Off we Go!

QM,
katika maswala ya mashuzi kama hayo mkuu wala usihangaike sanaa... kifupi ilikuwa ktk kuwaonyesha vijana tuliweza kuyarudi vipi... ingawa ndio walituona kama vile watu wa msituni tukipandisha mashetani..
Kitu kimoja tu lazima nikisema, haikuwa oldschool kwetu sisi maanake nyimbo nyingi zilikuwa kati ya 1988 hadi 90s.. huko kwetu sisi waligusagusa tu.. hata hivyo haikuchusha sana, Ma DJ hawakuchusha sana kama maandilizi yenywe, huko wala sitaki kwenda kabisa maanake duh! ilikuwa aibu..
Meeting U fellas, was worth every penny and time!
 
All I can say I had a heck of a weekend and it was fun to see
so many people together and happy!!!

One love always and let there be more meetings!!!

Enjoy the pics!

n1246250343_30089930_8936.jpg

n1246250343_30089931_9808.jpg

n1246250343_30089933_1773.jpg

n1246250343_30089928_6203.jpg
 
yes sir... QM.. ile wheelchair ilikuwa kasheshe kuingiza pale ndani... uzuri wa hizi za umeme wewe unashika kile kifimbo tu!! Ila wazee nimewaheshimu sana kwa uwepo wenu pale na zaidi nilivua kofia nilipoona wazee kama mimi.. mzee Mkandara akijirusha katika miondoko ya kilatino...
 
Ila wazee nimewaheshimu sana kwa uwepo wenu pale na zaidi nilivua kofia nilipoona wazee kama mimi.. mzee Mkandara akijirusha katika miondoko ya kilatino...

Haaa! haaa! haaa! mzee na wewe hukuwa nyuma ulinipa Chacha la nguvu..

Yaani kifupi dogo Bon Love na Luka bado hawakuweza kuniinua mimi kitini. Pale walitakiwa kina Gerry Kotto, John Peter Pantalakis, Seydou, Chris Phabby, Joe tukiwaacha nje marehemu kina Choggy Sly, Kalikali na Eddy Sally... hawa ndio ma DJ wetu bila shaka ningewasikia kina Brass Contraction, Kleer, Sky, D Train, Whispers, Brother Johnson na kadhalika..hapo mkuu ingebidi unishike shati!
Hata hivyo, mambo yalikuwa sii mabaya hivyo inatakiwa wazee wangu wa USA mjipange kisawasawa. next time msimwachie mtu mmoja kuandaa hii kitu..
 
Mkandara... next time tutafanya kitu cha kweli hapa. Kwanza tutaanza na kidogo mwaka huu. Kabla hatujaweza kufanya kikubwa. Tutafanya kidogo kwa watu wa Detroit na kuona how we gonna handle it.. na kwa vile sisi tuna systems zetu wenyewe ni rahisi kusimamia mambo yenyewe.

Tatizo kubwa la Columbus ukiniuliza mimi ni kitu kimoja tu kikubwa, hawakukadiria wingi wa Watanzania watakaojitokeza kuitikia mwito wa kusherehekea pamoja. Hivyo, idadi ya waadaji ilikuwa ni ndogo sana in proportion to the number of people expected.

Nimewahi kuandaa tamasha kubwa la kimataifa pale Mwanza; Na hiyo ilikuwa hakuna mambo ya internet. Lakini tulijua kitu kimoja, ukiwaalika vijana kwenye shughuli ambayo inahusisha zaidi ya jambo moja you better be prepared kufanya mambo mengi kuwaridhisha. So tulikuwa na level karibu tatu katika kamati ya Maandalizi.

Tulikuwa na Timu Kuu (Watu sita) ya maandalizi niliyoiongoza ambayo ilisimamia kila kitu kuanzia ratiba, wageni mashuhuri, mialiko n.k, tulikuwa na timu ya chakula na vinywaji ambalo jukumu lao lilikuwa ni kuhakikisha kunakuwepo na chakula na vinywaji, tulikuwa na timu ya uhamasishaji (promotion), tulikuwa na timu ya Usalama na Ulinzi ambayo ili coordinate na jeshi la Polisi wilaya ya Mwanza mjini, tulikuwa na timu ya Usafiri na Malazi (ambao iliwahakikishia wageni wetu wa kimataifa hasa kutoka Uganda na Kenya kuwa watapokelewa na watapelekwa walikofikia n.k) n.k n.k

Siku ya tamasha walitokea watu karibu mia tatu hivi tukifanya shughuli zetu pale Gandhi Hall, karibu na Jengo la CCM. Matokeo yake ni kuwa maandalizi yetu yalikuwa yamezidi sana idadi ya watu kiasi kwamba watu waliondoka wakiwa si tu wameridhika lakini wamekosheka roho zao.

Katika lililotokea Columbus kutokana na uchache wa waandalizi hawakuweza kuadjust haraka baada ya kugundua kwa watu ni wengi kuliko matarajio yao. Ndio maana unapokwenda vitani wanasema hakuna mpango wa vita (war plan) ambayo inadumu mara baada ya kukutana na adui. Wangeweza kufanya quick adjustment na hata baada ya kukutana na washirika wao wengine waliojitokeza kuwaomba waingilie kati na kutoa msaada au kutoa support ya aina fulani.

All in all, walijaribu kuorganize kitu kikubwa sana ambacho kingekuwa cha kukumbukwa. Natumaini next time watakuwa wamejifunza kutokana na mapungufu yao. Hata hivyo, nawapa hongera kwa kujaribu kwani asiyejaribu hawezi kujua kama anaweza au afanye nini ili aweze next time. Hongera waandaji kwa jitihada zenu, na kufanikiwa kutukutanisha. Next time tunatumaini mtaweza kutuburudisha vya kutosha na kutufanya tusahau ya Columbus. Bado sijaondoa shilingi.
 
Mimi ndio nime-recover hapa, Ilikuwa furaha sana kukutana na baadhi ya members wa JF ambao walitoka sehemu mbalimbali na kuja kukutana pale. Nimefurahi kuwaona Mkandara na crew nzima ya Toronto, QM, AB-Titchaz,Mwanakijiji, Kisura na wengineo wengi tu. Next time itabidi mje Chicago ngoja niandae mambo.
 
yes Sir.. Geeque hayo ndiyo maneno. Mzee kama ndio unarecover tangu siku ile then mwenzetu you had more fun that what humans are allowed to have.
 
yes Sir.. Geeque hayo ndiyo maneno. Mzee kama ndio unarecover tangu siku ile then mwenzetu you had more fun that what humans are allowed to have.

Mkjj utamweza GQ....huyo ni mzee wa shughuli acha mchezo. Tukiwa pale park kuna mshikaji mmoja alimwomba GQ amrushie zile bolingo asizozitaka, maana kila kona mzee yuko na bolingo za kila aina ya mapigo....ha ha ha
 
hahahahahahahah looooooooooool wale walikuwa my cousins bwana QM hahahahaha.
 
hahahahahahahah looooooooooool wale walikuwa my cousins hahahahaha

Yeah right!

Ebanae itabidi unipe schedule ya Chicago. Si unajua huko mimi ni hometown. Niliongea na "mtoto wa mbwa" akaniambia kuwa ulimwambia kuwa kutakuwa na program chi-town siku za karibuni.
 
Yeah right!

Ebanae itabidi unipe schedule ya Chicago. Si unajua huko mimi ni hometown. Niliongea na "mtoto wa mbwa" akaniambia kuwa ulimwambia kuwa kutakuwa na program chi-town siku za karibuni.

Yeah Mazee tarehe 26 July siku ya Jumamosi tutafanya bonge ya BBQ, maandalizi ndio yanaendelea na mambo yatakuwa mazuri kwani nitashikilia usukani mwenyewe kuhakikisha wageni wote mnapata burudani iliyoje. Nitatoa ratiba ya tukio lote in two days or so.

Karibu sana QM na wastue washikaji wote watie timu.
 
Jamani Kisura alisalimika.. maana katika mazingira yale nilikuwa na wasiwasi kidogo. Hatujamsikia isije kuwa tulimsahau kule maana kuna jamaa alijikuta amesahauliwa Columbus... that is another story.
 
yes Sir.. Geeque hayo ndiyo maneno. Mzee kama ndio unarecover tangu siku ile then mwenzetu you had more fun that what humans are allowed to have.
ha ha ha ha Mazee ilikuwa furaha ya kukutana na wengi ha ha ha. Mwanakiji tunakusubiri Chicago sasa on the 26th of July.
 
Yeah Mazee tarehe 26 July siku ya Jumamosi tutafanya bonge ya BBQ, maandalizi ndio yanaendelea na mambo yatakuwa mazuri kwani nitashikilia usukani mwenyewe kuhakikisha wageni wote mnapata burudani iliyoje. Nitatoa ratiba ya tukio lote in two days or so.

Karibu sana QM na wastue washikaji wote watie timu.

Tatizo wengine hatutakiwi tuonekane Chicago.

Mayor wa huko alitu-ban kukanyaga hiyo ardhi baada ya kubambwa na "illegal substance"
 
Jamani Kisura alisalimika.. maana katika mazingira yale nilikuwa na wasiwasi kidogo. Hatujamsikia isije kuwa tulimsahau kule maana kuna jamaa alijikuta amesahauliwa Columbus... that is another story.

Aisee kweli huyu mrembo sijui kama yuko salama. Mara ya mwisho kumwona alikuwa anasakata "inde moniii inde moniii....kumba eh kumba akishakula kumba".... Itabidi tutafute habari zake......
 
Tatizo wengine hatutakiwi tuonekane Chicago.

Mayor wa huko alitu-ban kukanyaga hiyo ardhi baada ya kubambwa na "illegal substance"

hahahahah usiwe na wasiwasi Mazee QM tumeshaongea na Mayor kwa hiyo kutakuwa na exemption siku hiyo wewe tia timu tu bila ya matatizo.
 
Mimi ndio nime-recover hapa, Ilikuwa furaha sana kukutana na baadhi ya members wa JF ambao walitoka sehemu mbalimbali na kuja kukutana pale. Nimefurahi kuwaona Mkandara na crew nzima ya Toronto, QM, AB-Titchaz,Mwanakijiji, Kisura na wengineo wengi tu. Next time itabidi mje Chicago ngoja niandae mambo.

True dat, son.
Huo mwaliko wa Chicago nausubiri kwa hamu na ghamu.
Kisha safari yenyewe saa robo.It was fun to meet the JF
massive and crew and despite the let downs, meeting people
was priceless!!!
 
haya Mialiko inazidi kupamba...
Na mimi nasema hivi, Jumamosi tarehe 2 August kuna kitu kinaitwa Caribana hapa T dot (Toronto) huwa wanakuja tourist (African Americans) kama millioni na nusu. Mji huchukuliwa na ngozi nyeusi kwa week nzima, Sunday kuna cruise boat yaani ni kujichana tu..
Sasa nawaomba wale wote ambao hawana matatizo ya Uhamiaji mnakaribishwa sana. Nina hakika Hotel zote mjini huwa zinajaa kwa hiyo nipigie simu mimi mapema nitakuwa mwenyeji wenu.. msiwe na wasiwasi maadam niijue number ya watu watakao kuja..

Karibuni Toronto...mji wa wazaramo (mdundiko)!
 
Hio Caribana nimekua naisikia siku kibao na nime-iazimia kishenzi.
Acha nitazame mambo ya schedule kazini kisha tuone kama tunaeza
kutia timu!
 
Back
Top Bottom