Ofisi za ardhi Manispaa ya Sumbawanga bado inatoza riba ya kodi ya Ardhi kinyume cha agizo la Rais

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Wadau Kupitia waziri wa ardhi Mama Mabula alitangaza kuwa Mhe. Rais katoa Msamaha kwa wadaiwa wa kodi za ardhi kwa kuondoa riba ya kodi ya ardhi.

Msamaha huo bado hautekelezwi na ofisi za ardhi nyingi ikiwemo manispaa ya Sumbawanga.

Ukienda kuchukua hesabu ya Kodi unayodaiwa bado watendaji wa Ofisi za ardhi wasio na weledi wanakupigia na riba ya kodi ya ardhi kinyume na agizo la Rais kupitia Waziri mwenye dhamana na ukiwauliza wanajibu kuwa hawajapata waraka.

Juzi Kamishna Msaidizi wa ardhi kasisitiza kuwa riba ya kodi ya Ardhi isitozwe.

Ombi kwa Waziri wa ardhi, Wizara itoe waraka wa huo msamaha wa ili Wananchi walipe kodi bila kutozwa riba ya kodi kwa Wakati uliowekwa.

cloudstv_1676273583871335.jpg
 
Back
Top Bottom