Ofisi ya ardhi kanda ya Magharibi (Tabora) iangaliwe


P

poteleambali

Member
Joined
Jul 23, 2015
Messages
45
Likes
22
Points
15
P

poteleambali

Member
Joined Jul 23, 2015
45 22 15
Ofisi hii imekuwa ikichelewesha kazi kwa makusudi huku watumishi wa ofisi hii hususan Msajili Msaidizi mwenyewe na baadhi ya wasaidizi wake kadhaa.

Kwao ni kawaida kuprocess mortgage kwa miezi, hata land search za kawaida ni zaidi ya wiki tatu hadi mwezi.

Yaani huyo Msajili awepo au asiwepo hakuna kinachoendelea, tena ukitaka kufuatilia huyu mama anakuwa mbabe na anaweza akaweka faili pembeni kabisa.

Sasa hivi ni kama mwezi wa pili Msajili hayupo, kuna bwana mmoja ambaye huwa ni kama msaidizi wa karibu wa Msajili, naye ni kama inaenda wiki ya tatu hayuko ofisini eti kaenda kufanya mitihani.

Sasa kama ni hivyo kwanini wasiache majukumu yao kwa watu wengine ili wananchi tusikose huduma?

Kwakweli waziri wa sekta hii tuomba uangazie ofisi hii manaake inapelekea hata raia kuilaumu sana serikali
 

Forum statistics

Threads 1,250,179
Members 481,248
Posts 29,723,322