Ofisi ya Rais Mstaafu Kikwete yasikitishwa na habari zinazoenea, yasema kuwa hotuba ya Kikwete haikumlenga mtu

Kajichota mwenyewe hajamchota mtu maneno aseme yeye halafu akanushe yeye mwaka huu tutaona mengi
Hajakanusha, hajafuta maneno yake. Amesema hiyo tafsiri mnayoitaka nyinyi siyo aliyomaanisha.
 
Kikwete atakua anaogopa kurogwa, maana Meko ana kikundi cha wachawi 900 kikiongozwa na Bashite wanaotumia uchawi wakishindwa kukuteka!
 
“ Ofisi ya Mstaafu Kikwete imetoa masikitiko juu ya upotoshwaji kuhusu hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano la Mwl. Nyerere “Hakuzungumzia mwingine zaidi ya Mwl. Nyerere na hakufanya ulinganifu kati ya Mwl. Nyerere na Marais waliofuata, waliostaafu na waliopo ”

Chanzo Taarifa: Millard Ayo na imetolewa dakika 65 hivi zilizopita ( nikimaanisha bado ni ya Moto Moto )

Limewashuka na sijui mtaficha wapi sasa Aibu zenu kwani mlilolitaka halijafanikiwa na Mkwere kawaruka kudadadeki!.
Sasa ulitarajia aseme alimlenga mtu! Hilo ni jiwe limerushwa gizani linamhusu kila mtu kwa matendo yake ...ila ujumbe umefika!
 
Hotuba na mwenendo wa nchi yetu kwa sasa ni kama mapacha wanaofanana ( identical twins) hauhitaji kuambiwa wala kufafanuliwa.
 
Sawa lakini msg ukisha isend huwezi tena kuikata eti isiende
Ofisi ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete imetoa taarifa ya masikitiko juu ya upotoshwaji uliofanywa na baadhi ya Watu kuhusu hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano la Mwalimu Nyerere.

“Mada ya kongamano ilikua Urithi wa Mwl. Nyerere katika Uongozi, Maadili, Umoja na Amani katika ujenzi wa Taifa, katika hotuba yake Rais Mstaafu Kikwete alielezea jinsi alivyomfahamu Mwl. Nyerere, kilichotushangaza na kutusikitisha sisi na Rais mstaafu ni kujitokeza Watu wanaopotosha ukweli kuhusu maneno aliyosema Rais mstaafu JK”

“Tunapenda kusisitiza kuwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kamwe hakuzungumzia Mtu mwingine yeyote zaidi ya Mwl. Nyerere na hakufanya ulinganifu Kati ya Mwl. Nyerere na Marais waliofuata baada yake, waliostaafu na waliopo sasa, katika hotuba yake hakutaja jina la Mtu yoyote hivyo tunaposikia wakidai Rais mstaafu alikua anasema Mtu ni jambo lililotusikitisha na kutusononesha, ni uzandiki fitna na uchonganishi”

View attachment 1229421
 
MMMH vipi tenahukoi Dreva nashuka kituo kinachofwata tafwadhali
 
Neno likitoka huwa halirudi. CCM wanapigana vikumbo mitandaoni kujibu maneno yake.
JK ni Rais mstaafu,ulitaka ofisi yake itamke kuwa maneno yake YALIMLENGA Rais aliyempokea kijiti?
Ametumia a diplomatic speech kufikisha ujumbe na umefika vyema. Huwezi kabidhiwa uongozi ukaanza kuona watangulizi wako hawajafanya kitu. Unajiona wewe ndiyo MALAIKA na KUJIMWAMBAFY.
Bado nasisitiza kwa kusema kuwa ' Limewashukeni ' na Mkwere kawaonyesha jinsi alivyowachoteni na kuwamwageni mazima.
 
Duu kweli JPM anaogopeka tehe tehe tehe mpaka watu wanakana clip zao
 
Binafsi nilielewa kulingana na hii statement ila kama kawaida yao, upinzani badala ya kujenga hoja yakinifu huwa wanaokoteza vioja na kugeuza sera, mnatukwamisha sana.
Wapinzani wamekujaje tena hapa mkuu?
Hotuba katoa Rais mstaafu, wana CCM wa Magufuli wakaitafsiri Kwamba, Kikwete alikuwa anamsema malaika wao, sasa wapinzani wametoka wapi?
Huwezi ukamaliza siku bila kuwataja wapinzani?
 
Mzee hakuna watoto wadogo humu kusoma hujui hata picha huoni??? Magufuli oyeeeeee piga kazi mkuu tena ongeza ndege zingine nyodo Kwa waajiliwa wa serikali hakuna tena wanyoosheee Baba magufulii jembeeeeeeeeeau niongeze sautiiiiii
 
Ni Mwalimu aliyemsema hadharani Mzee Mwinyi, lakini Mzee Mwinyi hakumsema Mkapa, Mkapa hakumchamba Kikwete, lakini Kikwete anamchamba JPM.

Hamtendei haki, huwa ninamuelewa sana JPM anapoomba aombewe kila mara, maadui wa hatari ni wale wa ndani ya nyumba unayoishi, wenye kuweza kukuwekea sumu kwani wapo karibu na jiko pamoja na jokofu.
 
Mheshimwa Raisi Mstaafu.
Miye nawe ni watu wa pwani kiswahili cha mafumbo na mila yetu.

Unapotaka kumuambia ukweli mtu huwa kwanza tunamuanzi kwa ishara na mafumbo yenye ushauri mwema.

Pia tusisahau wahenga walituasi kwa fumbo " FUMBO HUFUMBIWA MJINGA MJANJA HULITAMBUA"

Ushauru wako kwenye hili fumbo limeeleweka na wengi, na ni wakweli, pia inaonyesha kuwa mumejaribu kushauri faragha na hamkusikilizwa na wananchi wengi wanamitegemea, kweli mko kwenye hali ngumu sana.
 
Alichokisema kiko wazi na amefanya vizuri kukanusha kwani kwa nafasi yake atajikuta matatizoni. Hiyo hofu aliyonayo hakuna mtu hana, ila ambacho hataweza ni kubadilisha alichokisema mwanzo. Tafsiri Aachie wengine lakini ujumbe uko bayana fullstop.
 
Back
Top Bottom