Ofisi ya Rais Mstaafu Kikwete yasikitishwa na habari zinazoenea, yasema kuwa hotuba ya Kikwete haikumlenga mtu

Message sent tayari

Tatizo ni kwamba mtu ukiongelea uadilifu wa mwalimu lazima Jiwe atadhani unamsema yeye, maana mwalimu alijenga nyumba za serikali jiwe akahonga kwa mchepuko,

Sasa ktk mazingira haya ukiusema uadilifu wa mwalimu jiwe lazima ajistukie kwa kudhani kwamba unampiga madongo yeye!
Unao uhakika kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi kupiga hata mara moja?. Na hizo nyumba alizihonga yeye kama yeye au yeye kma sehemu ya baraza la mawaziri. Hujawahi kuja kutuambia za kina Mkapa na Sumaye walizifanyia nini.

Huyu tunaye mpaka 2025, tuombe uhai.
 
Hajakanusha, hajafuta maneno yake. Amesema hiyo tafsiri mnayoitaka nyinyi siyo aliyomaanisha.
Zamani kwenye mtihani tulikuwa tunaletewa kipengele cha hadithi.
Unaisoma halafu unaulizwa maswali kutokana na hiyo hafthi. Ndicho wananchi walichowrza kutoa mitazamo yao kutokana na hotuba waliyohotubiwa na raisi mstaafu.
 
Mzee Kikwete tatizo ni kale kamsemo kako. Acha tujiongeze mzee! Sasa kama hayawahusu mbona wamelia lia? Wewe ushatimiza wajibu wako, acha sisi tupake rangi.
 
Ofisi ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete imeeleza masikitiko yake kuhusu upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuhusu hotuba aliyoitoa Kikwete kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere

Imesema kuwa mada ya Kongamano hilo ilikuwa ‘Urithi wa Mwalimu Nyerere katika Uongozi, Maadili, Umoja na Amani katika Ujenzi wa Taifa’ na Rais Mstaafu alieleza kwa namna alivyomfahamu Mwalimu Nyerere kulingana na mada hiyo

Ofisi hiyo imesema Rais Mstaafu Kikwete ameshangazwa na kusikitishwa kwa kujitokeza watu wanaopotosha ukweli kuhusu maneno yake na kuwepo wanaojaribu kumuwekea maneno wakidai eti alikuwa anawasema baadhi ya viongozi waliopo sasa

Aidha, ofisi imeeleza kuwa hakufanya ulinganifu kati ya Mwalimu na Marais walifuata baada yake, waliostaafu na waliopo sasa pia hakutaja jina la mtu yeyote, hivyo kusikia kuwa Rais Mstaafu alisema mtu ni jambo linalosikitisha ni uzandiki, fitna na Uchonganishi

Mwisho, Rais Mstaafu Kikwete amesema alitegemea watu wamkosoe kwa aliyoyasema na si kumsingizia na pia amewataka watu wenye maoni yao wawe wajasiri na kuyasema na sio kujificha katika kivuli cha hotuba yake

View attachment 1229421

Hii barua ni feki sana!
Anyway, mimi nafikiri mh alisema ukweli na alizungumza kuhusu viongozi.
Amerufurahisha wengi na sidhani kama kuna aliyepotosha yaliyosemwa!
 
Unao uhakika kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi kupiga hata mara moja?. Na hizo nyumba alizihonga yeye kama yeye au yeye kma sehemu ya baraza la mawaziri. Hujawahi kuja kutuambia za kina Mkapa na Sumaye walizifanyia nini.

Huyu tunaye mpaka 2025, tuombe uhai.

Mbona hapo karibu, akae mpaka atembelee mkongojo akiwa na 90+.
 
Mbona juzi na jana hizi Kauli hamkuzitoa na mnazitoa leo baada ya Mkwere Kuwashushueni?
Kwa namna Magu alivyokuwa akisema katika hotuba yake huko Mpanda jana ni dhahiri kuna kitu kilimgusa kutokana na hotuba ya Mkwere!
 
Kwa namna Magu alivyokuwa akisema katika hotuba yake huko Mpanda jana ni dhahiri kuna kitu kilimgusa kutokana na hotuba ya Mkwere!

Hivi mwenye Dola na Mamlaka ya Kikatiba anaweza ' Kutishwa ' na Mtu ambaye kwa sasa hana ' Nguvu ' yoyote ile? Hivi nyie baadhi yenu Vichwani mwenu kumewekwa nini hadi mnakuwa Wavivu hivi wa Kufikiri?
 
Back
Top Bottom