Ofisi ya Msajili wa Hazina yakusanya asilimia 109.50 ya lengo

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Ofisi ya msajili wa hazina imefanikiwa kukusanya mapato yasiyo ya kodi ya jumla ya Shilingi bilioni 852.98 ikiwa ni asilimia 109.50 ya lengo katika Mwaka wa Fedha wa 2021/22 ulioishia Juni 30, mwaka huu.

Taarif iliyotolewa na ofisi ya msajili wa hazina imeeleza kuwa katika Mwaka wa Fedha wa 2021/22, Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) ilipangiwa kukusanya mapato yasiyo ya kodi ya jumla ya Shilingi bilioni 779.03, ambapo imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 852.98 ikiwa ni saw na asilimia 109.50 ya lengo.

Makusanyo hayo yameongezeka kwa Shilingi bilioni 214.11 kutoka kiasi cha makusanyo ya Shilingi bilioni 638.87 kwa mwaka 2020/21, sawa na ukuaji wa asilimia 33.50.

Matokeo haya yanatokana na:
1. Kuimarika kwa shughuli mbalimbali za uchumi chini ya uongozi madhubuti wa
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini

2. Uhusiano mzuri kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Taasisi zote inazozisimamia; kudhibiti matumizi pamoja

3. Kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji katika Taasisi na Mashirika ya Umma ambayo imekuwa chachu ya ufanisi huu mkubwa.

Hii ni moja kati ya vielelezo vinavyoonesha uchumi kurejea katika hali nzuri baada ya mazila makubwa ya task force, kutumia nguvu na mabavu kwa wafanyabiashara n.k
 

Attachments

  • Hazina.jpeg
    Hazina.jpeg
    168.8 KB · Views: 8
Back
Top Bottom