Nyumbani wamemkataa mchumba wangu. sababu: mhaya!

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Wadau
nipeni ushauri nipo njia panda. ni kweli sababu waliyonipa kuwa wahaya wana tabia mbaya?

mi ni mngoni, nishauri!!
 
hayo yalipitwa nawakati kuchaguliana wachumba kama unampenda shikilia msimamo wako jiamini unapofanya maamuzi yako nahiyo ndio sifa yamwanaume.oa unayempenda hatakama wao hawampend badae watamkubalitu hata kishingo upande.mke niwako si wawazazi
 
Wazazi wako wana nafasi katika maisha yako kama wazazi lakini nionavyo mimi hawastahili kuingilia chaguo lako la mtu umpendae kuishi nae katika maisha yako. Hata hivyo tabia mbaya ziko kwa makabila yote siku hizi. Nina rafiki yangu akutwa na issue kama yako. Kaacha Mhaya wake akapewa mke na wazazi, maisha yake yamejaa majuto. Huyo mke wa kabila lake aliwafanyia visa yeye na wazazi wake hadi leo anaishi naye kwa ajili ya watoto huku wakiishi kwa matumaini. Chaguo ni kako bwana.
 
wasikilize wazazi kwahilo mwisho watakuambia kwa wiki unamnanihi mara 1 tu
 
Wadau
nipeni ushauri nipo njia panda. ni kweli sababu waliyonipa kuwa wahaya wana tabia mbaya?

mi ni mngoni, nishauri!!
Hivi zamahizi bado kuna mtu anaomba ushauri wa namna hii, haya kama wazazi wako ndo watakuwa na huyo mhaya ndani ya kuta nne endelea kuwasikiliza
 
duh karateka pole sana wa kunyumba! Hata baba yangu alitaka kumkatalia dada yangu alipoleta mchumba jina lake lilifanania sana na wahaya lkn yeye ni muha wa kigoma, cha kushangaza aliwahi mwambia hata kaka yetu mkubwa kwamba hataki aoe mwanamke wa kihaya. Hapohapo dingi mdogo mkewe ni mhaya, mtoto wake wa mwisho wa kike aliishi sana bukoba mpaka alipomaliza std seven so ana lafudhi ya kihaya kabsaa shule hajamaliza kufukuzana na suruali tu sinza. Baba aliwahi fanya kazi karagwe labda alikuwa na sababu zake sijajua. Mimi nawafahamu wasichana wa kihaya wengi tu tena wako very decent na wamekuwa wake wazuri tu. Hii generation yetu kabila wala si sababu, sababu kubwa ni malezi mtu aliyoyapata toka kwa wazazi, pili uchumi au kipato tatu ndoto na tamaa ya kuwa na mafanikio bila kuwa na kipato cha kutosha, so kuepukana na yote hayo kijana piga shule ukipata kazi jikusanye atleast 5 yrs ndio uoe ukiwa umejiandaa kutunza mke! Pole sana wakunyumba
 
wazazi wengine bana, hivi hawajui kuna mipaka ya kujiingiza kwenye private issues za watoto wao hasa wanapokua wakubwa? wewe oa bana kwani huyo mke anaishi na wazazi au anaishi na wewe muoaji? mambo mengine sio kabisa
 
Mwache tu huyo dada yetu, uhaya wake isiwe tabu ...ila kama ana meet criteria zako nakushauri komaa make mpaka umempata kwa mtu anayeelewa wadada wa leo ataelewa namaanisha nn ...mke wa kuoa leo ni kama almasi ijapo barabarani ni wengi na wanapendeza haina kiwango
 
Kama unampenda kweli, we mjaze mimba azae mtoto tuone kama wazazi watamkataa, siku izi hupaswi kuangalia kabila kinachomata ni tabia ya mtu, naamini mmependana na kilamtu kalizika na mwenzie.
 
Mbona wangoni ndio walewale ..

Sikiliza wazazi .. achana na ulimwengu wa sasa unaowaona wazazi wamepitwa na wakati ..
 
Unatafuta MKE WENU au MKE WAKO??????????????????

Unatafuta Kabila au Mke wako????????????????????????

Ndoa yako ni kwaajili ya satisfication ya ukoo wenu????????????

MUOMBE MUNGU AKUPE MKE WAKO
 
Back
Top Bottom