ZRA yakusanya bilioni 565.8

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Yusuph Juma Mwenda amesema katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2022/2023, ZRA ilipangiwa kukusanya bilioni 579 Kwa mwaka mzima ambapo hadi kufikia June 30,2023 wamefanikiwa kukusanya bilioni 565.8 sawa na ufanisi wa 97.6%.

Mwenda amesema ufanisi huo umeongezeka kwa 51.1% ukilinganisha na 2021 ambapo walikusanya shilingi bilioni 374.2 katika kipindi kama hicho.

"Kiwango hiki ni zaidi ya mara moja na nusu ya tulichokusanya mwaka 2021/2022, kwanza ni kiwango kikubwa kwa ZRA kukusanya na sababu ni kwamba shughuli nyingi za kiuchumi zimeongezeka na pia tumeboresha huduma kwa Walipa kodi ikiwemo mfumo wa kutoa risiti na mfumo usimamizi wa kodi (ZIDRAS)”
 
Watakwambia Tanganyika ndio inawalisha Wazanzibar 😆😆

Ukitoa Dar,hakuna Mkoa mwingine ambao unafikia mapato ya Kodi ya Zanzibar na haya ni Yale ambao hayako kwenye vyanzo vya Muungano ambako TRA wanachukua.
 
Haya mlipe zile billion 60 za Tanesco chap
Watakwambia Tanganyika ndio inawalisha Wazanzibar

Ukitoa Dar,hakuna Mkoa mwingine ambao unafikia mapato ya Kodi ya Zanzibar na haya ni Yale ambao hayako kwenye vyanzo vya Muungano ambako TRA wanachukua.
 
Back
Top Bottom