yani umeandika makala ndefu ya kibaguzi, kweli makonda aliliona hiliNimekulia hapa Machame jirani kabisa na Nyumbani kwa Marehemu Mengi,kwa mujibu wa taratibu tunazojua sisi mke ndiye mmiliki wa nyumba iliyoachwa na marehemu
Jacky hajawahi kuishi huku tangu kuolewa na Mengi na kwa taraibu ni kwamba kuanzia sasa atamiliki yeye na watoto wake mapacha mpaka kifo kitakapo waondoa hapa duniani
Watoto wawili wakubwa wa Mengi ambao ni rika zetu hawana chao hapa hasa ukizingatia baba yake Mengi alitoka kijiji cha Mkuu akanunua hili shamba na kumrithisha Mengi naye akajenga hii nyumba jirani kabisa na mto weruweru
Nia na madhumuni yangu kuandika waraka huu ni kutokana na mawazo niliyo nayo juu ya hatma ya mila na desturi za kichaga jinsi zinavyoendelea kuharibiwa na watu wanaoitwa wanaume wa kichaga
tumejionea wenyewe wanaume wanavyokufa mapema sio wachaga tuu hata makabila mengine
Lakini kwa mtazamo wangu kabila hili lina mila zake maalum ndio maana ni vigumu sana kununua au kuuza ardhi huku uchagani. Wanaume wa kichaga wanachangia sana kuharibu mila na tamaduni zetu kwa kutuletea wanawake na kuwarithisha boma kinyume na mila zetu
Unaenda huko unatuletea moli wa kabila lingine halafu unakufa halafu huyo moli analeta ndugu zake wasiojua jinsi babu zetu walivyapambana kutuwekea mazingira katika hali hii tuliyo nayo
Ndugu zangu babu zetu wakifanya kazi na mangi wa machame walifanya kazi kubwa sana,nakumbuka babu yangu aliyezaliwa mwaka 1911 aliniambia baba yake aliyezaliwa mwaka 1870 ni mmojawapo wa wanajeshi walienda kijiji kinaitwa lyamungo kuzuia wakibosho kuendelea kusonga mbele kufyeka msitu wakisogelea maeneo ya machame
Ilibidi wanajeshi na majemedari wa kimachame wajitoe muhanga kupambana na hili kabila la kikibosho kuzuia ufyekaji wa msitu huku wakisogelea machame. Kuna watu wamepambana kufanya machame iwe hivi kama illivyo, haikuwa kazi rahisi kama tunavyofikiri
Mnatuletea wanawake wa makabila mengine mnawaacha hapa kwenye maboma ya kurithi halafu mnakufa mapema hao wanawake wanaleta ndugu zao kuvuruga taratibu zetu za heshima za mila na desturi halafu mkishakufa mnawaacha hawa wanawake bado vijana wanaolewa na wanaume wengine wanawaleta pale kwenye ile miji ya kurithi
Sijapenda sana jinsi hali inavyoedelea ni kujaribu kulifuta kabila la kichaga
huyo jacky alivyo na nyodo atawasumbua sana watoto wa Mengi wakitaka kuja likizo huku machame anaweza asiwaruhusu kukaa pale nyumbani kwa bab yao
naomba wanaume wa kichaga mfikirie ukubwa wa matatizo mnayotuletea huku kijijini