Nyumba imejengwa juu ya kaburi la Abushiri bin Salim al Harith

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,900
30,235
JUU YA KABURI LA BUSHIRI BIN SALIM PAMEJENGWA NYUMBA

Nimesoma historia ya Bushiri nikiwa shule ya msingi miaka ya 1960 pamoja na historia ya Vita Vya Maji Maji vilivyopewa jina la, "Maji Maji Rebellion."

Walioandika historia hii waliwaona Abushiri bin Salim, Abdulrauf Songea Mbano na Bi. Khadija Mkomanile, Mtwa Abdallah Mkwawa kwa kutoa mfano kutoka kundi la viongozi walioongoza vita dhidi ya Wajerumani si chochote ila waasi.

Kama waasi hukumu ya wao kunyongwa ilikuwa stahili yao.

Bushiri alitembezwa nusu uchi katika barabara za Pangani wakati anapelekwa kunyòngwa na huko alikotolewa alipokuwa amefungiwa Bushiri aliwekwa ndani ya chumba akiwa hana nguo.

Bushiri alikuwa kiongozi katika jamii yake aliyoishi na mtu aliyestahika kwa hiyo kumvua nguo hadharani kulikusudiwa kumwondolea heshima yake.

Kiasi cha miaka 20 iliyopita nilifika Pangani kwa nia ya kuzuru kaburi la Abushiri, kuutembelea msikiti ulioingizwa mbwa, kuona msikiti uliong'olewa mlango wa Kizanzibari uliokuwa na aya za Qur'an ukenda kufungwa bar panapouzwa ulevi na mwisho kutafuta baadhi ya nyumba walizoishi wazee wetu tuliopokea historia zao baada ya wao kufariki yapata miaka 100 nyuma.

Hakuna aliyekuwa anajua ni msikiti upi ulioingizwa mbwa enzi za Bushiri lakini nilionyeshwa na nilisali dhuhur katika msikiti uliong'olewa mlango.

Wala sikuwa na haja ya kuuliza kwani ule mlango mpya uliowekwa ulikuwa unachusha kama vile unasema, "Ning'oeni mahali hapa."

Nilifahamishwa na kiongozi mmoja mkuu wa serikali kuwa serikali ilikuwa ipo katika mchakato wa kulitafuta kaburi la Abushiri lakini bado hawajafanikiwa.

Kiongozi huyu wa serikali alinifahamisha kuwa serikali imeamua kulitafuta kaburi la Abushiri kwa sababu watu wengi kutoka nje ya Tanzania wamekuwa wakifika Pangani kwa nia ya kuliona kaburi lake.

Nilifahamishwa kuwa si mbali na Pangani sehemu inayoitwa Mahiwa kuna sehemu Bushiri alikuwa na makazi yake hapo na sehemu hiyo anaishi Mholanzi mmoja.

Nilikwenda hadi Mahiwa na nilipokelewa na huyo Mzungu.

Huyu Muholanzi alikuwa amejenga nyumba yake ya ghorofa moja pembeni ya Mto Pangani na aliniambia kuwa yeye amesikia kutoka kwa wenyeji kuwa Bushiri alipata kuishi hapo ambapo yeye alipojenga.

Sehemu hii imejitenga sana hakuna nyumba yeyote jirani.

Huyu Mzungu hakuwa anajua lolote kuhusu Abushiri ila hili la kunyongwa na Wajerumani.

Inawezekana hapa ndani msituni ndipo Bushiri alipojenga ngome yake na kuweka kambi wakati wa vita ile dhidi ya Wajerumani.

Lakini zipo taarifa kuwa hadi miaka ya 1960 wakati mimi nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi na nikifundishwa historia ya "uasi," wa Abushiri dhidi ya Wajerumani watu wa Pangani walikuwa wanajua wapi alipozikwa Bushiri.

Watu walikuwa wanajua sehemu kaburi la Abushiri lilipo ingawa kaburi lenyewe lilikuwa halionekani kwa kukosa matunzo.

Alipozikwa Abushiri kwa kwa wakati ule mwaka wa 1889 hapo palikuwa pori.

Wajerumani walimzika Abushiri porini pasipokuwa na watu wala makaburi akiwa kijana wa miaka 36.

Wajerumani walimzika Bushiri msituni kutokana na chuki waliyokuwa nayo dhidi yake na kwao wao walichukulia kitendo kile sawa na kufukia kitu kinachoudhi.

Wajerumani wakati wakimzika Bushiri porini, maiti za Wajerumani askari waliouawa na askari wa Bushiri zilizikwa katika viwanja makhsusi vya makaburi kwa heshima zote.

Makaburi haya ya Wajerumani yapo Pangani hadi leo na historia ya vifo vyao inafahamika.

Ukiingia Pangani kwa mara ya kwanza utapigwa na butwaa na utajiri wa historia iliyoko bayana mbele ya macho yako.

Halikadhalika utasikitishwa na magofu ya nyumba zilozojengwa zaidi ya karne mbili zikiachiwa zibomoke hadi zitoweke.

Watu niliowakuta Pangani miaka 20 iliyopita hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua historia ya Bushiri kwa ukamilifu wake wala kujua katika nyumba zile zilizobaki magofu Bushiri alikuwa akiishi nyumba ipi.

Lakini nilifanikiwa kuona msikiti wa Ibadh ukiwa bado umesimama katika hali yake ile ilivyokuwa wakati Bushiri katika uhai akisali.

Nilifarajika sana mwenyeji wangu kutoka Tanga aliyenisindikiza Pangani aliponionyesha gofu la nyumba iliyokuwa ya Suleiman Nasr el Lemki aliyekuwa Liwali wa Pangani wakati Bushiri na jeshi lake walipoamua kunyanyua silaha dhidi ya Wajerumani.

Taarifa ni kuwa kaburi la Bushiri bin Salim Al Harith lipo Pangani na sasa kaburi hili halipo tena porini.

Palipimwa kiwanja na mnunuzi wa kiwanja hiki amejenga nyumba yake juu ya kaburi la Abushiri.

Mengi yameandikwa kuhusu Wajerumani walioshiriki katika vita hivi lakini hakuna chochote kilichoandikwa kuhusu askari Waafrika walioletwa Pangani na Hermann von Wissman kutoka Sudan na Mozambique.

Kama Kleist Sykes asingeandika maisha yake na kueleza historia ya baba yake Sykes Mbuwane aliyepigana vita vile Bagamoyo dhidi ya Bushiri historia hii kwa upande wa Waafrika ingekuwa imepunjika pakubww.

Kutokana na kalamu ya Kleist ndipo leo tumefahamu kuwa von Wissman alipoamua kushambulia kambi ya Bushiri iliyokuwa Nzole nje ya Bagamoyo pamojanae alikuwapo Chief Mohosh (Affande Plantan), Sykes Mbuwane Chakulan na Machakaomo kwa kuwataja Wazulu wachache katika Wazulu 400 waliokuwa askari mamluki.

Wissman alishambulia kambi ya Abushiri tarehe 8 May 1889.

Haya majina ya hawa Wazulu waliopigana vita vyao vya kwanza Bagamoyo yapo katika mswada wa kitabu alioandika Kleist kabla hajafa mwaka wa 1949.

Na historia hii yote Kleist aliisikia kutoka kwenye kinywa cha mlezi wake Affande Plantan baba yao Thomas Plantan, Schneider Plantan na Mashado Plantan akaiandika kabla hajafa mwaka wa 1949.

Sishangai kwa nini wanahistoria hawampi Abushiri hapewi heshima sawa na ile anayopewa Mtwa Mkwawa na wala sistaajabu kwa nini jina lake la Abdallah halitosis katika maandishi yao kama vile yalivyokwepwa majina ya Abdulrauf Songea Mbao na Khadija Mkomanile.

Baada vita dhidi ya Bushiri na Mkwawa kumalizika Chief Mohosh sasa akijulikana kama Affande Plantan akafanywa kuwa mkuu wa Germany Constabulary katika Tanganyika.

Affande Plantan alifariki 1914 Vita Vya Kwanza Vya Dunia vikiwa tayari vimeshaanza na majeshi ya Uingereza yapo ndani ya ardhi iliyokuja kujulikana baada ya vita kama Tanganyika.

Kila ninapokwenda kumsalimu Mwalimu Maunda Plantan mjukuu wa Chief Mohosh, bint ya Mwalimu Thomas Plantan huondoka na jipya ambalo sikupata kulijua kabla.

Picha: Picha ya kitabu kinachoeleza kwa ufupi hali ilivyokuwa Bagamoyo wakati wa mapambano, gofu la nyumba ya Suleiman Nasr el Lemki na mtaa wa biashara Pangani kama ulivyokuwa mwaka wa 1910.

20210910_022544.jpg

Screenshot_20210910-091924_Facebook.jpg

Screenshot_20210910-022455_Chrome.jpg
 
Affande Plantan alifariki 1914 Vita Vya Pili Vya Dunia vikiwa tayari vimeshaanza na majeshi ya Uingereza yapo ndani ya ardhi iliyokuja kujulikana baada ya vita kama Tanganyika.

Kila ninapokwenda kumsalimu Mwalimu Maunda Plantan mjukuu wa Chief Mohosh, bint ya Mwalimu Thomas Plantan huondoka na jipya ambalo sikupata kulijua kabla.

Picha: Picha ya kitabu kinachoeleza kwa ufupi hali ilivyokuwa Bagamoyo wakati wa mapambano, gofu la nyumba ya Suleiman Nasr el Lemki na mtaa wa biashara Pangani kama ulivyokuwa mwaka wa 1910.

View attachment 1931577

View attachment 1931578

View attachment 1931579
Maandiko yako ni elimishi lakini mara zote huwa yana mlengo wa kidini! Siku zote unaandika kwa namna ya kulalamika.
 
Abdallah...
Umesema kweli kabisa.

Naandika historia iliyochukiwa na wakoloni wakaifanyia khiyana.

Kama nisingeandika historia hii wewe ungeijuaje?

Ni kweli khiyana hiyo ilifanywa kwa faida ya wakoloni dhidi ya Watanzania.Nashangaa Mtanzania analalamika badala ya kupongeza.Mimi nadhani tuwafundishe Watanzania kutokuamini ukweli ukisemwa juu ya uislam ni udini,au ukweli ukisemwa juu ya ukristo ni udini.
 
Nikiwa shule nilikuwa najua Abushiri na Bwana Heri ni mtu mmoja, sasa ni anaitwa Abushiri au Bushiri au ni mimi nachanganya mambo hapa kati kati Mzee wangu naomba nieleweshe hapo na huyo Bwana Heri ndio nani maana tumewaimba sana shuleni (miaka ya 2000)
 
Mgeni...
Ingia Ģoogle utasoma mengi kuhusu watu hawa.
 
Mohamed Said, siku moja tuandikie lolote kuhusu Mchungaji Mtilia Christopher
Kwa ufahamu wangu Mzee Mohamed huwa anaandika historia alizosimuliwa na wazee wake wa Kariakoo wa enzi za wakati kabla ya uhuru, na Kariakoo ya wakati ule kama ilivyokuwa kwa miji mingi ya Pwani (Dar Es salaam yote hadi Mkoa wa Pwani kwa sasa, Tanga, Lindi na hata Mombasa) ilijaa waislam kutokana na athari ya kuwa chini ya Utawala wa waarabu kwa muda mrefu, ndio maana rejea zake nyingi ni za watu
 
Usishangae ndo walivyo, huoni wanadai alexandre the great alikua muislam.
Bhachu...
Usidhani nafanya maskhara nakueleza kweli.

Jina lake Abdallah na katika makamanda wake alikuwa na nduguye anaitwa Yusuf.

Kwani wangapi wanajua kuwa Songea Mbano jina lake ni Abdulrauf?

Wangapi leo wanajua kuwa Mkomanile jina lake ni Khadija?

Wangapi wanajua kuwa Kleist Sykes jina lake ni Abdallah au Schneider jina lake ni Abdillah?

Nenda Kalenga ukaone barua alizokuwa akiandika Mkwawa.

Utapigwa na bumbuazi.

Au wangapi walikuwa wanajua kuwa kadi no1 ya TANU ya Julius Nyerere alipewa na Ally Sykes na yeye akachukua kadi no 2 na no 3 akamwandikia kaka yake Abdulwahid.

Kwani hawa hata kwenye historia ya TANU umepata kuwasoma?

Nini kinakushangaza?
 
Back
Top Bottom