Nyumba ya baba mkwe kuuzwa kisa deni la mahari

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,102
36,060
Katika hali isiyo ya kawaida, nyumba ya Seleman Mussa (65), Mkazi wa Kijiji cha Nkoma, wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu, iko hatiani kuuzwa kama fidia ya deni la Sh 1.1 milioni, analodaiwa baada ya kutokamilisha deni la mahari ya kijana wake.

Kijana wake ambaye ni mwalimu wa shule moja ya sekondari mkoani Shinyanga, alimuoa binti wa Mwita Kati, toka mwaka 2019 kwa ndoa ya kimila, kwa makubaliano ya mahari ya ng'ombe 15.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Mussa amekiri juu ya makubaliano hayo kwa kusema: “Tulikubaliana mahari ya ng'ombe 15 kwa thamani ya Sh150, 000 kila mmoja, baada ya maridhiano walikuja nyumbani wakasema wanataka mahari yote lakini tuliwaomba wachukue nusu na inayobaki tutailipa baadae," amesema Seleman.

Hata hivyo kwa mujibu wa Seleman, ilipofika mwaka 2020 baba mzazi wa binti alianza kudai mahari iliyosalia, ndipo alipoomba muda wa kuendelea kutafuta pesa ili kukamilisha deni hilo, na hapo ndipo ugomvi ulipo anzia.

"Hakuelewa alitaka nimlipe pesa yote iliyobaki Sh 1.5 milioni….pale vikao vya familia viliposhindwa kupata muafaka walihamia katika ngazi ya Serikali ya kijiji hadi mahakamani. Huku mimi nikikimbilia ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu kutafuta Suluhu,” amesema na kuongeza;

"…nikiahidi kupunguza….na nilifanikiwa kulipa Sh 500, 000 na hivyo kubaki na deni la Sh 1.1 ambayo licha ya Mkuu wa Wilaya kututaka tumalize kifamilia, wao waliendelea na kesi mahakamani na hukumu kutolewa.”

Katika shauri hilo la madai namba 81 la mwaka 2020, hukumu ilitolewa ambayo ilitaka kukamata nyumba ya Seleman namba 27B iliyopo kijiji cha Nkoma ili kufidia kiasi cha Sh1.21 na hivyo kukamilisha kiasi cha Sh2.255 milioni zilizokuwa zilipwe kama mahari.

Nani alaumiwe? Je, ndoa itabaki salama?
 
Mahari yanadaiwa mpaka mahakaman? Si wangeshughulikia mambo yao kimila?

Kama imeshindikana kulipwa, si angesamehe tu?

Kudaiana mahari mahakamani hakuleti mtazamo kuwa Mwalimu aliuziwa mke?

Baadhi ya tamaduni zinatia ukakasi!
 
Katika hali isiyo ya kawaida, nyumba ya Seleman Mussa (65), Mkazi wa Kijiji cha Nkoma, wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu, iko hatiani kuuzwa kama fidia ya deni la Sh 1.1 milioni, analodaiwa baada ya kutokamilisha deni la mahari ya kijana wake.

Kijana wake ambaye ni mwalimu wa shule moja ya sekondari mkoani Shinyanga, alimuoa binti wa Mwita Kati, toka mwaka 2019 kwa ndoa ya kimila, kwa makubaliano ya mahari ya ng'ombe 15.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Mussa amekiri juu ya makubaliano hayo kwa kusema: “Tulikubaliana mahari ya ng'ombe 15 kwa thamani ya Sh150, 000 kila mmoja, baada ya maridhiano walikuja nyumbani wakasema wanataka mahari yote lakini tuliwaomba wachukue nusu na inayobaki tutailipa baadae," amesema Seleman.

Hata hivyo kwa mujibu wa Seleman, ilipofika mwaka 2020 baba mzazi wa binti alianza kudai mahari iliyosalia, ndipo alipoomba muda wa kuendelea kutafuta pesa ili kukamilisha deni hilo, na hapo ndipo ugomvi ulipo anzia.

"Hakuelewa alitaka nimlipe pesa yote iliyobaki Sh 1.5 milioni….pale vikao vya familia viliposhindwa kupata muafaka walihamia katika ngazi ya Serikali ya kijiji hadi mahakamani. Huku mimi nikikimbilia ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu kutafuta Suluhu,” amesema na kuongeza;

"…nikiahidi kupunguza….na nilifanikiwa kulipa Sh 500, 000 na hivyo kubaki na deni la Sh 1.1 ambayo licha ya Mkuu wa Wilaya kututaka tumalize kifamilia, wao waliendelea na kesi mahakamani na hukumu kutolewa.”

Katika shauri hilo la madai namba 81 la mwaka 2020, hukumu ilitolewa ambayo ilitaka kukamata nyumba ya Seleman namba 27B iliyopo kijiji cha Nkoma ili kufidia kiasi cha Sh1.21 na hivyo kukamilisha kiasi cha Sh2.255 milioni zilizokuwa zilipwe kama mahari.

Nani alaumiwe? Je, ndoa itabaki salama?
Anayeoa ni mtoto, mzazi inakuwa awe dhamana?
 
Tena walipe na fidia kabisa km mtoto wao keshazaa hapo. Huyo mwalimu hana adabu na inawezekana ni tapeli. Inawezekanaj ashindwe kulipa mahali yote tangu 2019. Pia inaonekana huyo mwalimu anadekezwa na baba yake, inakuwaj mtu ana kazi alafu baba yake ndiye anamtolea mahari. Huyo mwalimu ni mtu hovyo sn sasa kakutana na mkurya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom