Ofisa Usalama mstaafu afichua siri ya CCM kushindwa Mbeya

Wanatoa siri ambazo wenyewe wakiwa nje wanakana. Kumbe ccm inasaidiwa na TISS? Sasa huwa wanakana nini kuwa ni nguvu ya dola inayotumika?
Na sasa hivi tumeamriwa tuchukue kadi za vyama vya upinzani ili tuvuruge hivi vyama
 
Mbeya. Ofisa Usalama wa Taifa mstaafu, Said Salmin Said amefichua siri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kufanya vibaya katika uchaguzi.

Salmin aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, amesema hayo leo Jumapili Desemba 3,2017 akiomba kura ukumbini kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi uliofanyikia jijini Mbeya.

Amesema CCM mkoani Mbeya imekuwa haisikilizi na kufanyia kazi ushauri wa kitaalamu inaopewa na ndiyo sababu ya kufanya vibaya kwenye uchaguzi.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kuulizwa swali na mjumbe wa mkutano huo kwamba amekuwa kiongozi wa usalama wa Taifa mkoani Mbeya kwa miaka mingi, hivyo kutaka aeleze kwa nafasi yake alikisaidiaje chama hicho kupata maendeleo.

“Katika nafasi yangu nilikuwa mshauri kwa chama na nilitekeleza wajibu wangu kwa kukishauri, lakini tatizo likawa ni chama kutopokea na kupuuza ushauri na ndiyo sababu hakikufanikiwa,” amesema Salmin.

Amesema CCM mkoani Mbeya ina tatizo kubwa la makundi miongoni mwa wanachama, hali ambayo inasababisha kukosa umoja na mshikamano wa kuwakabili wapinzani wao.

Salmin amesema matatizo yote hayo anayatambua vizuri na kwamba endapo akichaguliwa kwa nafasi anayoomba, kazi yake kubwa ni kuyatatua.

Katika nafasi hiyo, Salmin alichuana na Dk Momole Kasambala, Jacob Mwakasole na Andilile Mwambalaswa.

Dk Kasambala amesema endapo atapata ridhaa ya kushika wadhifa huo atahakikisha anarejesha imani na kukusanya miradi ili kukuza uchumi wa chama hicho, lakini pia kuhakikisha kata zote zilizopo upinzani zinarejea CCM.

“Naomba mnipe ridhaa hii, nitahakikisha jimbo la Mbeya Mjini na kata zote ambazo zipo upinzani tunazirejesha mikononi mwa CCM,” amesema.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 CCM ilipoteza jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na Joseph Mbilinyi maarufu Sugu wa Chadema ambaye ameongoza kwa vipindi viwili mfululizo.

Pia, katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Ibighi wilayani Rungwe uliofanyika wiki iliyopita Lusubilo Simba wa Chadema alishinda kwa mara nyingine.

Chanzo: Mwananchi
Alianza lini kuwa kada wa chama cha siasa? Au ndio yale ya Jaji Mkuu mstaafu aliyewahi kuwa Brigedia?
 
Kwani.hata chadema si walituambia nusu ya idara nzima ya usalama wanaripoti kwao?
Huwezi kutenganisha chama tawala,na idara ya usalama wa taifa katika kupashana habari za kiinteljensia, acheni kujidanganya

Hata chadema wakiingia ikulu watatumia.tu idara kupata habari
Mohamed morsi alipoingia madarakani,aliamini mno makada wa chama chake,akafukuza mkuu wa majeshi,akafukuza mkuu wa usalama,akajiamini kwa kutegemea mizizi pekee ya chama chake

Kilichotekea ni Al-sisi kumwambia malizana kwqnza na wananchi wako halafu nikupe nchi,mwisho akampa siku7, lakini kwa kuwa hakuwa na watu wa intelijensia akafeli
 
Napta shida sana, yani mtu ni Dr. tena ofiosa usalama una anzaje kuanagaika na MACCM?
by the way hawa jamaa huwa wanastafu kumbe ?
 
Mbona liko wazi Tume huru police wakifanya kazi yao bila kuingiliwa na mtu yoyote CCM uwezekano wa kushidwa mkubwa sana
 
Nimewahi kuwaza hili kwamba inawezekana kabisa asilimia karibu na mia ya TISS ni makada wa CCM
 
Wanatoa siri ambazo wenyewe wakiwa nje wanakana. Kumbe ccm inasaidiwa na TISS? Sasa huwa wanakana nini kuwa ni nguvu ya dola inayotumika?
Kwa kila nafasi ya utumishi serikalini,utawajibika kutii sera,kutimiza ilani ya chama kinachotawala kikiwa CCM au NCCR mageuzi. Hiyo ndiyo kanuni.
 
Ungekua na akili sana kama ungetuwekea CV ya huyo jamaa na historia yake ili kuthibitisha kama kweli alikuwa mtu wa TISS ndio tujadili hayo mengine maana bila kuclear drought juu ya ofisi yake ya zaman tutaishia kulaum watu na taasisi zao tu
 
Bavicha wanaandika habari na kuitafsiri wenyewe.
 
Mbeya. Ofisa Usalama wa Taifa mstaafu, Said Salmin Said amefichua siri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kufanya vibaya katika uchaguzi.

Salmin aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, amesema hayo leo Jumapili Desemba 3,2017 akiomba kura ukumbini kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi uliofanyikia jijini Mbeya.

Amesema CCM mkoani Mbeya imekuwa haisikilizi na kufanyia kazi ushauri wa kitaalamu inaopewa na ndiyo sababu ya kufanya vibaya kwenye uchaguzi.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kuulizwa swali na mjumbe wa mkutano huo kwamba amekuwa kiongozi wa usalama wa Taifa mkoani Mbeya kwa miaka mingi, hivyo kutaka aeleze kwa nafasi yake alikisaidiaje chama hicho kupata maendeleo.

“Katika nafasi yangu nilikuwa mshauri kwa chama na nilitekeleza wajibu wangu kwa kukishauri, lakini tatizo likawa ni chama kutopokea na kupuuza ushauri na ndiyo sababu hakikufanikiwa,” amesema Salmin.

Amesema CCM mkoani Mbeya ina tatizo kubwa la makundi miongoni mwa wanachama, hali ambayo inasababisha kukosa umoja na mshikamano wa kuwakabili wapinzani wao.

Salmin amesema matatizo yote hayo anayatambua vizuri na kwamba endapo akichaguliwa kwa nafasi anayoomba, kazi yake kubwa ni kuyatatua.

Katika nafasi hiyo, Salmin alichuana na Dk Momole Kasambala, Jacob Mwakasole na Andilile Mwambalaswa.

Dk Kasambala amesema endapo atapata ridhaa ya kushika wadhifa huo atahakikisha anarejesha imani na kukusanya miradi ili kukuza uchumi wa chama hicho, lakini pia kuhakikisha kata zote zilizopo upinzani zinarejea CCM.

“Naomba mnipe ridhaa hii, nitahakikisha jimbo la Mbeya Mjini na kata zote ambazo zipo upinzani tunazirejesha mikononi mwa CCM,” amesema.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 CCM ilipoteza jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na Joseph Mbilinyi maarufu Sugu wa Chadema ambaye ameongoza kwa vipindi viwili mfululizo.

Pia, katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Ibighi wilayani Rungwe uliofanyika wiki iliyopita Lusubilo Simba wa Chadema alishinda kwa mara nyingine.

Chanzo: Mwananchi
Kumbe maafisa usalama wa taifa wakiwa kazini ni washauri wa ccm .duuhh basi siri kubwa hapa kwangu naiona ni hii ya usalama wataifa kuwa afisa usalama wa chama [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Hili li TISS ni linavujisha siri zao etiiiiiiiiiiiiiiiiiii hiii LA wapi hili boya
 
Back
Top Bottom