Jamani nina rafiki yangu amepata ajali sasa cha kushangaza nyumba ndogo a.k.a Mchepuko unang'ang'ania umuuguze wakati jamaa ana mke kabisa leo nimebeba msala kwa kukubali kuwa ni mchumba wangu baada ya mwenye mali kuhoji nikaona itakuwa timbwili wodini, tumejaribu kushauri lakini haelewi somo, mwaka jana kuna rafiki yangu mwingine aliugua nyumba ndogo akang'ang'ania wodini ili amuuguze mpenzi wake huku akijua jamaa ameoa hivi kwanini hii michepuko inakuwa na viherehere sana.