Morogoro: Auwawa na mashemeji zake baada ya kushindwa kumalizia deni la mahari ya dada yao shilingi laki tano

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,112
49,826
Ukistaajabu ya Musa Utayaona ya Firauni.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 nimeshindwa kujizuia kucheka japo simaanishi nimefurahi.R.I.P Mwamba.

Vijana mnaojiandaa kuoa kueni makini.
---
WATU wanne wa familia moja akiwemo Masele Machibya Masele (65) mkulima na mkazi wa Tabora wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kula njama na kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Itegete, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro ambaye alikuwa anadaiwa kushindwa kulipa deni la mahari ya Sh 500,000.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama ametoa taarifa hiyo ambapo amesema, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa Agosti mwaka huu katika kijiji hicho kilichopo wilayani Kilombero.

Mkama amewataja watuhumiwa waliokamatwa ni Masele Machibya Masele (65), mkulima na mkazi wa Tabora, Mwalu Ndama Hassan (18), Pawa Ndama Kema (16) na Rehema Masele (35), wote ni wakulima na wakazi wa kijiji hicho.

Amesema watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa walikula njama ya kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Itegete, ambapo kimsingi inadaiwa alikuwa ameshindwa kulipa deni la mahari.

“Hawa ni wafamilia moja, Masele Machibya Masele ni Baba mkwe wa marehemu, alitoka Tabora kuja kumdai mahari mkwewe, na hao wengine ni mke na watoto wa marehemu“ amesema Mkama

“Sasa walipoona huyo (Marehemu) amekuwa mkaidi muda mrefu halipi mahari na ameshapata watoto tayari waliamua kula njama na kumuua“ amebainisha Kamanda Mkama.

Nipashe
 
Sasa hiyo mahari ni ya nani tuanzie hapo
Ya nani kivipi?

Wanasema: Kuna mkulima mmoja Morogoro alienda kuoa mke Tabora kwa mkopo(alilipia mahari pungufu) ikabaki anadaiwa 500k kwa muda zaidi ya miaka 16.

Kwa tukio hili baba mkwewe alikusanya wanae Toka Tabora kwenda Moro kudai deni lake la mahari.
Kilichotokea au mtafaruku gani hadi ikapelekea kumuua mdaiwa hakijaelezwa.

Sasa hapo unaweza kuuliza mwenye mahari ni nani?
 
Ukistaajabu ya Musa Utayaona ya Firauni.

nimeshindwa kujizuia kucheka japo simaanishi nimefurahi.R.I.P Mwamba.

Vijana mnaojiandaa kuoa kueni makini.
---
WATU wanne wa familia moja akiwemo Masele Machibya Masele (65) mkulima na mkazi wa Tabora wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kula njama na kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Itegete, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro ambaye alikuwa anadaiwa kushindwa kulipa deni la mahari ya Sh 500,000.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama ametoa taarifa hiyo ambapo amesema, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa Agosti mwaka huu katika kijiji hicho kilichopo wilayani Kilombero.

Mkama amewataja watuhumiwa waliokamatwa ni Masele Machibya Masele (65), mkulima na mkazi wa Tabora, Mwalu Ndama Hassan (18), Pawa Ndama Kema (16) na Rehema Masele (35), wote ni wakulima na wakazi wa kijiji hicho.

Amesema watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa walikula njama ya kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Itegete, ambapo kimsingi inadaiwa alikuwa ameshindwa kulipa deni la mahari.

“Hawa ni wafamilia moja, Masele Machibya Masele ni Baba mkwe wa marehemu, alitoka Tabora kuja kumdai mahari mkwewe, na hao wengine ni mke na watoto wa marehemu“ amesema Mkama

“Sasa walipoona huyo (Marehemu) amekuwa mkaidi muda mrefu halipi mahari na ameshapata watoto tayari waliamua kula njama na kumuua“ amebainisha Kamanda Mkama.
Sidhani kama inawezekana. Kuna jambo zaidi limefichwa

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Tujitahidi sana kutokomeza umaskini ni kitu mbaya sana. Mimi mahari nimekuja kulipa mwaka jana na familia hakuna aliekua anaongelea hilo swala wala kudai na nizaidi ya miaka 8 tuangalie na familia za kuoa jamani ogopa sana familia inayodai mahari wakati ndoa ni kuunganisha familia sio kuuziana mwanamke.
 
Ya nani kivipi?

Wanasema: Kuna mkulima mmoja Morogoro alienda kuoa mke Tabora kwa mkopo(alilipia mahari pungufu) ikabaki anadaiwa 500k kwa muda zaidi ya miaka 16...
Mahari katika Uislam ni ya mke kama zawadi au ahadi ya zawadi kutoka kwa mume kwenda kwa mke
Ni haki ya mke ndio maana nikauliza hivyo wala sikuwa na kusudio lolote

Ila kwa maelezo yako hapo neelewa

Sisi kwa uislam ukitoa ahadi ya mahari iwe chochote ni deni linalokusubiri.

Wengi huwa wanatoa haraka na wengine kwa awamu lakini linakusubiri kwa hiyo ni bora kumpa mke chake ulichoahidi

Kama ni dini zingine sijui kwa kweli
Ila Asante kwa kunielewesha hili Sakata
 
Ukistaajabu ya Musa Utayaona ya Firauni.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 nimeshindwa kujizuia kucheka japo simaanishi nimefurahi.R.I.P Mwamba.

Vijana mnaojiandaa kuoa kueni makini.
---
WATU wanne wa familia moja akiwemo Masele Machibya Masele (65) mkulima na mkazi wa Tabora wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kula njama na kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Itegete, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro ambaye alikuwa anadaiwa kushindwa kulipa deni la mahari ya Sh 500,000.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama ametoa taarifa hiyo ambapo amesema, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa Agosti mwaka huu katika kijiji hicho kilichopo wilayani Kilombero.

Mkama amewataja watuhumiwa waliokamatwa ni Masele Machibya Masele (65), mkulima na mkazi wa Tabora, Mwalu Ndama Hassan (18), Pawa Ndama Kema (16) na Rehema Masele (35), wote ni wakulima na wakazi wa kijiji hicho.

Amesema watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa walikula njama ya kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Itegete, ambapo kimsingi inadaiwa alikuwa ameshindwa kulipa deni la mahari.

“Hawa ni wafamilia moja, Masele Machibya Masele ni Baba mkwe wa marehemu, alitoka Tabora kuja kumdai mahari mkwewe, na hao wengine ni mke na watoto wa marehemu“ amesema Mkama

“Sasa walipoona huyo (Marehemu) amekuwa mkaidi muda mrefu halipi mahari na ameshapata watoto tayari waliamua kula njama na kumuua“ amebainisha Kamanda Mkama.

Nipashe
kwa vyovyote vile hawa watakuwa ni waisilamu
 
Back
Top Bottom