Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wenzetu - hasa kwenye nchi zilizoendelea sana - wanapoamua kuwakamata mafisadi hawafanyi kwa kificho na wakiamua kufanya wanafanya kweli kweli. Pamoja na kuwakamata watuhumiwa, nyumba zao zinasachiwa, ofisi zao zinasachiwa, kompyuta na vielelezo mbalimbali vinakusanywa ili kuhakikisiha kuwa ushahidi wote unaowezekana kukusanywa unapatikana.
Maofisa wa FBI, IRS (TRA ya Marekani) na wengine wakitoka na nyaraka mbalimbali toka ofisi za chama cha Democrat ambapo kulikuwa na tuhumiwa wea ufisadi huko New York na California (Soma Hapa)
Maofisa wa FBI Walipovamia ofisi ya Dkt Salomon Melgen kwa tuhuma za ufisadi ikiwemo kusababisha hasara serikali kupitia uhujumu taasisi za bima mbalimbali za afya. Soma Hapa
Hapa kwetu Detroit hivi majuzi maofisa wa FBI walivamia ofisi ya daktari mwingine kwa mambo hayo hayo, siyo tu ofisi lakini pia hadi nyumbani kwake ili kukusanya ushahidi mbalimbali.
Yote hii ni mifano michache tu ya jinsi gani unapoamua kupambana na ufisadi unapambana mzima mzima. Haitoshi kuwapigisha magoti kina Rugemalira na Singh bila kuhakikisha kuwa mali zao zote, ofisi zao zote zinapekuliwa pamoja na majumba yao yote ili kukusanya ushahidi wote unaowezekana.
Haitoshi tu kusema unawashtaki kwa tuhuma zipi wakati hujatumia muda wa kutosha kukusanya ushahidi mzito dhidi yao. Sijui hadi hivi sasa kama kuna warranti zimetoleaw dhidi yao zina upana gani.
Ni matumaini yangu kuwa DPP na vyombo vya dola vitatumia nguvu zote za uwezo wote wa sheria kukusanya ushahidi na kutengeneza mashtaka ambayo yatakusanya wote waliohusika na kashfa hii na kuwashtaki to the full extent of the law!