Nyumba ndogo jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba ndogo jamani!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Fidel80, Mar 5, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Neno 'Nyumba ndogo' sio geni katika vinywa na masikio ya watu wengi. Kwa nini akina baba wanathamini sana nyumba ndogo kuliko wake zao wakubwa?Yaani mke wa kwanza.
  Nyumba ndogo inatunzwa na kuthaminiwa sana kuliko mama wa watoto wa nyumbani....baba anajali sana na kusikiliza nyumba ndogo na hata huduma zinatolewa zaidi kwenye nyumba ndogo....
  Kwa nini akina baba wanapenda sana nyumba ndogo?
  Nyumba ndogo zinajua sana kuwaliwaza akina baba?
  Nyumba ndogo zinajua sana mahaba?
  Nyumba ndogo zinajua sana kubembeleza akina baba?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Labda nyumba ndogo inahudumiwa zaidi kutokana na nyumba ndogo kujua kwamba tayari kuna mwenye mali hivyo ili kuhakikisha huduma nzuri toka kwa njemba mama wa nyumba ndogo huongeza vikolombwezo katika departments zote ili kuhakikisha njemba inarudi kila kukicha maana nyumbani njemba haipati huduma nzuri kama za nyumba ndogo.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu BAK nimekupata.
  Kwa hiyo nyumba ndogo inaongeza makorombwecho kibao kama unavyo pika pilau.Yawezekana Nyumba kubwa zikisha wekwa ndani zinajisahau ndo maana wanazidiwa kete na nyumba ndogo katika idara ya mambo ya makulaji na masix kwa six.
   
 4. Tulamanya

  Tulamanya Senior Member

  #4
  Mar 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fidel,

  Wewe umeoa?if yes, ndoa yako ina muda gani?

  Kama ndoa yako ina umri wa zaidi ya miaka mitano......try wewe mwenyewe small house...nakwambia utachonga mzinga huko!
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Unajua predators wanawake wanaoiba waume za watu wako wengi siku hizi!

  Na wametoa tu makucha..yaani mwanaume akinasa hautoki!

  Mimi sijui akina baba kwa nini wanakubali kunaswa kirahisi hivi na ujanja wao!

  Taabu tu hizi nyumba mara nyingi huchochea maambukizi mapya ya ukimwi..na istoshe maambukizi mapya ya ukimwi Tz ni kwa wanandoa zaidi ya waliko single!

  Kubwa kwa kina baba ni kujiepusha sana na hawa preditors..ili wasije wakanaswa!

  Wake ndo wana jukumu la kuwafundisha waume zao mbinu za kuepukana na hawa predators wanaoiba waume za watu!
   
  Last edited: Mar 5, 2009
 6. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama lilivyo jina "Nyumba Ndogo" ni potabo kuzimaintain...Nyumba kubwa huwa zinahitaji mambo makubwa, wakati nyumba ndogo zinajua ni ndogo hivyo zinaridhika na udogo wake...
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Mkuu nadhani ulimaanisha predators?

  anyways hili la nyumba ndogo sijui kubwa...inategemea na mtu mwenyewe na isitiche hata wenye Gf na wao bado huwa wana kuwa na tendency ya kuwa na second one so tusilaumu wenye ndoa tu zaidi ni tabia ya mtu mwenyewe
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Source yake bwana ni skills.....nyumba ndogo zina skills hasa.....zikipewa nafasi hata dakika za majeruhi lazima zitikise nyavu na kesho unahamia.....

  .....wakina mama wakishaolewa wanasahau au hawataki skilla za ki GF na kiBF.....zile tik taka hawataki tena wanaona za kitoto.....nashukuru dinah bongoradio anawafunda
   
 9. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  The bottom line ni kwamba Nyumba Ndogo inajua kwamba iko kwenye competition and will always try to impress, wanamake sure kwamba ukionja tu- lazima urudi tena na tena, na ikibidi umsahau mkeo na hata watoto, they will do whatever it takes to convince you that they are better than your 'first choice' , wakati mafirst lady wanajua kwamba wako peke yao! hawajui kwamba wana compete na yeyote na hii inawafanya wajisahau kwenye 'uboreshaji huduma' na performance kwa ujumla. Competition leads to improved products and services kama wasemavyo wataalamu wa masoko!
   
 10. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu,

  Unamshauri Fidel ajaribu uwezo wa sumu kudhuru kwa yeye mwenyewe kuionja.....what an advice!
  Phew!

  Fidel,i dont have to tell you:please,DONT.....

  Festog,talking from experience i guess.........shindwa na ulegee!Kha!
   
 11. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Hivi kumbe ndio maana unaweza kukuta mwanamme mzima kaganda kwa nyumba ndogo ya ajabu ukiilinganisha na nyumba kubwa. Yaani unakuta nyumba ndogo miguu yote ya kushoto, lakini nyumba kubwa shape namba eight, lakini jibaba limeganda kwa nyumba ndogo.
   
 12. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  That is a nature of MAN to hunt. Hatosheki na mmoja hata sikumoja.
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Nyumba ndogo sanasana ni viburudisho vya kujamiiana zaidi ya hapo ni manjonjo ambayo mwanaume anapewa kwasababu lazima atakuwa amelalamika vinavyomkera/anavyokosa Nyumba halali(Kubwa). Hivyo nyumba ndogo itajitahidi kumpa mambo anayoya-miss au yanayomkera kujaribu kuziba ufa ila siyo bure mwanaume lazima agharamikie!

  Mwanaume asipokuwa na pesa za kugharamikia hiyo nyumba ndogo anatoswa tu na service inaisha. Mwisho wake ni stress juu ya stress!

  Bora utulie na Nyumba Halali(kubwa) muishi zaidi kama marafiki siyo tu mume na mke tu. Wakati wa tendo la ndoa sema unataka nini? Tatizo mawasiliano na uoga!..Unataka ufanyiwe pedicure sema,ukunwe mgongo sema!.Utashangaa raha ya kuishi kama best friends, daima unawaza kuwa home na mkeo(nyumba halali) na watoto wako.

  Marriage is full of challenges but it worth!..
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hii inaitwa hekima.. tatizo watu wanapenda "nyumba ndogo" kwani "kubwa" hawaziwezi!!! Sisi wengine tunagandana na Nyumba kubwa tu mbele kwa mbele hizi ndogo hizi kubomoka haraka!!
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Unachosema ni kweli kabisa. Kwenye nyumba kubwwa wake kwa waume wote hujisahau na matokeo yake mapenzi hupungua. Kwa mfano utakuta kuna mambo waliyokuwa wanafanya kabla ya ndoa yao lakini baada ya ndoa yakawa hayapo tena. Mzee akirudi akisema mgongo le unaniuma naomba unikande mama wa nyumba kubwa nilikuwa busy mno leo kazini au hata nyumbani nimechoka sana siwezi kukukanda, akienda nyumba ndogo na kuomba kukandwa basi hakutakuwa na matatizo yoyote atakandwa tena huku mama wa nyumba ndogo akifanya hivyo kwa furaha. Si kweli kwamba nyumba zote ndogo zinahitaji uwe na bulungutu maana nimewaona wegi tu waliokuwa na nyumba ndogo hawana pesa kiasi hicho lakini bado walipata huduma nzur katika nyumba ndogo. Ushauri wangu ili kupunguza hili tatizo la nyumba ndogo ni wte ndani ya ndoa kutojisahau na kuona kwamba kwa kuwa umeshamuoa au kuolewa basi ukapunguza mapenzi kwa namna yoyote ile kila siku inabidi wote mjitahidi kadri ya uwezo wenu katika kila dept ya mambo ya ndoa ili muwe na ndoa iliyo na uhai.
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  MKJJ 'rekodi zetu' hapa JF so far zinaonyesha unatafuta tafuta tena huko uchagani, hizi nguvu za kuzungumzia eti una nyumba kubwa unazipata wapi? LOL
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Moyo wa binadamu hautotulia abadan asilani, usipotulia ndani ya Mola wake. Hakuna utulivu nje hapo wakulu.

  My few cents.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  MKuu Festog mi bado nipo nipo kwanza.
  Mkuu nimeshuhudia baba yangu mzazi kanasa kwa nyumba ndogo na kututelekeza sie nyumbani na mama yetu.Mzee siku hizi hata nyama haleti nyumbani kwa nyumba ndogo huko wanakula na kunywa.Basi mzee naona ameamua kuchonga mzinga kabisa kutokana na vitu adimu anavyo pewa na nyumba ndogo.
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  kweli nakubaliana kuwa kuwa wanawake wengine wakishaingia ndani huwa wanajisahau but kuna wengine hawajisahau kwa lolote ana mu handle mume wake kama wamekutana jana vile,mapenzi moto moto! lakini wapiiii huyo huyo mwanaume ana nyumba ndogo yake huko na mbaya zaidi utashtukia mpaka hiyo nyumba ndogo inakutumia msg mama nyumbani ya kukukashifu, jamani tunajionea mengi ndani! looo...kuna wale dizaini hawawezi kuwa na mwanamke 1 so kwake yeye hata umfanyaje/umpe mapenzi ya namna gani still atakuwa nayo...haaa
   
 20. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mimi kama mwanamke mpaka leo sijajua kwa nini waume zetu wanaenda nje? Hakika siyo kwamba tumebweteka, tunafanya mambo mengi na uzoefu wa kitchen party tunazopewa lakini bado utakuta mume anatoka nje.

  Nimegundua kwamba mawasiliano wa walioowana ni magumu, siyo kama mkiwa GF na BF. Utakuta vitu vingi tunafichana especially kwenye ankara kwa maana kwamba hutaki mimi nijue unapata ngapi since I can track you.

  Ushauri wangu ni mdogo, wanaume ndiyo chachu ya familia, ukiona mimi sifanyi vizuri basi nifundishe nifanye, ma first lady hatuna ubishi ukizingatia you are a husband whaterver you tell will be done. Tusione aibu kufundishana, ni katika kuepusha matatizo, utakapoenda nyumba ndogo ukanisahau mimi na watoto inakuwaje?

  ulimbukeni kwamba mke wangu hajui kufanya mapenzi, mfundishe aruke kihunzi uone kama anashindwa
   
Loading...