Nyumba za kupanga uswahilini shida

wambagusta

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
2,825
2,291
Yeye na mumewe siwaherewi ! siku moja nilimuona mumewe katoka chooni akaenda kwenye malango wa chumba changu akajifuta miguu yake kwenye zuria langu la mlangoni alivyo maliza akaenda chumbani kwake siku hiyo nikadharau. Khee ! tena juzi namuona mkewe kafanya kama alivyofanya mumewe sasa nikashangaa sana nikaona bora nimwambie huyo dada nikamtafutia muda akiwa peke yake hili nimwambie ukweli kwamba sipendizewi na hiyo tabia. kheee ! baada ya kumwambia bidada .yeye na mumewe wamenichunia salamu namie hawataki
 
isee hatari sana,heri ya hilo mimi niliwahi kukaa nyumba,mpangaji mwenzangu alikuwa anaishi na nyoka,alikuwa akikaa kwenye ngazi unamuona anakaa naye anamshika shika,akiondoka na gari yake anamuweka kwenye gari anaondoka,usiku nikiwa nimelala saa saba nikichungulia kwenye dirisha namuona amekaa nje na nyoka wake
 
duuh!! angalia usije ukafanywa mbuzi wa kafara?
tafakari, chukua hatua..!!!
 
isee hatari sana,heri ya hilo mimi niliwahi kukaa nyumba,mpangaji mwenzangu alikuwa anaishi na nyoka,alikuwa akikaa kwenye ngazi unamuona anakaa naye anamshika shika,akiondoka na gari yake anamuweka kwenye gari anaondoka,usiku nikiwa nimelala saa saba nikichungulia kwenye dirisha namuona amekaa nje na nyoka wake
Heheheee.. Are you sure hazikua illusions? Mbona ni hatari sana hiyo..?
 
Nyumba za kpanga zina vituko vingi mno na kupitia vituko hivyo tunajifunza mengi mno juu ya walimwengu na ulimwengu na labda hao jirani walikuchukulia ki-ujirani tu na wakapenda mat lako kama ungekuwa na mawili ungemwita tu huyo mwanamke badala ya kumletea niaje unampa Doormat ingine unamwambia iekeni pale mlangoni kwenu muwe mnajifutia miguu...Hakika usingepungukiwa na unachukulia ni moja ya sadaka umetoa...
 
Kwa nini usimweleze mwanaume mwenzio badala yake umeongea na mkewe?
 
Sijui wewe mkuu umelichukuliaje ila ningekua mimi nisinge mind hata kidogo sababu hakuja kufutia chumbani kwako ni zulia lakufutia miguu hiyo ni sadaka pia kwa Mungu,mbona ni vitu vidogo sana hivyo? hao niwapangaji wenzio wewe ni binadamu huenda ukapata tatizo na hao ndio majirani wako wa kwanza,chukulia kawaida tuu sikunyengine usi mind vitu vidogo kama hivyo......
 
Yeye na mumewe siwaherewi ! siku moja nilimuona mumewe katoka chooni akaenda kwenye malango wa chumba changu akajifuta miguu yake kwenye zuria langu la mlangoni alivyo maliza akaenda chumbani kwake siku hiyo nikadharau. Khee ! tena juzi namuona mkewe kafanya kama alivyofanya mumewe sasa nikashangaa sana nikaona bora nimwambie huyo dada nikamtafutia muda akiwa peke yake hili nimwambie ukweli kwamba sipendizewi na hiyo tabia. kheee ! baada ya kumwambia bidada .yeye na mumewe wamenichunia salamu namie hawataki

Hapo dawa ni kwenda kupanga uzunguni tu ili uepukane na kero za uswahilini kinyume cha hapo jenga nyumba yako, weka fensi uishi kwa amani au endelea kuvumilia.

Au hutambui uswahilini kuna vituko? by Suma G ft. Inspector Haroun enzi hizo.
 
Sijui wewe mkuu umelichukuliaje ila ningekua mimi nisinge mind hata kidogo sababu hakuja kufutia chumbani kwako ni zulia lakufutia miguu hiyo ni sadaka pia kwa Mungu,mbona ni vitu vidogo sana hivyo? hao niwapangaji wenzio wewe ni binadamu huenda ukapata tatizo na hao ndio majirani wako wa kwanza,chukulia kawaida tuu sikunyengine usi mind vitu vidogo kama hivyo......
Bro fikilia mara mbili act angekuwa yeye!
 
S
Hapo dawa ni kwenda kupanga uzunguni tu ili uepukane na kero za uswahilini kinyume cha hapo jenga nyumba yako, weka fensi uishi kwa amani au endelea kuvumilia.

Au hutambui uswahilini kuna vituko? by Suma G ft. Inspector Haroun enzi hizo.
sawa mkuu nitajitahidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom