Ofisa JWTZ ahofiwa kutorokea Rwanda

Naona Kagame yupo serious sana na program yake ndani ya Tanzania kuna mwingine ametimuliwa miaka kama miwili tu iliyopita kutoka pale DUCE. Kwahakika hawa jamaa wapo kwenye kila taasisi ya Tanzania, nashangaa ni kwanini watanzania hatujawa na uwezo wa kupenyeza intelligence yetu nchi za nchi lakini Kagame kawajaza kila mahali kiasi cha kwamba wanaua yeyote wanayemtaka kwa muda wanaojisikia kana kwamba wapo nchini kwao, kama walivyofanya kwa Prof. Mwaikusa. Sina shaka kwamba Kagame anajua kwamba ana timu ya kutosha ndani ya jeshi la Tanzania ndiyo maana anajivuna kwamba atampiga Kikwete.
 
Daudi Mchambuzi, hapa mimi sioni kama tatizo ni Kikwete, maana huyu mtu hadi amefikia cheo cha luteni kanali, ni dhahiri kwamba alikuwepo jeshini siku nyingi. Sasa hapa cha kulaumu ni mfumo wetu wa uandikishaji wa watu kwenye sekta nyeti kama hizi. Nafikiri kungekuwa kuna utaratibu kabambe wa kuhakikisha ufuatiliaji wa maisha ya mtu kwa vizazi kadhaa kabla ya kumuingiza kwenye sekta nyeti kama hizi. Hivi tunajua kuna wanyarwanda wangapi ni usalama wa Taifa? Lakini pia najiuliza, hizo documents ambazo huyu jamaa kakimbia nazo zitakuwa ni za aina gani? Na ni za hatari kiasi gani kwa usalama wa nchi yetu?
 
Last edited by a moderator:
Alafu tunajisifu eti tunajeshi imara?aibu kweli kweli

Mkuu mimi sina wasi wasi wowote kuhusu uimara wa JWTZ,mambo ya wanajeshi kutoroka au kusaliti Taifa lao yapo dunia kote - mimi nafikili Mnyarwanda huyo katoroka baada ya kung'amua nyenendo zake za kijasusi zinakaribia ukingoni i.e yuko karibu kutiwa mbaroni na watu wa usalama - swali ni Je nani kampa tipoff? Kuna uwezekano mkubwa kwamba jamaa hawa wamekwisha compromise baadhi ya watumishi wa vitengo vyetu nyeti! Kwa usalama wetu, JK anapashwa kufanya reshuffle kali sana na kuwaondoa jamaa hawa bila ya kujali lawama (hata wakiwekwa kwenye makambi au warudishwe kwao) vile vile Viongozi walio katika Mikoa ya Kagera na Kigoma wahamishiwe mikoa mingine ambako hawajazoeleka sana na zoezi hili lifike mpaka viongozi kwenye grass root level, bila ya kufanya hivyo zoezi zima la kuwarudisha makwao wahamiaji haramu litakuwa sawa sawa na hakuna.

Mkoa wa Kagera kwa mfano: Takwimu zinaonyesha wahamiaji haramu wanakaribia 60,000 na ushee leo hii wanasema waliorudi makwao ni 8,000 plus tu wengine wamekimbilia mikao ya jirani kwa muda, baadae watarudi tena! One gets the impression Wanyarwanda hawa wana agenda ya siri, kwa nini wanakuwa vig'ang'anizi na hawataki kuhamia nchini mwetu kihalali kwa nini? Sisi tunao toka kwenye Mkoa unao pakana nao tumekwisha choshwa na tabia zao zisizo za kistaarabu na kukosa kwao shukrani. Taifa letu likiwalazia damu watatumaliza kilahini.

Binafsi namshukuru sana Mh.JK kwa kutamka kwamba hawezi kupuuzia kauli za PK na vitisho vyake - that guy means business si wa kupuuzia na inaonekana amekwisha infiltrate watu wake wa kijasusi wengi tu kwenye Taifa letu, ndio maana anazungumza kwa kujiamini kupita kiasi - nchi kama Uingereza iliwahi kuwatia mbaroni majasusi wa Kinyarwanda walio kwenda nchini humo kuwamaliza wapinzani wa PK, bila ya kujali kwamba Waingereza ni mahili katika ujasusi (MI6 na MI5), kama Wanyarwanda wanaweza kuwa na ujasiri kiasi hicho cha kujaribu kufanya uharifu wao nchi za Ulaya - Je nchi za Kiafrica zina usalama GANI - ukitilia maanani tamaduni zetu za kuchukulia mambo ki-laissez faire?? Mimi nina mashaka sana na Wanyarwanda walio hamia nchini mwetu miaka ya 1957/58 Mkoa wa Kagera/Kigoma hasa hasa Kagera nafikili hao ni rahisi kutumiwa na utawala wa Rwanda ku-recruit Watutsi wenzao waliyo kwenye vitengo nyeti ndani ya Serikali kufanya mambo ya ujasusi - lika hilo lifatiliwe kwa karibu SANA - jamaa hawa wana mtandao mkubwa nawa hatari.

Taifa letu lisije likabweteka Wanyarwanda specifically ABATUTSI will always owe allegiance to their country of origin i.e hawasahau kwao - wahulize wenyeji wa Karagwe watawaeleza mambo mengi, wala mimi siamini kwamba kauli ya Mh.Kikwete ndio ilimfanya PK kuja juu, mbona wanamsema mambo mengi tu lakini anakaa kimya, inawezekana kuna kitu aliwahi kufahamishwa na mtandao wake siku za nyuma kutuhusu sisi lakini alihamua labda kukakaa kimya akitafakali moyoni mwake nini la kufanya, sasa alipo changanya na Ushauri wa Mh.JK ndio maana PK akaripuka!!! He was visibly angry and indignant - kuna kitu pale, si bure.

Nilisha sema/onya sana kwamba Jamaa hawa ni mahili sana katika kutekeleza plan zao, si watu wa kupuuziwa, leo hii kwa mfano mkuu wa kikosi sijui platoon cha jeshi ya Kabila Jr katoroka jeshi la Serikali ya DRC akiwa na wapiganaji zaidi ya hamsini wakaenda na kujiunga na jeshi la waasi i.e M23 (Jeshi la Rwanda) je unajua kaondoka na siri gani kupeleka Kigali ambazo zinaweza kuweka vikosi vyetu vya umoja wa Mataifa kwenye hali ngumu?
 
mwamunyange%20davis.jpg

Mkuu wa JWTZ, Meja Jenerali Davis Mwamunyange

*Adaiwa kutoweka na nyaraka nyeti
OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili ya Rwanda, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, huku akiacha wingu la mashaka kwamba, hatua yake hiyo inaweza ikawa imeambatana na kupotea pia kwa baadhi ya taarifa muhimu za kijeshi.

Taarifa za kutoweka kwa ofisa huyo mwenye cheo cha luteni kanali, zinalihusisha tukio hilo na hatua za makachero wa JWTZ kufuatilia nyendo zake na zililifikia gazeti la MTANZANIA Jumapili kwa mara ya kwanza katikati ya wiki hii.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa, tayari maofisa wa JWTZ wameshaanza kufuatilia kwa karibu tukio la kutoweka kwa ofisa huyo, ambalo pia limezusha hali ya sintofahamu kwamba, huenda akawa ameondoka na nyaraka nyeti za kijeshi.

Kabla ya kutoweka ofisa huyo, ambaye nyendo zake zimekuwa katika darubini kali za makachero wa JWTZ, alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).

Hatua ya kutoweka kwa ofisa huyo wa juu wa JWTZ anayetajwa kwa jina moja la Selumbo, imekuja siku chache tu baada ya kuibuka kwa msuguano wa kauli baina ya Ikulu ya Dar es Salaam na ile ya Kigali.

Chanzo cha msigano huo wa maneno uliogeuka na kuwa mzozo wa kidiplomasia, ni ushauri uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Rais Paul Kagame wa kumtaka awe tayari kukaa meza moja na waasi wa kundi la FDLR wanaopigana Rwanda, kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tayari msigano huo wa Kikwete na Kagame umeanza kutajwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa tishio kubwa la kwanza la ustawi, uimara na misingi ya mshikamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo mataifa hayo mawili ni wanachama wake.

Siku chache baada ya ushauri huo, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Rwanda akimkejeli Kikwete, hata kufikia hatua ya kutoa kauli zenye mwelekeo wa vitisho dhidi yake.

Kauli hizo za Kagame zilisababisha Rais Kikwete, kupitia katika hotuba yake ya mwishoni mwa Julai, kujibu mashambulizi, huku akieleza bayana kushangazwa na kushtushwa na kejeli na matusi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.

Akitumia maneno ya kidiplomasia ambayo yametafsiriwa na baadhi wa wachambuzi wa masuala ya diplomasia na sayansi ya siasa kuwa yanabeba ujumbe mzito, Rais Kikwete alisema alikuwa amesikia yote yanayosemwa kutoka Rwanda na alikuwa hakusudii kuyapuuza.

Kauli hiyo ya Kikwete ambayo ilitanguliwa na ile aliyoitoa siku chache mkoani Kagera ya kuwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini, ilifuatiwa na matukio ya kuondoka nchini kwa Wanyarwanda wanaokadiriwa kuzidi 5,000.

Wakati hali ikiendelea kuwa ni ya mashaka na kutoaminiana kati ya Tanzania na Rwanda, katikati ya wiki hii, gazeti dada la MTANZANIA Jumatano, lilikuwa na habari kubwa yenye kichwa cha habari kisemacho; ‘Nini kinamtia Jeuri Kagame?’ ambayo pamoja na mambo mengine, ilieleza namna watu wenye asili ya Rwanda walivyojipenyeza katika taasisi mbalimbali nyeti za umma.

Kuvuja kwa taarifa za kurejea Rwanda kwa maelfu ya wahamiaji haramu sambamba na hizi za sasa za kutoweka kwa ofisa wa juu wa JWTZ kunathibitisha kuhusu kuwapo kwa mwelekeo huo wa mambo.

Vyanzo vya habari vya gazeti hili, vinamtaja ofisa huyo kuwa ni mmoja wa makachero wenye asili ya Rwanda waliokuwa wakifanya kazi ndani ya JWTZ na ambao wanahofiwa kuwa watu wenye mawasiliano ya karibu na serikali ya Rwanda, kwa malengo ambayo bado hayajawekwa bayana.

“Ni kweli, huyo ofisa ametoweka jeshini na sijui sababu zilizo nyuma yake…hili suala la kuwa anakusanya taarifa za siri za jeshi letu na kuzipeleka Rwanda nadhani ziligunduliwa na watu wetu ambao wapo kwenye mfumo wa kijeshi,” alidokeza mmoja wa watoa taarifa wa MTANZANIA Jumapili.

Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alishindwa kukubali au kukataa, kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo ni zito hivyo alikuwa akipaswa kuzungumza kwanza na viongozi wake kabla ya kulitolea taarifa.

Meja Komba alieleza kuwa, wanajeshi wanaotoroka ni wengi na wapo waliofungwa kwa kosa hilo la utoro.

“Jamani suala hili ni zito, naliogopa, nyinyi hamlioni kama ni zito? Sio kwamba sipendi wananchi wapate habari, suala hili tupeni muda kwanza tulifanyie ‘analysis’, mbona wanajeshi wengi wanatoroka na hamripoti! Waliotoroka ni wengi, wangine wametorokea Rwanda na kwingine na wamefungwa.

“Ni lazima kwanza niongee na mabosi wangu ndiyo nizungumzie vizuri hili… njoo ofisini Jumatatu (Kesho),” alisema Meja Komba.

Sanjari na tukio hilo, taarifa zaidi zilizonaswa na gazeti hili zimedai kuwa sasa imebainika pasipo shaka kuhusu kuwapo kwa makachero wa Serikali ya Kigali wanaodaiwa kupandikizwa katika taasisi na idara nyeti za serikali kwa ajili ya kufanya ushushu kwa maslahi ya Rwanda.

Inadaiwa kuwa intelijensia ya JWTZ iliyo na mizizi ndani na nje ya nchi ilibaini mapema kuwapo kwa majasusi wa Kinyarwanda ndani ya mfumo wa dola na nyendo zao zimekuwa zikichunguzwa kwa muda mrefu na zilibainisha hali hiyo.

Watusi wapo wengi sana na imani serikali wanalijua hilo. Jinsi wanavyoshughulikia ndio hatuwezi kujua. Kwenye vyuo vyetu wapo kibao. Mlimani moja alipewa nafasi nyeti lakini waliokosa ile nafasi wakapiga kelele na kweli akatolewa. Jamaa zao wengi hata kwa kuangalia tu ndio hao hao.

Wakati fulani nilishangaa jamaa ambao tulikuwa nanakaa sehemu moja kila wakati mpirani, wakati wa CEFACA mwaka fulani uzalendo ukawashinda ndio tukajua kumbe watusi lakini tunaishi nao mitaani kama watanzania.

Tusimpuuze Mtikila kwa hili. Lakini najua pekuapekua ya hawa jamaa haiwezi kuwa ya wazi kihivyo. Bila shaka serikali yetu inawafuatilia chinichini. Kitu cha msing zoezi la vitambulisha vya taifa lisaidie katika hilo. Ni vizuri wakatangaziwa kabisa kwamba kutoa taarifa za uongo ni kosa wakati wakujisajili. Baadae inaweza kuwa njia nzuri ya kuwabana na kuwasweka ndani kama watachukua vitambulisho vya utanzania wakati wanajua kuwa sio raia. Wachni wavamie tu kwanza tupate sababu ya kuwafunga baadae.
 
Kumbe ndiyo maana kajamaa kana kidomo domo sana! Yaani mpaka mamluki anafikia cheyo cha Luteni Kanali hagunduliki tu?? Naanza kupata wasiwasi na intelijensia ya JWTZ.

Siyo rahisi mkuu! Yawezekana huyu askari amezaliwa hapa hapa na kusomea hapa; inawezekana babu au baba yake na huyu askari walikimbia ile vita ya kwanza ya akina Michombero or the like hata kabla sisi kupata uhuru wetu so si rahisi kumtambua. Yawezekana sura yake inaonyesha kuwa na asili ya Rwanda, hapo tatizo ndipo linapoanzia.
 
mwamunyange%20davis.jpg

Mkuu wa JWTZ, Meja Jenerali Davis Mwamunyange

*Adaiwa kutoweka na nyaraka nyeti
OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili ya Rwanda, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, huku akiacha wingu la mashaka kwamba, hatua yake hiyo inaweza ikawa imeambatana na kupotea pia kwa baadhi ya taarifa muhimu za kijeshi.

Taarifa za kutoweka kwa ofisa huyo mwenye cheo cha luteni kanali, zinalihusisha tukio hilo na hatua za makachero wa JWTZ kufuatilia nyendo zake na zililifikia gazeti la MTANZANIA Jumapili kwa mara ya kwanza katikati ya wiki hii.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa, tayari maofisa wa JWTZ wameshaanza kufuatilia kwa karibu tukio la kutoweka kwa ofisa huyo, ambalo pia limezusha hali ya sintofahamu kwamba, huenda akawa ameondoka na nyaraka nyeti za kijeshi.

Kabla ya kutoweka ofisa huyo, ambaye nyendo zake zimekuwa katika darubini kali za makachero wa JWTZ, alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).

Hatua ya kutoweka kwa ofisa huyo wa juu wa JWTZ anayetajwa kwa jina moja la Selumbo, imekuja siku chache tu baada ya kuibuka kwa msuguano wa kauli baina ya Ikulu ya Dar es Salaam na ile ya Kigali.

Chanzo cha msigano huo wa maneno uliogeuka na kuwa mzozo wa kidiplomasia, ni ushauri uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Rais Paul Kagame wa kumtaka awe tayari kukaa meza moja na waasi wa kundi la FDLR wanaopigana Rwanda, kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tayari msigano huo wa Kikwete na Kagame umeanza kutajwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa tishio kubwa la kwanza la ustawi, uimara na misingi ya mshikamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo mataifa hayo mawili ni wanachama wake.

Siku chache baada ya ushauri huo, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Rwanda akimkejeli Kikwete, hata kufikia hatua ya kutoa kauli zenye mwelekeo wa vitisho dhidi yake.

Kauli hizo za Kagame zilisababisha Rais Kikwete, kupitia katika hotuba yake ya mwishoni mwa Julai, kujibu mashambulizi, huku akieleza bayana kushangazwa na kushtushwa na kejeli na matusi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.

Akitumia maneno ya kidiplomasia ambayo yametafsiriwa na baadhi wa wachambuzi wa masuala ya diplomasia na sayansi ya siasa kuwa yanabeba ujumbe mzito, Rais Kikwete alisema alikuwa amesikia yote yanayosemwa kutoka Rwanda na alikuwa hakusudii kuyapuuza.

Kauli hiyo ya Kikwete ambayo ilitanguliwa na ile aliyoitoa siku chache mkoani Kagera ya kuwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini, ilifuatiwa na matukio ya kuondoka nchini kwa Wanyarwanda wanaokadiriwa kuzidi 5,000.

Wakati hali ikiendelea kuwa ni ya mashaka na kutoaminiana kati ya Tanzania na Rwanda, katikati ya wiki hii, gazeti dada la MTANZANIA Jumatano, lilikuwa na habari kubwa yenye kichwa cha habari kisemacho; ‘Nini kinamtia Jeuri Kagame?’ ambayo pamoja na mambo mengine, ilieleza namna watu wenye asili ya Rwanda walivyojipenyeza katika taasisi mbalimbali nyeti za umma.

Kuvuja kwa taarifa za kurejea Rwanda kwa maelfu ya wahamiaji haramu sambamba na hizi za sasa za kutoweka kwa ofisa wa juu wa JWTZ kunathibitisha kuhusu kuwapo kwa mwelekeo huo wa mambo.

Vyanzo vya habari vya gazeti hili, vinamtaja ofisa huyo kuwa ni mmoja wa makachero wenye asili ya Rwanda waliokuwa wakifanya kazi ndani ya JWTZ na ambao wanahofiwa kuwa watu wenye mawasiliano ya karibu na serikali ya Rwanda, kwa malengo ambayo bado hayajawekwa bayana.

“Ni kweli, huyo ofisa ametoweka jeshini na sijui sababu zilizo nyuma yake…hili suala la kuwa anakusanya taarifa za siri za jeshi letu na kuzipeleka Rwanda nadhani ziligunduliwa na watu wetu ambao wapo kwenye mfumo wa kijeshi,” alidokeza mmoja wa watoa taarifa wa MTANZANIA Jumapili.

Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alishindwa kukubali au kukataa, kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo ni zito hivyo alikuwa akipaswa kuzungumza kwanza na viongozi wake kabla ya kulitolea taarifa.

Meja Komba alieleza kuwa, wanajeshi wanaotoroka ni wengi na wapo waliofungwa kwa kosa hilo la utoro.

“Jamani suala hili ni zito, naliogopa, nyinyi hamlioni kama ni zito? Sio kwamba sipendi wananchi wapate habari, suala hili tupeni muda kwanza tulifanyie ‘analysis’, mbona wanajeshi wengi wanatoroka na hamripoti! Waliotoroka ni wengi, wangine wametorokea Rwanda na kwingine na wamefungwa.

“Ni lazima kwanza niongee na mabosi wangu ndiyo nizungumzie vizuri hili… njoo ofisini Jumatatu (Kesho),” alisema Meja Komba.

Sanjari na tukio hilo, taarifa zaidi zilizonaswa na gazeti hili zimedai kuwa sasa imebainika pasipo shaka kuhusu kuwapo kwa makachero wa Serikali ya Kigali wanaodaiwa kupandikizwa katika taasisi na idara nyeti za serikali kwa ajili ya kufanya ushushu kwa maslahi ya Rwanda.

Inadaiwa kuwa intelijensia ya JWTZ iliyo na mizizi ndani na nje ya nchi ilibaini mapema kuwapo kwa majasusi wa Kinyarwanda ndani ya mfumo wa dola na nyendo zao zimekuwa zikichunguzwa kwa muda mrefu na zilibainisha hali hiyo.

Jeekay katuletea matatizo sana ya kuanzisha ugomvi na watusi nooma
 
Siyo rahisi mkuu! Yawezekana huyu askari amezaliwa hapa hapa na kusomea hapa; inawezekana babu au baba yake na huyu askari walikimbia ile vita ya kwanza ya akina Michombero or the like hata kabla sisi kupata uhuru wetu so si rahisi kumtambua. Yawezekana sura yake inaonyesha kuwa na asili ya Rwanda, hapo tatizo ndipo linapoanzia.

Naunga Mkono hoja.
 
kwa suala hili mbona lipo , tena inawezekana wako wengi tu hata dogo mmoja aliwahi kufukuzwa jeshini kumbe ana asili ya rwanda na baadaye alisepa yupo rwanda jina EUGENE NZEYIMANA eti wa manyovu kgm kumbe hamna lolote. tena walimstukia depot na cheti kilikuwa si chake , ila alisomea bongo akafeli form 4. kwa kigoma ndiyo wengi . mngine alianzisha na NGO,s ya NWB(neighbour without border) ilikuwa based kgm karibu na depot ya TOTAL, sasa hivi nasikia ni waziri rwanda . Kwa hiyo serikali inahitaji umakini mno katika hili . kigoma inabidi wachunguze hasa maana inaonyesha ndiyo kitovu cha haya majamaa na wengi wanakimbilia makanisani hasa roman catholic.
 
Alipandaje hadi ngazi hiyo,vetting ina maana gani?haya bwana serikali yetu na vyeo vya kishkaji hadi jeshini
 
Hili la kuwa na Wanyarwanda na watu wa Malawi wengi kwenye sekta nyeti humu nchini lilishazungumziwa humu. Tuwe makini.

sijui wakiondoka wote kwa pamoja: wajaluo na wakurya ambao ni mapandikizi ya Kenya, wahaya feki ambao ni waganda, wanyasa na makabila la kusini ambao ni wa zambia na wamalawi, warundi na wanyarwanda wote wakasaidi nchi zao..tubaki na wakwere, wapemba wenye wake wa kisomali etc...
 
Mtikila watu wanamwonaga punguani! Lakini mimi sijawai kumpuuza ata siku mmoja, ona jinsi Gagame alivyo tokwa na pofu katika kuujibu ule waraka wake.

Humu JF si kila mtu kil amtu anayesema kitu vichwa maji wa kitanzania wanaojiona wana akili wanchokiogopa basi nji arahisi ni kuita wengine mapunguani, wajinga, viroba etc biahsra ya Lumumba imekwishwa.

Mlaya wengi wa kibongo wanashida vitu kibao vya maafisa wetu wa jeshi wasiojua computer vizuri...malaya wengi tuu bil akujali nchi zao wanaachiwa nyumba za maafisa wetu wa jeshi.
 
Mbona hii ni kwaida jamani? Unafikiri hakuna hata watanzania ktk majeshi ya jirani? msitake kuamplify hii issue ionekana as if ndo tmevamiwa nk. Ni kawaida ushushu kati ya nchi na nchi kuwepo. Inaweza kuhusu technologia, ulinzi nk. Wewe unafikiri wachina au wafaransa nk wanafanya nini kama wakitaka kupata technology ya wa wamerakani? Sisi tubakie kuuza madawa na labda kuuza mbinu za kupitisha madawa ya kulevya katika baadhi ya viwanja vya ndege!! Shame on us

sidhani km ni rahisi flash system kirahisi hivyo..na hata km ingekuwa rahisi sijui km ni rahisi kuflus project proposals za projects ambazo ndizo zinaanza sasa hivi baada ya kupitishwa na kutafutiwa hela...

Ach aku symplify issue kirahisi hivyo kijana mwenye akili na matumaini ya Lumbumba...hata mwigulu alipokuwa kiwaadithia Lumumba jinsi anakwenda mmaliza Dr.Slaa walimshangilia...ila na CDM waliposema kuwa kuna hujuma mliacha cheka kuwa wasikilizie kichapo.Ila baada ya CDM kubadili time kidogo tuu Mwigulu akageuka kituko na Lumumba yote panic.
 
Halafu kuna uzi uliletwa hapa kwamba, hata mke wa kigogo mmoja wa POLICCM ni Mtusi toka ukoo wa Kagame, huku akiwa na mishughuliko inayo tia shaka!!!

Tanzania itaponea wapi, maana hizi taasisi za ulinzi karibu zote zimejikita kuhangaoka na CHADEMA huku nchi ikiwa shakani?

haha..mbaya pia hawaambiliki kabisa..ukizidi waambia wanakomaa kuwa wewe si mzalendo au CDM ..CCM wamewalipa upumbavu wa kutosha,kiasi cha kuwafanya wajisikie kuwa CDM ndio hatari kwa nchi.Ila ukweli we are going to be stmped down.
 
Ndugu usiogope Mtu mwenyewe kumbe wa IT situnaflsh maprogram yote kijeshijeshi tunaanza upya -Mi ningeogopa sana kama angekuwa mkuu wa pale Ngelengele au Monduli

Na project plans amabzo zinaanza fanyika nazo mtaflush wakati jamaa keshawepelekea hadi map, na size?Kwani lazima uwe ngerengere ili upate docuemnetion , na plans za extention?Kw ataarifa yako kuna report nyingi sana zipo well detailed za project mpya hulu ziielezea zilizopo. majeshi yetu yanatembea nazo ktk laptops, tena wanaancha kwa vile wanajua watu wanawaogopa sana, na hata huwapa mafunsi kibaduzi hivyo hivyo km wafanyavyo kikabila humo ktk majeshi..Madai yao watu wa kaskazini hawastahili kuwa majeshi,usalama wa taifa etc..sasa wekeni majinga ..mshuhudie haya..mijitu inapigwa na wake zao na ubabe wao wote, ni vipi sasa watazuia wife asipoteze docs?

Sijui taasis ngapi bongo zinauza used deviced bila kutoa n akuharibu memmory km hard disks.
 
Hapa inatakiwa watu wawajibike sana!
Inawezekenaje akatoroka wakati jeshi letu limekuwa likimfuatilia? Nani kamtorosha na wahusika wa hilo tukio wako wapi?
Kuna maswali mengi yanayotakiwa kujibiwa!

Yes, your are right! All the above questions have to be answered analytically!
 
Hapa inatakiwa watu wawajibike sana!
Inawezekenaje akatoroka wakati jeshi letu limekuwa likimfuatilia? Nani kamtorosha na wahusika wa hilo tukio wako wapi?
Kuna maswali mengi yanayotakiwa kujibiwa!

Haha....umewahi jiuliza saga lilipoanza "KUNA JAMAA KAGAME WALIKUWA AKIMTAKA NA MAHAKAMA ZA KIMATAIAFA PIA" akatoka kongo na kuja dar kuongea na kiongozi wa Tanzania, wakati anarudi makomando wa Rwanda wakamchukua mpakani.Ni wazi kuwa hata huyo km amefika mpakani watakuwa wamemvusha..anaweza pitia kongo kampala kutoke anairobi na bishara ikaisha.
 
Back
Top Bottom