Ofisi ya CHADEMA Jimbo la Tunduma yapigwa kiberiti na watu Wasiojulikana, nyaraka zateketea

Mmeanza tena zile ishu zenu za kutengeneza matukio ili kutafuta huruma za wananchi? Sijui mtakua lini nyie jamaa, zama za ujinga ujinga za JK zilishapita kitambo, now watu wanachapakazi tu..
Mwaka jana stoo yangu iliuungua mashine pamoja na mizigo ninaanza ikidaiwa chanzo umeme ninaanza kuwa na wasiwasi huenda ikawa ni siasa
 
Mara baada ya uchaguzi kuisha tarehe 5mwezi wa kumi na moja ofisi yangu iliungua moto ikidaiwa chanzo umeme lakini kadili muda unavyozidi kwenda naanza kubaini jambo.mm siyo mtu wa siasa ila nakosoa penye mapungufu huenda kuna mahali niliingilia vibaya ila Mungu si athumani
giphy.gif
 
Mungu ibariki CHADEMA... Kukichwa kutapambazuka.. Lakini kabla jua kuchomoza kiza huwa kinene
Mshana Jr mm naishi hapa karibu ila kuna mambo hayako sawa tunduma itoshe Tu kusema kuna wanachama either ccm au chadema ni waharifu wana siasa za chuki sana mpaka tulipofika hapa tuna mengi yaliyotokea
 
Mshana Jr mm naishi hapa karibu ila kuna mambo hayako sawa tunduma itoshe Tu kusema kuna wanachama either ccm au chadema ni waharifu wana siasa za chuki sana mpaka tulipofika hapa tuna mengi yaliyotokea
Unyama wa Polisi kwa Chadema ndio chanzo cha Uhasama , nakuhakikishia kwamba visasi vya tunduma havitokuja kwisha
 
Chadema followers are attention seekers!! Hapo wanatafuta huruma ya wananchi ili Hali ofisi wamechoma wao wenyewe
 
Jambo hili la kusikitisha limefanyika usiku wa kuamkia leo, ambapo watu wasiofahamika wamelipua ofisi hiyo na kisha kutokomea kusikofahamika, nyaraka kadhaa za Chama hicho zimeteketea na nyingine zenye thamani kubwa zimeibwa.

Ikumbukwe pia kwamba Viongozi wa Chadema zaidi ya 50 wa Tunduma wamerudikwa rumande kwa zaidi ya mwaka kutokana na visasi vya kisiasa.


Mungu ibariki Chadema
Mungu gani?
 
Upinzani bado hawajajua adui yao ni nani wao wamekalia kuaminishana eti magufuli ndie alikua adui yao,haya leo hayupo yote yanayotokea nani anayachangiza? leo hii mbowe yuko ndani takribani miezi 4 wapo kimya kama hakuna kilichotokea,sio jumuia za kimataifa hakuna tena anaekemea uminywaji wa uhuru wa kisiasa unaoendelea nchini,ofisi zinachomwa moto hawajui nani mchawi wao bado wamekalia eti kufuta legacy ya mwendazake badala kuchange gia kuendana na utawala uliopo ili waweze kufanya siasa na kujenga chama.

kisha mwaka 2025 waje tena na malalamishi et wameibiwa kura,mara wanasusia uchaguzi chini ya tume iliyopo japokua sijui kama watamtukana tena mama samia eti ameiba kura na kwakua wao ndio waliotuaminisha anaupiga mwingi.
 
Back
Top Bottom