OFFICIAL : Samsung watoa simu yenye 7000mAh muda mfupi uliopita(M51)

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
6,661
20,997

Kwa mara ya kwanza Katika ulimwengu wa kampuni KUBWA na MAARUFU za Simu(Tuelewane hapo, usikimbilie ligi uje unitajie Doogee, Energizer au ulefone).

Hatimaye leo mchana samsung ametoa ingizo jipya katika series yake ya 'M', series inayojuulikana kwa kutoa simu zenye battery kubwa.
Hii ni Samsung M51 yenye ukubwa wa 7000mAh,huko German.

Ni mwezi haujapita ter 6 mwezi huu alitoa M31s yenye 6000mAh, na hapo nyuma alikua na M30s, M31 zote zikiwa na 6000mAh.

Ili kuokoa mda wanakupa fast charge ambayo itahitaji takribani saa moja na nusu kuijaza charge,
Ukiachana na Battery ambayo ndio inayoitambulisha hii simu zaidi, tukiangalia specs nyingine tunaona....

Camera 4 za nyuma, ikiwemo ya 64MP
Selfie ya 32MP

Processors ya pekee katika M-series maalumu kwa ajili ya gamingkutoka katika kampuni ya kimarekani Qualcomm Snapdragon 730G, katika mid range smartphone hii si haba.
High build quality wakitumia
Glastic(glass+plastic) katika rangi mbili nyeusi na nyeupe.
Display : full HD+ Super Amoled + infinity - O display.
RAM 6/8GB(market dependable)
Storage 128GB,

Kioo cha 6.67 inch
Face unlock na side fingerprint
Na specs nyingine nyingi..

Naomba ieleweke, hii ni MID range smartphone SI flagship, na kwa kujua kuna wapenda ligi humu pia ieleweke sijasifia simu, sijasema ni the best bali nimetaja specs zake, hasa hasa nikilenga battery..
Najua na Unajua kuna simu bora zaidi ya hii nyingi tuu.

Bei ni Tsh laki 9,
Ni Hayo tuu kwa wapenda simu zenye battery kubwa.
 
Sawa kongole kwao.....sisi wa mbagala tunaisubili ishuke maana iyo mia tisa si ni bei ya jumla maana huku itakuwa kwenye milioni na.......
 
Inapatikana globally au India tu kama kawaida ya m series zote
 
Mkuu nataka kuagiza Doogee N20 ram 4, ROM 64, rear camera 16MP na front 8 kwa 218000/=

Na kuna ule phone ina specifications kama izo kwa 237000/=

Nipe neno Mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…