Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 356
- 1,605
HII NDIO HISTORIA YA FAMILIA YA SYKES.
Historia hii inaanzia kwa MZEE SYKES MBUWANE KLEIST. Huyu ndiye baba yake KLEIST SYKES.
MZEE SYKES MBUWANE KLEIST ni nani?
Sykes Mbuwane ni mamluki wa KIZULU aliyechukuliwa yeye na vijana wenzake wa kizulu kutoka kijiji cha LIKUNYI MSUMBIJI.
Walifikaje Tanganyika?
Kipindi cha UTAWALA wa kikoloni wa kijerumani chini ya HERMANN VON WISSMAN aliwachukuwa kwa meli ya kivita kama askari mamluki mpaka Pangani Tanga, Tanganyika kuja kupigana na ABUSHIRI BIN SALIM AL HARITH NA MTWA MKWAWA WA IRINGA.
KLEIST SYKES ALIZALIWA WAPI?
KLEIST SYKES alizaliwa mwaka 1894, Pangani Tanga kwa baba yake SYKES MBUWANE KLEIST na MAMA yake ni Mnyatulu, baada ya baba yake kufariki Kleist Sykes baadae alikuja Dar es salaam.
MAISHA YA KLEIST SYKES BAADA YA KUJA DAR.
KLEIST SYKES alimuoa Bi MLUGURU BINT MUSSA, na alibahatika kupata watoto watatu wa kiume.
(1) ABDULWAHEED KLEIST SYKES. (1924__1968).
(2) ALLY KLEIST SYKES. (1926__2013).
(3) ABBAS KLEIST SYKES. (1929__2021).
Kama inavyoonekana katika Picha namba (1). Waliosimama kutoka kulia ni Abdulwaheed Kleist Sykes, na Ally Kleist Sykes. Aliyekaa kutoka kulia ni Abbas Kleist Sykes na Baba yao mzazi Mzee Kleist Sykes.
Picha hii ilipigwa 1942, kipindi Abdulwaheed Kleist Sykes alipokuja kumuaga baba yake akitokea LOWER KABETE KENYA mafunzoni kabla ya kwenda BURMA kama Askari wa KAR BURMA INFANTRY. Na picha namba 2, ni MZEE ALLY KLEIST SYKES kipindi cha uhai wake.
Vile vile MZEE KLEIST SYKES ALIKUWA NA WAJUKUU.
Wafuatao ni baadhi ya wajukuu wake:
(1) EBRAHIM (EBBY) ABDULWAHEED KLEIST SYKES. 1952__2015). Kama anavyoonekana katika picha namba 3. Huyu ndiye Baba yake mzazi DULL SYKES msanii wa bongofleva.
(2) MUSSA ABBAS KLEIST SYKES.
(3) KLEIST ABDULWAHEED SYKES. Alifariki 22 novemba 2017.
(4) ABRAHAM ALLY KLEIST SYKES.
ASANTENI: