Kwenye ndoa wanaume hufuata ngono na heshima (norms, customs). Wanawake hufuata usalama, heshima, maisha (it is like a job). Hii mitazamo haiwezi kushabihiana siku zote.
Hutokea mme akakosa ngono ndani ya ndoa, jibu rahisi ni kuifuata nje. Hutokea mwanaume akakosa heshima kwa mke aliyemuoa na hivyo akaamua kuitafuta heshima huko nje.
Hutokea mwanamke akaona ndani ya ndoa hapati usalama (anatukanwa/anapigwa) akaamua kuutafuta usalama nje. Huyo atakayempa usalama mara nyingi ni mwanaume mwingine, naye atahitaji malipo - Ngono. Hutokea tena mwanamke katika ndoa akakosa heshima (familia ya mme hawamtaki) au akakosa maisha (mkwanja hakuna hivyo no shoping ya nguo, vipodozi, na misosi ya nguvu). Hivi vitu akivikosa mara nyingi atajalibu kujazilizia huko nje.
Sisemi kufanya hayo ni halali, la hasha. Ninachosema ni kuwa hayo ndiyo yanayotokea ndani ya nyumba zetu. Huko kujazilizia kilichokosekana wakati mwingine huwa si conscious. Kunakuwa na msukumo wa kufanya kitu fulani kutokana na stress inayosababishwa na void fulani ambayo imeletwa na matarajio au matamanio ambayo hajakamilishwa (not realized).
Kwenda kwenye nyumba ndogo (zingine hugeuka kuwa kubwa), siyo suluhisho. Mara nyingi ni sign ya kuwepo kwa hayo niliyotaja hapo juu. Huwa si suluhu. Anayefanya hufanya huku akiamini kuwa anajazia ile void na Matokeo yake siku zote (au mara nyingi) huwa ni kutengeneza void zaidi. Kwa hiyo mtokaji yuko likely kutoka tena. Mwenye nyumba ndogo yuko likely kutafuta ya pili, ya tatu, na ya nne, ... kuliko hata yule ambaye hana.
SULUHISHO
Kujaribu kuwa wazi na kuwasiliana kuhusu unmet expectations kwenye ndoa zetu. Kuwa wakweli kuhusu matarajio yetu na kuwasiliana na wenzetu juu ya kile tulichokuwa tunawatarajia watufanyie. Kuwa wakweli na kukubaliana na hali inapotokea kuwa si kila tulichotarajia kitatokea kuwa vile tulivyokuwa tukifikiria. Kuwa tayari kurekebisha standards (viwango vyetu vya yale tunayotarajia kutoka kwa wenzetu). Kujua udhaifu wetu ndani ya ndoa na kujaribu kujirekebisha kila wakati. Kuwaheshimu wenzetu na kujiheshimu sisi wenyewe. Kuwa tayari KUKUBALI YAISHE, NA SI KUTAFUTA USHINDI KWA NJIA YOYOTE NDANI YA NDOA (Hata kama wewe ni fighter vipi au super star vipi lazima ukubali kuwa ndani ya ndoa kuna wakati utakuwa chini).
Smile on and enjoy!