View attachment 2530948
Wakati vyama vingine vya siasa vikipora majengo ya Umma na kuyafanya mali zao , ama kurithishwa majengo ya viongozi waliokufa na kuyapiga rangi , Hali ni tofauti kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo .
Chadema imeamua kujenga ofisi zake yenyewe kuanzia ngazi ya chini kabisa , wanachama wake wameamua kujipapasa mifukoni na kununua viwanja na kujenga ofisi za kisasa .
Tuliwahi kuandika humu kwamba mpaka sasa chadema imejenga ofisi za kisasa 457 nchi nzima , Wajinga wakabisha , Sasa huu ni mfano halisi wa tunayoyaandika humu mara zote
Leo Freeman Mbowe amepita kwenye kata hii akitokea Kyela , amejionea mwenyewe jitihada za Wanachama hao , na yeye akaguswa na kujipapasa kwenye Kombati yake na kutoa Ubani wa Laki 5 , Mungu amzidishie , Amina