livewise1
JF-Expert Member
- May 25, 2019
- 837
- 972
Morning JF!
Kuna hizi nyumba zina wapangaji wengi, kusema ukweli zina chengamoto nyingi zaidi.
Hususani kama kuna mchanganyiko wa walioko kwenye ndoa na walio single. Waliopo kwenye ndoa hawana amani kwa namna fulani wanapoona kuna mazoea kati ya mwenza wake na mpangaji mwengine wa jinsia tofauti.
Mfano majuzi nilimtembelea workmate amepanga nyumba ya wapangaji wengi. Wanawake wanaoishi hapo wenye waume wakaanza kumuuliza mwenyeji wangu "eti dada huyu ndio shemela yetu eeh" (niliskia wakati wanaulizana nje mi nikiwa ndani).
Mara kidogo akaingia mwanaume (mume wa mmoja wa wanawake wa chumba cha pili) akamsalimia mwenyeji wangu " habari za saizi jirani, naona unarekebisha mahanjumati!" Cha ajabu akadakia mkewe huyo jamaa, "we nae baba xx huoni viatu hapo kaja mtu wake upunguzage shobo"
Nilistuka kiasi nikaskilizia...mwenyeji wangu akacheka na kujibu salam kisha akamwambia huyu ni workmate tu jaman sio mtu wangu. Jamaa akajibaraguza kwa kusema "Jirani utamuweza huyu we mchukulie tu hivo alivo"
Nikacheka ndani kwa ndani kisha nikawaza ni chengamoto kiasi gani wanakumbana waliopanga nyumba za namna hii.[emoji3]
Alipoingia ndani workmate akatenga chakula, akaniambia huyo mwanamke aliemkatisha mumewe anatembea na mpangaji mwenzao na wanafanyia hapo hapo.
Duh....changamoto sana.
Sent using Jamii Forums mobile app