Ofisa Mipango Chamwino ajiua.... baada ya kumshika mke na lijamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisa Mipango Chamwino ajiua.... baada ya kumshika mke na lijamaa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by lifeofmshaba, May 27, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  fred.jpg
  alimaliza masomo korea miezi sita iliyopita
  fred 1.jpg Ofisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Fred Kaombwe (28), amejiua kwa kijipiga risasi kichwani baada ya kumkuta mkewe akiwa na mwanamume mwingine katika baa mojawapo mjini Dodoma.

  Baada ya hapo, Kaombwe inadaiwa alimkimbiza mkewe huyo Vicky Kaombwe (34) na baadaye alimpiga risasi na kumjeruhi sehemu za mbavu.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Elizabeth Masiaga alisema ,Kaombwe alijipiga risasi juzi saa 3.00 usiku katika mtaa wa Madole eneo la Kigamboni mjini Dodoma.

  Kamanda Masiaga alisema, Kaombwe alifariki dunia wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kupatiwa matibabu wakati mkewe Vicky amelazwa katika hospitali hiyo.

  Hata hivyo, hali ya majeruhi huyo anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana mjini Dodoma bado si nzuri na Kamanda Masiaga aliahidi kutoa taarifa zaidi mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

  Akizungumza na gazeti hili, mkwe wa marehemu, Thadei Nghwaya, alidai kulikuwa na ugomvi wa kifamilia na kwamba, Kaombwe alijipiga risasi kifuani na si kichwani baada ya kuhisi kuwa amemuua mkewe.

  Nghwaya alisema, baada ya vipimo, ilibainika na wataalamu kuwa risasi aliyojipiga Kaombwe ilipitiliza na haikubaki mwilini.

  Akizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina, mmoja wa mashuhuda alidai kuwa, kabla ya mauaji hayo Kaombwe alimkuta mkewe akiwa na mwanamume mwingine katika baa.

  Alidai kuwa, baada ya hapo, Vicky alikimbilia katika gari lake na kuondoka nalo huku akifukuzwa na mumewe katika gari lingine hadi walipofika nyumbani kwao eneo la Kigamboni.

  Shuhuda huyo alidai kuwa, Vicky aliposhuka katika gari kwa lengo la kufungua geti, Kaombwe alikuwa ameshafika akatoka ndani ya gari lake na kumpiga risasi mkewe.

  Kaombwe alisafirishwa jana kwenda Tabora kwa maziko.

  source: habari leo

  MAONI; sasa hapa kuna nafuu gani?
  anyway wamama na wadada jamani kuna wanaume ni dhaifu sio vizuri kuchakachua
  mali zao, wanaume kujiua kwa ajili ya penzi, inaingia akili kweli

  >>>>>>>>>>>HOT POST YA HII MADA

  Re: Ofisa Mipango Chamwino ajiua.... baada ya kumshika mke na lijamaa
  [​IMG] Originally Posted by Sikonge [​IMG]
  Bakantanda,

  Mie ni mpenzi wa kuangalia Investgestion Discovery (ID) TV. Kwa hayo uliyoyaandika hapo juu, huyu mama LAZIMA achunguzwe kwa uhakika zaidi. Inaonekana kuna njama zilishasukwa ili kummaliza jamaa. Haiwezekani wanaume wawili wanakufa kwa RISASI wakiwa na huyu mama. Panga pangua hapa kuna namna,

  Kama kuna watu wa karibu yake hasa usalama wa Taifa, basi huyu POLISI hawezi kabisa kuwa tishio kwenu. Fuatilieni hili tukio hadi kilichotokea hapo kijulikane. Msimuache huyu mama akaja kuuwa mwingine (kama ni kweli anahusika).

  RIP Kaombwe,,,,,,,,<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
  NA
  >>>>>>>>>>>>>LEONARDO>


  Upo sahihi kabisa mkuu, sema kwa tanzania yetu hii sijui kama marehemu atapewa haki yake, mimi nimeumia sana maana alikuwa a very close friend of mine. Cha kupigania kwa sasa ni walau wadogo zake ambao ni yatima wapate mgao wa mali za marehemu Fredy na alizoachiwa na wazazi wake kabla huyu mwnamke ajawadhulumu. Kweli si kila mwanamke wa kuoa.

  UPDATED 29.05.2011 new development on the story now police involved <<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

  Originally Posted by Sniper
  {Latest news nilizozipata ni kwamba Fredy hajajiua, Fredy ameuwawa na polisi dodoma. Mkumbuke mwizi wa Fredy ni polisi wa dodoma ambaye anasoma Chuo cha St.John, na siku ya tukio mwizi huyo (polisi) alikuwa na Vicky. Fredy alipigwa risasi ya ubavuni, sehemu ambayo ni ngumu sana kwa mtu kujipiga mwenyewe (na sio kifuani kama vyombo vya habari inavyoripoti), risasi iliyomuua Fredy haijapatikana eneo la tukio, simu ya marehemu haijulikani ilipo na Vicky hajapigwa risasi hata moja kama vyombo vya habari vinavyoripoti.

  Hii yote inaonesha kwamba habari iliyotolewa kwenye vyombo vya habari na polisi ni ya uzushi na uongo mtupu. Kwakuwa mmoja wa watuhumiwa ni polisi, na Polisi imeanza kwa kutoa habari zisizo za kweli kuhusu tukio zima, Polisi pia hatuwaamini katika uchunguzi wa kifo cha marehemu.

  Naomba kama kuna ndugu wa huyo polisi au Vicky wanapita hapa JF muwa taarifu kabisa kwamba maisha yao yako hatarini, Watu wa dodoma wana hasira na uchungu sana na kifo cha Fredy.
  ]
  <<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

  Originally Posted by Gagurito
  ebwana huyu bwana tunaishi nae jilan hapa kitaani, magorofa mengi kikuyu! Huyo mwanamke huyu ni mume wake wa 3 kati ya wa4 kufariki tena kwa kupigwa au kujipiga risasi. Mmoja aliyenusurika mpaka sasa ni chizi, mwili wa jamaa keshasafirishwa kwenda tabora kwa mazishi. Mungu ampumzishe mahala pema!<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

  Hapa sasa patamu, sijui kama INVISIBLE unaweza kusaidi wengine mikono yetu iko mbali na eneo la tukio,
  wanajamvi wa DODOMA , tunaomba DATA Tafadhali
   
 2. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kwamba watu wengine maumivu ya kimapenzi wanashindwa kuyahimili na kuchukua hatua hii.
   
 3. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ni kweli bora kufukuza tu, huo ukimwi kuliko kujiua sasa ndio jamaa kabaki hapa dunia anakula matunda kwa raha zake
   
 4. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Dahhhhh kweli mapenzi kizungu zungu..mapenzi ni wivu na mapenzi yana uwa..
   
 5. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yaani naomba kikombe hiki kiniepuke
   
 6. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
   
 7. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 8. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
   
 9. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Kuna vitu maishani vinashangaza. Ila we are part of it
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hii haiwezekani bana! Toka lini wanawake wameanza kuchiti? Wanawake huwaga hawachiti bana. Huyo jamaa maisha tu yamemshinda na akaamua kujiua sasa wanamsingizia infii mkewe.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Unajiua bcoz of fvcking chick? aisee mie siezi fanya huo ujinga.
   
 12. RR

  RR JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  sad....hiyo ndo inaitwa kupenda upande mmoja sio...damn!
  Dogo kajiua akiwa na miaka28, wakati mke ana miaka 34....!
   
 13. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Inaonekana dogo aliolewa na huyo mama, 28 kwa 34!!! ndio maana wivu kibao..
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mi bado nakataa bana. Wanawake huwaga hawachiti.
   
 15. s

  sugi JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  we we weeee,ishia hapo hapo,ndo unavyojidanganya hivyo,mimi tu hapa mke wa mtu kaniganda mbaya,huwa nachakachua kiaina,sasa hawachiti vp?au waolewe kabisa mara mbili?
   
 16. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,177
  Likes Received: 1,180
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana mtu anapoamua kujidhulum uhai wake, Fred was my classmate enz za o levo na alikuwa na udhaifu wa mapenzi tangu kipindi icho.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wanawake hawachiti bana. Huo ndo ukweli wenyewe. Jamaa alikuwa na wasiwasi wa bure tu.

  Sijawahi kabisa mimi kuona mwanamke anayechiti. Hata hapa uliza hawa akina dada waliopo hapa JF watakwambia.
   
 18. s

  sugi JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Ngabu,u cant be serious,women?"they are warry transgrassors"thats why they look so inocent
   
 19. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ..........inasikitisha, ila dawa ya mtu anayecheat ni kumuacha na kuendelea na maisha yako. Kujiua wala sio uamuzi wa busara, sasa yeye kafa bado mdogo masikini dahhhhh!!! Ila huyo mama naye hatoishi kwa furaha tena kusababisha mtu kufa si jambo dogo atiii!!!
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ebwana huyu bwana tunaishi nae jilan hapa kitaani, magorofa mengi kikuyu! Huyo mwanamke huyu ni mume wake wa 3 kati ya wa4 kufariki tena kwa kupigwa au kujipiga risasi. Mmoja aliyenusurika mpaka sasa ni chizi, mwili wa jamaa keshasafirishwa kwenda tabora kwa mazishi. Mungu ampumzishe mahala pema!
   
Loading...