Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 257
Mke wa beki wa zamani wa Simba, Victor Costa Nampoka amelia na kusema umasikini unaendelea kuwamaliza hasa baada ya nyumba yao iliyo maeneo ya Tegeta kuteketea na moto.
"Umasikini huu jamani, kama unavyoiona, nyumba yote imeteketea, kweli inatia uchungu sana," alisema Jasmini ambaye pia ni mjumbe wa kamati tendaji ya Simba.

Masaibu hayo yameikuta familia ya Costa wakati akiwa mkoani Shinyanga na timu yake ya sasa ya Mwadui FC.
Costa amesema chanzo cha moto huo ni kibatari kilichowashwa baada ya umeme kukatika na baadaye moto wa kibatari kushika kwenye pazia na kwa kuwa watu hawakuwepo ndani, moto ule ulisambaa.
Costa aliongeza kuwa moto huo umeteketeza kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba na hakuna kilichosalimika.
Kabumbu