Ofisi ya AG Yashtukia Kuzagaa Katiba Feki!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Zuhura Mmari na Grace Ndossa

OFISI Ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) imewata watu wanaochapisha, kusambaza kuuza na kugawa katiba za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 toleo la 2008 kusitisha shughuli hiyo mara moja kabla ya kuchukuliwa kwa sheria.

Taarifa hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Naibu AG ilisomeka kuwa umma unatahadharishwa wasinunue, kupokea au kutumia nakala za katiba hiyo za toleo la mwaka 2008 katika lugha ya kiswahili.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa toleo halisi la katiba iliyorekebishwa na iliyo katika lugha ya kiswahili ni la mwaka 2005 na siyo la mwaka 2008 kama ilivyoonyeshwa kwenye nakala feki.

"katika mwaka 2008 ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ilichapisha toleo moja la katiba katika lugha ya kiingereza tu na siyo katika lugha ya kiswahili," ilisomeka taarifa hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo ilieleza kuwa katika nakala hizo imeongezeka ibara ndogo ya (3) katika ibara ya 139 ambayo haipaswi kuwepo, pia rangi ya nakala na muonekano ni tofauti, na nakala halisi ina rangi ya zambarau iliyokolea wakati nakala feki ina rangi ya damu ya mzee (maroon).

Pia ilieleza nakala hizo hazina jina la mchapishaji na nembo ya Taifa iliyoka katika nakala hizo ni tofauti na nembo hali ya Taifa, kwa kuwa ile feki haina alama ya mlima Kilimanjaro

Pia katiba hizo zina tofauti katika mpangilio wa maelezo ya pembeni, katika nakala hizo kwani maelezo yako upande wa kulia tofauti na nakala halisi ambapo maelezo yapo upande wa kushoto.


Source: Majira.
 
Back
Top Bottom