri zao kwenda kwa wapinzani hasa pale wanapo gombania maslahi flani binafsi baadhi ya wananchama wao.

Sisi tulizoea CHADEMA kulikuwa na nidhamu na usiri. CHADEMA ilisifika kwa intelijensia makini.
Mafuriko yameziba kiungo muhimu cha CHADEMA kunusa na kuzuia hujuma mapema kabla hazijaleta madhara.
Kukosea ni kujifunza, cha muhimu viongozi wakubali walikosea na wajisahihishe.
 
Hakuna cha maana wanachofanikisha na ndio maana kila siku wanahangaika.

Walitarajia mpaka sasa chama kiwe kimesambaratika na hii hamahama lakini chama kiko imara.

Waambie wakupe hata ushahidi wa kimazingira kuwa chama kinakufa uone kama watakuwa nao.Aliondoka Dr.Slaa wakadhani chama kingekufa lakini ikawa kinyume chake.

Hii ya kununua wanasiasa imeshafeli na sasa wataibuka na mbinu nyingine.

Jiulize wanavuna wanachama wetu kwa mbinu gani na pia jiulize wanaohama ni wananchi au viongozi tena wengi wao ni hao waliokuwa huko CCM.

Angalia hata sababu za wanaohama eti kumuunga mkono raisi na sababu nyingine za kushangaza kabisa.

Leo hii watakwambia intelijensi ya CHADEMA imekufa.Waulize ni lini waliwahi kukiri kuwa intelijensi ya CHADEMA ni nzuri au iko juu?

Walichokifanya Lema na Nassari kuwarekodi wale mamluki haikuwa intelijensia? Ingekuwa ni uzushi, wangeacha kuwakamata?

Na wewe binafsi unataka intelijensi gani?
 
Kwa mtazamo wangu,

Ni vizuri kujitambulisha hivi. Lakini mtazamo wako ni potofu. Hakuna binaadam asiyekuwa na upande.

Kutokuwa na upande wa siasa, haina maana mtu hawezi kuwa na upande wa mambo ambayo angependa kuona yakitendeka katika jamii na kwa nchi yake. Maana yake ni kwamba, wapo watu ambao upande wao daima ni Taifa lao bila kujali ni shetani au malaika gani anacheza ngoma kwa wakati husika.

Kwa baadhi ya hawa watu, kuna mstari mwekundu usioweza kuvukwa na shetani, halafu wakashangilia matendo machache yanayoonekana kuwa mazuri.

Kwa hiyo huwezi kulazimisha watu wawe upande wako kwa vile tu upande mwingine kuna shetani. Kama yapo mazuri upande wako hawa watu watayakubali hayo mazuri yako na kuendelea kuyakataa ya shetani. Kama shetani anafanya matendo ya kukuonea wewe na kukudhurumu haki yako, hawa watu watasimama na wewe bila ya kujali kama wanakubaliana na mambo unayoyasimamia na kuyaamini wewe. Na huna haki ya kuwasuta na kuwalaumu kwa nini wasijisalimishe kwako.

Kwa upande mwingine, watu wenye upande mara nyingi huangalia zaidi dhamira ya kiongozi na sio matendo au maamuzi anayoyafanya ambayo wakati mwingine ndani yake yanaweza kuwa yamejaa hadaa fulani ili kupumbaza watu.

Jambo la msingi kwa mtu yeyote ni dhamira na imani aliyonayo mtu huyo, na sio dhamira na imani ya mtu mwingine awaye. Siwezi kubadili ninayoyaamini kwa vile mtu mwingine (kiongozi) mwenye dhamira yake imenishawishi niiache ya kwangu.
Hapa ni kama unataka kufanya kupunguza thamani yangu mwenye akili timamu ya kufikiri na kuchagua niayatakayo. Hilo haliwezekani hata siku moja.

Hii ni dhana uliyoianzisha ijadiliwe, lakini hukuitendea haki hata kidogo kurahisisha jambo muhimu kama hili.
 
ukishakuwa na upande tayari umepoteza uhuru wako. hakuna kitu muhimu katika maisha kama uhuru. uhuru ni msingi wa mambo yote. siasa za mavyama kumbatieni tu wakuu. sisi tutawasuport pale tutakapoona mmelinda maslahi ya umma. pale mtakapoboronga tutasema.
 
Huwa sipigi kura kabisa,nimesimamia chaguzi mbalimbali katika nchi yangu,wala sikuwahi kutilia maanani kile wanachokifanya (kupiga kura)zaidi ya kutimiza wajibu wangu kama nilivyoelekezwa ili nipate stahiki yangu.
 
katika siasa za hizi nchi zetu za dunia ya tatu hakuna namna ya kukwepa kuwa kigeugeu kwani vyama havitofautiani kisera

Unaweza kuwa uko chama tawala lakini ukisikiliza hoja za zitto unaona kabisa zina mashiko sasa unaachaje kumsapoti

Kitu cha msingi sasa ni kuangalia maslahi ya taifa na si kupinga kila kitu au kusapoti kila kitu

Kwa lugha rahisi ni kuwa unatakiwa kujiepusha kuwa na mwenendo kama wa robot
Maneno machache yaliyochukua uzito mkubwa.
Ahsante mkuu.
 
Sina upande wowote wa siasa ukifanya upuuzi nakosoa uwe A au B.

Sijawahi kupiga kura katika maisha yangu na SITAKUJA KUPIGA KURA.
Watu wasiopiga kura ndio huwachagua viongozi wabovu. Kura za wasiopiga kura ndio zingekuwa kura za kumkataa kiongozi wa hovyo lakini kwakuwa hawapigi kura wanawaachia wachache wanaomuunga mkono kiongozi sababu ya kupewa tu kapelo, tshirt, skafu na vilemba mwisho hao wakileta kiongozi mbovu wasiopiga kura ndio wanakuwa wa kwanza kulalamika. Your vote can make a difference!
 
Aliyekwambia wapiga kura nyie ndio mnachagua viongozi ni nani?
 
Hawa wanaotung'ang'aniza kwenye vyama wanataka tutetee matumbo yao kimakundi kwa kufuata mkumbo kama nyumbu.
Utachaguaje chama kama vyama vyote havina itikadi na sera zinazoeleweka?
Sio kazi nyepesi kulibishia wazo hili. Lakini sielewi kwa nini hili lisieleweke kirahisi kabisa kwa yeyote anayetaka kucjua.
 
Aliyekwambia wapiga kura nyie ndio mnachagua viongozi ni nani?
Ni kwamba ninyi msiopiga kura mkiwa wengi mnatufanya sisi tunaoishi kwa kutegemea kapelo, tshirt, vilemba na skafu tuwachague wasiofaa kumbe mngepiga kura mngemchagua anayefaa badala ya kuchagua kwa viwewe vya push ups na kuletewa wasanii kibao eti kwasababu hatuna viingilio. Wakishapita ndio wanaanza kutuita ni masikini na wanyonge na masikini wa nchi hii simply because tunategemea kila chaguzi tupewe kapelo, tshirts, kanga na skafu
 
Hapana kwangu mimi kupiga kura ni MARUFUKU.

Kwa mtazamo wangu,licha ya haki yao ya kutokuwa na upande,hili ni kundi la watu "mzigo" maana ni watu wanaokuwa influenced na matukio yanayofanya na wanasiasa pasipokujali dhamira za wanasiasa hao na wanakuwa ni watu wa kuyumbishwa tu na bahati mbaya kura wanapiga kuchagua viongozi.

Watu wa aina hii,mwanasiasa leo akipata tuhuma za kuua, ufisadi au kudhuru, na kesho akajenga barabara,akawapa hela, n.k, wao watakuja hadharani na kumsifia wanasahau kabisa kuwa ni lazima mwanasiasa huyu afanye mazuri machache ili apate kuungwa mkono ili kesho tena aweze kudhuru, kuiba, n.k(anang'ata na kupuliza).

Watu wasio na upande ambao leo watamsifia na kesho watamlalamikia, wanashindwa kuelewa kuwa mwanasiasa wa aina hii lengo lake ni kuwa-fool watu ili aweze kupata kundi la watu wa kuumunga mkono, hata kama ni wache, licha ya madhambi ya makusudi anayoyafanya.

Kwa upande mwingine, watu wenye upande mara nyingi huangalia zaidi dhamira ya kiongozi na sio matendo au maamuzi anayoyafanya ambayo wakati mwingine ndani yake yanaweza kuwa yamejaa hadaa fulani ili kupumbaza watu.

Watu wanye upande, mara nyingi wao huangali zaidi dhamira ya mtu na wakishagundua ni mtu wa aina gani, basi hufanya maamuzi ya ama kumuunga mkono au kumkataa (kuwa na upande mmoja) na watu wa aina hii ndio wanaweza kufanya maamuzi sahihi katika sanduku la kura tofauti na wale utakaowasikia wakisema mimi niko neutral ambao huyumbishwa na matukio au maamuzi ya wanasiasa pasipo kuwapma dhamira zao na matokeo yake hufanya maamuzi yasiyo sahihi katika kuchagua viongozi.

Kwahiyo, wale wote ambao leo utwasikia wanamlalamikia mwanasiasa fulani na kesho wanamfagilia,mjue tu watu wa aina hiyo teyari ni mateka wa fikra na hawana tofauti na mwanaume alielishwa "limbwata" na kuwa "zezeta" na hawa wanaponza hata wale walioamua kufanya maamuzi ya kumkataa mwanasiasa au kiongozi wa aina hiyo (mwenye tabia ya kung'ata na kupuliza).

Ni kweli binadamu wote tuna mapungufu, lakini kufanya au kutenda mambo mabaya kwa makusudi,hii huwa ni dhamira ya mtu ambayo siku zote ndio tunapaswa kuitumia katika kumpina mtu, kiongozi au mwanasiasa yoyote yule.

Kiongozi bora apimwe wa dhamira iliyo nyuma ya maamuzi au matendo yake na kamwe si kwa kutazama matendo au maamuzi anayoyafanya kwani mtapotea na kudanganyika.
Kama MTU anajiita P. Mselewa na Mtazamo kama vile wana ubongo wa samaki,
 
Baada ya MO kutekwa, CHADEMA IKAJA NA AJENDA YA VOICE CLIP NA KIKAO CHA KAMATI KUU

Je kuna jambo limejificha?
 
Back
Top Bottom