Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,916
- 30,259
- Thread starter
- #61
Mrangi,Hivi waarabu hawajafanya biashara ya utumwa
Ova
Ukitaka kuelewa biashara ya utumwa anza na Across Atlantic Slave Trade kisha Belgian Congo Slave Trade.
Mrangi,Hivi waarabu hawajafanya biashara ya utumwa
Ova
Ni kweliMaandiko yako ni elimishi lakini mara zote huwa yana mlengo wa kidini! Siku zote unaandika kwa namna ya kulalamika.
Kwahiyo African Association kilikuwa chama cha kidini cha waislamu kama Muslim brotherhood cha Masri?Trace...
Umesema kweli kabisa.
Wakoloni waliwachukua Waislam kama maadui zao na wakafanya kila hila kuwahujumu.
Hii ndiyo sababu Wajerumani katika Vita Vya Maji Maji waliwanyonga makamanda zaidi ya 60.
Makaburi yao yapo Mahenge, Songea.
Walipokuja Waingereza hali haikubadilika na Waislam wakaunda African Association kuwakusanya Waafrika kwenye umoja ulikuja kuzaa TANU.
Historia hii ilipokuja kuandikwa ilifanyiwa hujuma kubwa.
Nimenyanyua kalamu kusahihisha historia hii kwa kueleza nafasi ya Uislam na Waislam katika kupambana na ukoloni.
Mkwawa alikuwa na urafiki mkubwa na Waarabu na alikuwa akifanya nao biashara ya pembe za ndovu na wao waarabu ndio waliompa bunduki Mkwawa kwa mara ya Kwanza.Kweli hii ni changamoto kubwa kwa Mzee wetu halafu ulalamishi wenyewe mm sioni mantiki maana Wote Abushiri tumemsoma mashuleni ila hapa Mzee anakwambia majina yao yamekwepwa ila kwa upande wangu leo ndio nimesikia kuwa kumbe Mutwa Mukwava mukwavinyika Akiitwa Abdalah kiukweli nilikua sijapata kulisikia jina hili kabla
Kwahiyo alikua Dalali?Mkwawa alikuwa na urafiki mkubwa na Waarabu na alikuwa akifanya nao biashara ya pembe za ndovu na wao waarabu ndio waliompa bunduki Mkwawa kwa mara ya Kwanza.
Na hata mavazi asili ya wahehe ya kuvaa mashuka meupe ni Mkwawa ndio aliletewa hayo mashuka na Waarabu na ndio limekuwa vazi lao la asili kama unavyoona Wamasai.
Ni kweli Mkwawa aliingia kwenye uislamu kwa sababu Waarabu ndio walikuwa washkaji zake na hapakuwa na dini kwenye nchi ya uhehe.
Ni kweli
Lakini chukua elimu
Mengine yaache
Chivala.Huyo Abushiri ana asili ya nchi gani?
Wyatt,Mkuu
Wadini wakubwa ni hawa hapa:
View attachment 1948117
Huyu wewe utaona ni sawa na hamna mtu wa kumuambia chochote wewe included.
Mnaona ni sawa mpumbavu huyu kuleta one religion supremacy ideas wakati Mohamed Said anatuletea historia with facts ambapo it happens in characters ndani wana majina ya Kiislam wala hajaja na idea binafsi za supremacy za kidini hapa
Sijui kwanini mtu wa dini fulani akiona dini ingine anakua uncomfortable kabisa bila hata kuambiwa chochote kile?
Get used to others,infact wewe ndio sio tolerant,infact this speaks more of your udini sentiments more than anybody's else
Dini zenu binafsi wekeni vichwani mwenu,sisi tusio na dini tunawashangaa sana...
Historia imejengwa na watu,na hawa watu happen to have dini na majina ya dini zao,leo Mohamed katuletea historia ya hawa wanadamu..
Ulitaka alete za wanadamu wenye majina ya kikikristo?Itakua ni biased na not factual..kaleta kitu kilivyo regardless!
Janja...Alifanya sana
Na Mohammed Said ni zao
Sijui nimuite vipi, ila mbuga ya Ruaha ipo Iringa, na yeye ndio alikuwa mtawala wa nchi ya Uhehe, kwahiyo alikuwa akitumia rasilimali zao za Uhehe kuwauzia Waarabu.Kwahiyo alikua Dalali?
Hujasikia Waafrika walifanya biashara ya watumwa? Biashara huwa na pande mbili: anayeuza na anayenunua. Pamoja ya yule anayezalisha bidhaa.Hivi waarabu hawajafanya biashara ya utumwa
Ova
Hamza mwengine...!Maandiko yako ni elimishi lakini mara zote huwa yana mlengo wa kidini! Siku zote unaandika kwa namna ya kulalamika.
Geza...Hamza mwengine...!
sasa usalama wa huyo Mholanzi aliyeuziwa kiwanja na serikali unakaaje? Yeye kama hakujua anahukumiwa vp? Huoni maandishi yako yana chembe ya kujenga chuki? halafu tafiti zako ni historia ya Waislam tu? Mbona Mkwawa alikuwa Muislam wenzio walifanya tafiti na hawakulenga kum-categorize kwenye Uislam bali kama chief aliyepigania maslahi ya wananchi wake?Gear...
Sijui una maana gani kusema "kulalamika."
Ikiwa historia iliyoandikwa si kweli akatokea mtu akasahihisha kama nilivyofanya huku ni kulalamika?
Wataalamu wanakichukulia kitabu changu kama "corrective history."
Wewe umetoa maoni yako unasema naandika "dini," je huku ni kulalamika au ni kueleza fikra zako?
Mimi nimefanya utafiti katika historia ya Waislam kutaka kujua kwa nini wao walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na Wajerumani na pia Waingereza na kwa nini Wengine walikuwa nyuma.
Nikaenda mbele zaidi kutaka kujua kwa nini baada ya Tanganyika kukombolewa kukazuka matatizo ya ubaguzi dhidi ya Waislam?
Hii ni "field of enquiry," mfano ambao wasomi kote ulimwenguni hufanya ili kujua tatizo liko wapi na kutafuta ufumbuzi wake.
Geza...sasa usalama wa huyo Mholanzi aliyeuziwa kiwanja na serikali unakaaje? Yeye kama hakujua anahukumiwa vp? Huoni maandishi yako yana chembe ya kujenga chuki?
Mzee, ukiuliza maswali kuhusu ubaguzi wa waislamu katika Tanganyika unauliza maswali yenye maana.Mimi nimefanya utafiti katika historia ya Waislam kutaka kujua kwa nini wao walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na Wajerumani na pia Waingereza na kwa nini Wengine walikuwa nyuma.
Nikaenda mbele zaidi kutaka kujua kwa nini baada ya Tanganyika kukombolewa kukazuka matatizo ya ubaguzi dhidi ya Waislam?
Mwana...Mzee, ukiuliza maswali kuhusu ubaguzi wa waislamu katika Tanganyika unauliza maswali yenye maana.
Ila sijui itasaidia nini ukipinda historia ya Waislamu na ukoloni?
*Ni kweli kwamba Waislamu walipatikana kwenye mstari wa mbele wa kupinga mwanzo wa ukoloni wa Wajerumani. Umetaja mifano
`*Ni kweli pia kwamba uvamizi wa kikoloni katika Tanganyika ulitekelezwa na wanajeshi Waislamu chini ya maafisa Wajerumani. Maana jeshi la kijerumani la Schutztruppe lilianzishwa hasa na askari mamluki kutoka Nubia (Misri kusini / Sudani kaskazini) na hao "Wasudani" walikuwa uti wa mgongo wa jeshi la "Kijerumani" kwa miaka mingi. (lilipoanzishwa 1888 na Wissmann lilikuwa na maafisa 21 na masajini 40 kutoka Ujerumani, askari mamluki Wasudan 600 walioongezwa na Wazulu 150 kutoka Msumbiji)
*Ni kweli kwamba utawala wa kikoloni ulitegemea Waislamu waliojua kuandika na kusoma; Wajerumani walikuwa wachache mno; walipompata chifu aliyeweza kushirikiana nao, walimtumia chifu kwa kusimamia eneo. Pale ambako hawakukuta machifu, waliweka maakida waliosimamia maeneo ya vijiji kadhaa. Siwezi kukumbuka kutoka miaka ya kwanza hata akida mmoja ambaye hakuwa Mwislamu. Ukali wa maakida ulikuwa sababu muhimu ya Wamatumbi kujiunga na harakati ya Kinjitikile; akida wa kwanza aliyeshambuliwa na wanamajimaji aliitwa Sefu bin Amri.
* Wamisionari Wajerumani walilalamika mara kwa mara kwamba jeshi la kikoloni lilisambaza Usilamu kote Tanganyika. Maana kwa wenyeji wengi uso wa utawala wa kikoloni haukuwa yule Mjerumani mmoja aliyekaa mbali nao kwenye boma lake (vituo vichache nchini), lakini askari wa kikoloni aliyepita katika vijiji vyao ambaye alikuwa mara nyingi Mwislamu;
*umefanya utafiti kuhusu historia ya akina Sykes; ukiuliza kwa nini mamluki Mzulu anageukia Uislamu jibu mojawapo ni kwamba alikuta askari wenzake wenye vyeo na heshima katika jeshi la kikoloni walikuwa Waislamu, sivyo? Aliendelea kwa uhodari kueneza utawala wa Kijerumani kote alipotumwa - na pia kueneza dini yake.
Sitaki sasa kugeuza masimulizi yako kinyume, au kuwashtaki Waislamu.... Lakini historia halisi ina nyuso nyingi. Kuteua yale tu ambayo mimi au wewe tunapenda haileti picha ya kweli.
Pitia hiki kitabu ili uipate Historia mujarabuHujasikia Waafrika walifanya biashara ya watumwa? Biashara huwa na pande mbili: anayeuza na anayenunua. Pamoja ya yule anayezalisha bidhaa.
Kwa jumla Waafrika walizalisha bidhaa yaani watumwa kwa kukamata wafungwa, halafu kuwauza. Waarabu walikuwa wateja wakubwa, hasa katika biashara ya kuwapeleka ng'ambo;
tangu Waingereza walibadilika kutoka wafanyabiashara wakuu wa watumwa kuwa wapinga biashara hiyo, waliwasumbua Waarabu karika Afrika ya Mashariki hivyo walianza kutumia watumwa wengi kwa kazi kwenye mashamba waliyoanzisha pwani na Unguja.
Kwa hiyo: unataka kusema nini Waarabu walifanya biashara ya watumwa? Nisipokosei watu wa pekee ambao hawakufanya biashara ya watumwa walikuwa Maasai.
Kaka usirejelee kitabu fulani ambacho hutaji. Afadhali eleza: hao watumwa walionunuliwa na Waarabu waliuzwa na nani???Pitia hiki kitabu ili uipate Historia mujarabu
Mambo yanaenda FaizaWa Aleykum salaam.