Ogopa hizi shuhuda

Kuna siku nilikua zangu nyumbani likizo fupi.basi nikiwa sina hili wala lile nilishangaa meseji inaingia kwenye simu yangu frm mamdogo wangu yupo Arusha.Akaniambia amepata matatizo nimsaidie elf 50 kwa mpesa atanirudishia akijisort.nikaamua kumpigia ajabu akawa hapokei.nikapiga kama mara nne nilitaka kumuuliza kama kuna tigopesa maana mimi mpesa yangu nilikua na 2000 tu.wapi?hapokei.

Basi nikamtumia hivyo hivyo atajijua mwenyewe maana simu hapokei.kama nusu saa hivi dadaangu nae ananipigia kuniambia kama mamdogo amekwama lakini nimemsort.nikamwambia basi tumemtumia kwa wakati mmoja.sio kesi.sijakaa sawa mama ananiambia hebu mpigieni mama yenu mdogo mimi nikimpigia hapokei kasema kuna tatizo anaomba hela.apo alarm ikalia.

Nikampigia mume wake.eti mamdogo yuko wapi?akasema sijui maana kanitumia meseji eti amepata shida nirushie elf 50 sasa nikipiga hapatikani.na akipatikana hapokei.tukahisi tumeliwa.muda huo huo na mamdogo akampigia mumewe kumwambia kama kaibiwa simu na anarudi nyumbani.daah heka heka iliopita hapo si mchezo.mbio mpaka kwa

wakala.yangu ilifanikiwa kurudishwa ila zingine zilienda maana alikua anatumia tigo na mimi nilituma tigopesa kwa hiyo ikashindwa kutolewa.ile zile laki moja mpesa za dada na mama zikaliwa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
you're genius


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko Kyela huku kuna mahali panaitwa Ipyana darajani karibu na Kambi ya jeshi la JWTZ kuna jamaa anaitwa Chaurembo mkinga mmoja kapigwa 2 million kwa kuamini uganga uganga na jamaa anaduka lenye vitu full, siku nne hajafungua duka stress za kupigwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nilikaa sana hapo darajani...njia kuu ya kuelekea NGONGA BEACH..hv bdo ipo ile?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro mmoja kariakoo alipigwa 124m
Aiseee walimpeleka LINDI PANGONI ETI AKASHIKE MKONO WA MALAIKA WA ULINZ WA PESA.ANASEMA WA BARIDI
HALAFU WALIMPELEKEA SANDUKU TATU ZA DOLA ETI AWEKE NA HELA ZAKE ZA KIBONGO.AISEEEEE
Naomba story zaid please,,,,,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wa kushuhudia biashara fulani inalipa ni wengi sana,hao ni wahujumu uchumi wa vijana wenye uchungu wa maisha.Maana wengine ni wazee wanaoonekana kuwa na hekima kumbe maboya tu na wanaishia kuumiza watu wanaowaamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…