Ofisi ya mbunge Temeke na ziara ya dharura hospitali ya rufaa Temeke

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Mhe Dorothy George Kilave, akiwa Nje ya Jimbo Kwa Dharura, ameielekeza Ofisi yake, Kufika Hospitali ya Temeke Imefuatiwa na Taarifa Iliyosika katika Wasafi Media Kipindi cha Good Morning (Uchambuzi wa Magazeti)

Hoja "Watu zaidi ya Mmoja Kulala kitanda kimoja wakisubiri kujifungua Hospital ya Temeke"!!!

Ofisi ya Mbunge imefika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa iliyopo Jimbo la Temeke Temeke, na kuzungumza na Dr Kamaro Mganga Mkuu wa Hospitali.

Kwa Mujibu wa Maelezo ya Dr Kimaro, Sio kweli kuwa tunalaza Watu zaidi ya Mmoja katika kitanda ila kunamrundikano Mkubwa katika wodi za Wazazi hivyo uhitaji wa kuongeza Wodi ni Mkubwa" ( Kuhusu Picha iliyo oneshwa kwenye Ukurasa wa Gazeti ameahidi kuitolea Ufafanuzi)

Pia, Mganga Mkuu ameionesha Ofisi ya Mbunge Wodi za Wazazi zilizopo. kisha kutupitisha kuona Jitihada walizozifanya katika kuongeza Jengo Jipya Kwa ajili ya Wodi ya Wazazi (Jengo litaanza kutumika Hivi Karibuni)

Ofisi ya Mbunge imepokea Maelezo ya Mganga Mkuu na kusisitiza kuwa Temeke Hospital, ni Hospitali ya ngazi ya Mkoa, inahudumia Watu wengi hivyo Kwa kuwa ipo Ndani ya Jimbo la Temeke wanapaswa kuzingatia huduma Bora Kwa Wananchi, Kisha Ofisi ya Mbunge imeahidi kufika Hospitalini hapo mala Kwa mala ili kuona Maendeleo ya Utoaji wa huduma Kwa Wananchi.

View attachment 2555137View attachment 2555135View attachment 2555133View attachment 2555136
IMG-20230317-WA0350.jpg
View attachment 2555134
 
Back
Top Bottom