OCD ampiga risasi mhadhiri SUA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OCD ampiga risasi mhadhiri SUA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lifeofmshaba, May 20, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  MKUU wa Polisi wa Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, jana alishikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumpiga risasi sehemu ya makalio, Mkufunzi wa Sanaa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Dadie Kitururu (42).

  Hata hivyo, baadaye ofisa huyo wa polisi aliachiwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Adolphina Chialo, alithibitishwa kutokea kwa tukio hilo.

  Alisema inadaiwa kuwa jioni ya siku ya tukio Kitururu alimgonga kwa gari mpanda baiskeli aliyetambuliwa kuwa ni Salumu Chiga (58), mfanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

  Kamanda huyo alisema ajali hiyo ilitokea karibu na ofisi za Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kilichoko katika eneo la Kilakala, mjini Morogoro.Chialo alisema wakati ajali hiyo inatokea ofisa huyo wa polisi alikuwa nyuma ya Kitururu, akiwa anaendesha gari lake.

  Alisema baada ya ajali hiyo, Kitururu alikimbia kuelekea eneo la Forest.

  Alisema baada ya kumuona Kitururu akikimbia Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kigoma, alifyatua risasi kwa kutumia bastola yenye namba PA06897 aina ya Chaineez na kupasua tairi la mbele la gari la Kitururu.

  Kamanda huyo alisema hata hivyo risasi hiyo ilipenya na kumfikia Kitururu kwenye makalio yake."Baadaye, OCD alimkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika kituo Kikuu cha Polisi cha Morogoro na kumweka rumande. Hata hivyo baadaye polisi waligundua kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na majeraha na kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi zaidi," alisema kamanda Chialo.

  Alisema baada ya kufikishwa hospitalini mtuhumiwa alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa sababu hali yake ilikuwa mbaya na kwamba katika uchunguzi, aligundulika kuwa na kipande cha risasi katika makalio yake.

  Alisema hata hivyo madaktari walifanya jitihada kuondoa kipande hicho cha risasi.Kamanda Chialo alisema baadaye polisi walimshikilia OCD huyo kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MKUU wa polisi wa wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma (OCD) Onesmo Lianga alijikuta akishikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa muda na baadaye kuachiwa kwa tuhuma za kumpiga risasi sehemu ya makalio mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Dadie Elieli Kitururu (42), mkazi wa Forest.

  Habari toka kwa ndugu wa karibu pamoja na marafiki wa Kitururu zinaeleza kuwa ndugu yao huyo alipigwa risasi Mei 11 mwaka huu majira ya jioni katika eneo la Forest wakati akiwa njiani kurejea nyumbani kwake. Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa siku ya tukio majira ya jioni Kitururu alimgonga mpanda baiskeli Salumu Chiga (58) mfanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Morogoro na mkazi wa Kichangani.

  Alisema mpanda baiskeli huyo aligongwa karibu na eneo la ofisi za Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) Kilakala, manispaa ya Morogoro na Kitururu akaanza akakimbia. Chialo alisema OCD huyo aliyekuwa nyuma ya Kitururu, aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 320 ANQ Suzuki Samurai, alikuwa akiendesha gari lenye namba T 630 BFZ aina ya Rav Four, alimkimbiza Kitururu hadi eneo hilo la Forest. Alisema kuwa OCD huyo mara baada ya kuona Kitururu anakimbia zaidi ndipo alipofyatua risasi kwa kutumia bastora yenye namba PA06897 aina ya Chinese na kupasua taili la mbele ambalo alidai kuwa risasi hiyo ilipenya hadi kumfikia Kitururu kwenye makalio yake.

  Kamanda alisema kisha OCD alimkamata mtuhumiwa huyo na kumfikisha katika kituo kikuu cha polisi mkoani Morogoro na kuwekwa rumande na baadaye polisi waligundua kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na majeraha baada ya kuona akivuja damu na ndipo alipopelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi.

  Alisema kuwa baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa wa Morogoro mtuhumiwa huyo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na hali yake kuwa mbaya na aligundulika kuwa na kipande cha risasi katika makalio yake na hivyo kupatiwa matibabu. Alisema sababu hiyo ndiyo iliyosababisha polisi kuamua kumshikilia OCD huyo kwa mahojiano juu ya tukio hilo na kubaini kuwa alipiga tairi la gari ya Kitururu na baadaye kumfikia katika makalio na kuongeza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.

  Hata hivyo ndugu pamoja na marafiki wa Kitururu waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wamesikitishwa na kitendo hicho wakisema kuwa kazi ya polisi ni kukamata mtuhumiwa pale anapofanya uhalifu na si kuadhibu kama alivyofanya askari huyo wa cheo cha juu katika jeshi hilo.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  PHP:
  Hata hivyo ndugu pamoja na marafiki wa Kitururu waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wamesikitishwa na kitendo hicho wakisema kuwa kazi ya polisi ni kukamata mtuhumiwa pale anapofanya uhalifu na si kuadhibu kama alivyofanya askari huyo wa cheo cha juu katika jeshi hilo.
  Moja ya jambo ninalofurahia vyombo vya habari huria kufichua habari nyingi kama hizi ambazo serikali inafanya kila jitihada kuficha tusijue, na hii ni moja ya skendoo ya jeshi la polisi nchini kunyanyasa wananchi ambao ni dhamana yao kuwalinda. Huyo aliyepigwa risasi hakuwa na silaya yo yote na hakuua.
   
 4. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yaani huyu lecturer kamgonga mfanyakazi wa hospitali ambayo baadaye ilimuadmit kwa matibabu.
  Mi nadhani amestahili kutiwa risasi ya matakoni kwa sababu hakuwa muungwana baada ya kumgonga mpanda baiskeli.
   
 5. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  how come risasi itoke kwenye tairi hadi makalioni? Huyo kamanda alikuwa kwenye engo gani alipokuwa akipiga hiyo risasi?
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mimi pia hapa sijapaelewa, tairi ya mbele na makalio!
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Uko sahihi kabisa, risasi haipigi kona, gurudumu lipo mbele na kiti kipo nyuma. Alyepiga risasi yu nyuma ya aliyepigwa risasi.
  Itawezekana vipi risasi ipige gurudumu halafu irudi tena kumpiga mtu makalioni!

  Police this is a holy lie, please remember you can fool some people some time, but you cant fool all the people all the time.
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  OCD wa Kibondo, eneo la tukio Morogoro, maelezo hayaridhishi sana.

  Hii ni hadithi ya funika kombe mwanaharamu apite.

  There is more in this story more than what meets the eye. An independent investigator should deal with this case.
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hilo nalo neno......................
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Soma post mstari baada ya mstari, usikurupuke kucomment.
  Kuna mapungufu mengi kwenye hii hadithi ya polisi mpaka utagundua kuwa ni hadithi ya kutunga
   
 11. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  :mod::mod::mod::mod:
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  .. Kwa nini aligonga mtu na kukimbia? Polis nao wanatumia risasi bila mpango siku hizi watu wanauawa na kupewa jina kwamba ni majambazi kweli nchi haina utawala wa sheria!
   
 13. c

  chetuntu R I P

  #13
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  OCD Angemuua mhadhiri story ingekuja kivingine. Matumizi ya silaha kwa raia yako hovyo. There is somethin behind the story. Waseme ukweli.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Huyu mhadhiri vipi, kagonga halafu anakimbia, si angesimama kumsaidia huyo mpanda baiskeli?
   
 15. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hapo ndipo muhimu zaidi kuliko hata hiyo risasi ya makalioni. nchi nyingine ukigonga na kukimbia bila kujali matokeo ya ile ajali, basi unahesabiwa ulikusudia kuua. nimewahi kuona mtu anamgonga mwendesha pikipiki, akaacha gari na pikipiki pale ili polisi waje kupima, akakodi taxi na kumkimbiza mpanda pikipiki hospitali huku yeye mwenyewe akiwapigia simu polisi na kuwaeleza kilichotokea na kuwaelekeza hospitali alipompeleka majeruhi!

  wenzetu wanajali utu kwanza!
   
 16. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Unajuaje labda alikuwa anakimbilia polisi au alikuwa anataka kujiokoa.

  Je tumeskia aliyepigwa risasi akitoa utetezi wake?

  Unategemea nini wakati mtuhumiwa ni afisa wa ngazi ya juu kwenye jeshi la polisi ambao ndio wanapepeleza kesi hii?
   
 17. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
   
 18. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  tatizo wabongo wanajifanya wana hasira,ukigonga ukakaa watakupiga,kuna watakaochukua vioo vya sight,pochi,simu e.t.c.so sometimes ni beta kukimbia
   
 19. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160

  Hata Tanzania kuna watu wanafanya hivyo.

  Lakini lazima uangalie mazingira ya usalama wako kwanza. Ajali ambazo watu hawakimbii ni za gari kwa gari.

  Ukimgonga mwenda kwa miguu au mwenye baiskeli, kuna watu wana hasira tu na wenye magari na ndio hapo hupata sababu ya kukubonda na kufanya vandalism.

  Kwa ujumla raia wengi hawana uelewa na huruma na mwenye gari kama kuna ajali iliyomuumiza asiye na gari.

  Kwa sababu hii unatakiwa uangalie usalama wako, na unaruhusiwa kisheria kukimbilia polisi.

  Kwenye hiyo stori, haijaeleweka huyo OCD wa kigoma alikuwa anaonekana ni OCD kweli hapo morogoro au alikuwa kama kibaka mwingine. Labda dereva kwa fikra zake, alikuwa anakimbia kujiokoa toka kwa vibaka.

  Na kama walivyosema wengine, hapo kuna stori zimefichwa. Huyo OCD kwa utalaam na kazi yake, nafikiri alitakiwa tu kuchukua namba za gari, na kurudi kumsaidie aliyegongwa. Badala yake inaonekana alianza kumfukuza huyo dereva na kupiga risasi. Halafu risasi ikapitiliza toka kwenye tairi na mavyuma vyuma mengine hadi kufikia makalio ya dereva... Wizi mtupu!! Bora uniambie Simba inaweza kuifunga Man united 10 bila. Ninaweza kuamini. lakini si hii stori kwa jinsi ilivyoandikwa.
   
 20. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  :grouphug::mod::A S-rose:Hongera OCD huo ndiyo uzalendo,hata kama siyo kituo chako cha kazi,ukiona uhalifu chukua hatua mtuhumiwa akiresist use reasonable force hiyo ndiyo falsafa ya usalama ,hata ungeua hakuna shaka kuliko kuacha mtuhumiwa aende untouched:A S-rose:
   
Loading...