Obama hana shukrani?

At least boma umenisaidia maana hapa JF jamaa walishaanza kunishambulia ati ooo arudi kufanya nini, mara ati ana ratiba ngumu....mbona wachaga kila mwaka wanasahau ratiba ngumu na wanakwenda kwao kuhesabiwa? Obama alipata hadi dua za wazee kule Wajir, akavalishwa mishuka akafanana kama msomali ndio maana akaukwaa urais....ni lazima aje aseme wazee taire.....

Kwa hiyo urais ameupata kwa dua za kabila lao na siyo kuwa kipenzi cha wamarekani siyo? Nina wasiwasi na hii ya dua! Imekaa ki-sheikh yahya zaidi. Nafikiri mimi kura alipigiwa na wamarekani kwa kumpenda tu pamoja na kampeni strong.
 
obamavuka.jpg


Hakuna shaka Obama (kulia) ni mjaluo wa Kisumu na alikwenda kijijini Kogelo kutangaza nia ya kugombea urais na kupata baraka zote za wazee. Na alipopata urais watu wa kijijini kwake walifanya bonge la pati kwa kuchinja ng'ombe 4. Sasa mbona harudi kusema asante? Au anasubiri uchaguzi ukaribie?

Jinsi jamii yake ilivyosherehekea Kenyan village awaits Obama's historic inauguration_English_Xinhua

Akichaguliwa tena 2nd term ndiyo utajua kuwa hana shukrani au anayo. Hivi anawanyima wale wabaguzi hoja za uchaguzi wa 2012.
 
Iwapo anahofia vitu vidogo vidogo kama hivyo kuhusiana na kwao basi afadhali akose huo uraisi kipindi cha pili.Mbona hakuhofu mambo kama hayo kwa kwenda kujinasibu kule Scotland?.
Kukosa kwake uraisi itakuwa ni nafuu kwetu waislamu wa Kenya na EA kwa sababu siku akija kama raisi tutadhalilika sana.Hata nchi yetu nayo itadhalilishwa sana.Nakumbuka Bush alipokwenda Tanzania walipanda mpaka juu ya paa za ikulu bila kuomba ruhusa ya mtu yeyote.Askari waliokuwepo walijifanya kama hawawaoni na hawakusema nao.
Akija tena Kenya wacha aje kama mtoto mpotevu anayerudi kwao.


Umeanza la uislam tena! Hivi wewe pasipo kuweka udini hujisikii raha? Unajivunjiaheshima yako bure. Hivi uislam nao ni jambo la kujivuni kwa mtu mwenye akili hasa wakati huu wa kujitia mhanga! Mh! Pole sana
 
Namchukia huyu mjaluo anampiga Ghadaff mbona sasa halipi mishahara ya wanajeshi wa uganda wanaolinda amani kule somalia?!!!
 
Huyo sasa ni rais wa nchi ambayo viongozi wao wanategemewa kuonyesha mafanikio ya uongozi wao hamna time ya kuranda randa Afrika na watu wavivu. Wanamuangalia kwa mafanikio katika hali ya uchumi, nyadhifa za kazi, usalama, afya, elimu n.k. nae anajua yote hayo kuwa akicheza hakuna awamu ya pili atakuwa ni ' one term president'

Ni juu ya hao wanakijiji huko kenya kutumia jina la Obama kupata watalii nakustawisha jumuiya yao - zaidi ya hapo wataishia kulala tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom