hiyo ni falsafa ya usalama wa nchi gani? ninavojua mimi, polisi hatakiwi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi ili kumdhibiti mtuhumiwa, huyo polisi alifanya vizuri kumfatilia mtuhumiwa lakini kufyatua risasi alifanya kosa, it's unproffessional! jaribu kufikiria kama lile gari lililogonga lingekuwa ni taxi na wewe ni abiria halafu dereva anakimbia baada ya ajali halafu polisi anafyatulia gari risasi kwa kulenga tairi la mbele na gari
linapinduka na wewe abiria unajeruhiwa au kufa kwa ajili ya upumbavu wa huyu polisi, itakuwa ni busara hiyo? hata kama mwenye baiskeli naye afe baada ya ajali bado kitendo cha polisi huyo kitakuwa ni cha kipumbavu, na vipi ikiwa mwenye baiskeli akinusurika huku wewe abiria ufe au dereva wa taxi afe au wote! ni upumbavu tu! na una uhakika gani kama sababu ya ajali ni uzembe wa dereva wa gari au ni makosa ya mwendesha baiskeli yaliyoshidwa kuepukika? it's a traffic case! madereva wengine huwa wanakimbia baada ya ajali kwa kusalimisha maisha yao kutoka kwa wananchi wanaochukua sheria mkononi na baadae huenda kuripoti polisi.kupiga risasi ya 'maajabu' iliyopasua tairi la mbele na halafu ikamwingia dereva matakoni ni makosa na ni vigumu kuamini!