Nyumba iliyochomwa na FFU Mtwara

Nyumba iliyochomwa na FFU Mtwara

BURIANI KAMANDA KARIM: KIFO CHA HUYU KIJANA SASA HUENDA UKALETA MAANA MPYA KABISA NA LISILOTARAJIWA KATIKA SWALA ZIMA LA SAKATA YA GESI KUFULIWA KUSINI AU BAGAMOYO:yell:

SAWA NA KIJANA BUAZIZI WA TUNISIA ALIYEWATIA MACHUNGU TAIFA ZIMA NA UMMA NCHI HIYO KUONA HERI KUTIMUA SERIKALI FISADI NCHINI HUMO NAYE HAYATI KARIM ANAINGIA KATIKA HISTORIA KUWA NI SHUJAA WA KUTETEA GESI YA KUSINI IWAONDOLEE MDHALILIKO WA 'KUITWA MACHINGA WASOTAJI WA KUDUMU KAMA WANAVYOJULIKANA JAMII YA KUSINI MWA NCHI HII.

KALALE SALAMA KIJANA MWENZETU NA YULE MAMA MJAMZITO MLIOONDOLEWA ROHO KWA KUTOA TU MAONI YENU KWAMBA GESI IPATE KUFULIWA HUKO HUKO KUSINI KABLA YA KUSAFIRISHWA ILI MIKOA HII ILIOSAHAULIKA NAYO IPATE KUENDELEA.

KAMANDA KARIM INGAWAJE UMEANGUSHWA LEO HII KUTOKANA NA UBINAFSI NA MASLAHI YA BAADHI YA VIONGOZI WETU WACHACHE KULAZIMISHWA KUFUNIKA MASLAHI YA WALIO WENGI, HATA HIVYO KILE KILICHOKUFANYA UKAANGUSHWA KWA RISASI KAMWE HAITOANGUSHWA NA MTU AWAYE YEYOTE YULE.

NASEMA KALALE SALAMA KAMANDA KARIMU:

:shock:

:yell:
Pumzika kwa Amani ya Bwana, kijana na mpiganaji wa ukweli umeshindana na wadhalimu wa nchi hii umeshinda tena ushindi wako ni wa kipekee na siku yaja kuudhiilika kuwa tanzania ni yenye neema kwa wote na mwisho wa mafisadi utakua umekwisha.. Amani na mwanga wa nuru ya bwana ikuangazie siku ya ushindi wa mauti na uzima wa milele, Mungu Baba na mwanaye Yesu kristo wakuepushe na adhabu ya kaburi umeshinda karimu lala salama kamanda.
 
Wananchi wakichoma nyumba, mahakama, magari, ofisi na kuharibu miundombinu mnashangilia tena kuhamasisha juu kuwa waendelee kuchoma. Ila ikisemwa polisi wamechoma mnawaandama polisi na kuwalaani kwa nguvu zote kana kwamba wakati nyumba inachomwa mlikuwa mnashuhudia na kuhakikisha kuwa kweli aliyechoma ni polisi.
Maboso ni mapovu ya pombe, hasa ulanzi.... Yale magunia 18 si ya polisi? Lile fuvu halikuwa lao? Polisi wamekuwa majambazi siku hizi... Wanatumia madaraka yao vibaya
 
Hivi CCM wataenda kuomba kura Mtwara kwa style gani? kwa bendi ya TOT na bongo flavor au wataenda wakiwa wabubujikwa machozi ?
 
Casualities are not those who gladly died in battle field defending their rights,nor those whose houses were burnt down by instruments of power,neither the defenceless pregnant mother raped and shot in stomach. True casuality is the state, by unleashing wanton terror on its citizen the state has inadverntely signed its own death warrant.
 
Yote kwa yote askali police either kwa maksudi au kwa umbumbumbu wao wameingia kunako mtego wa watawala bila kujua .Nasasa kwakuwa wanaajiri ajiri tu hata wezi kwani askar wa sasa hawana maadili

Sitaki kuamini kama Askar we2 hawana Maadili vp mbna hauzungumzii nyumba za askari za uraiani zilizochomwa Nyambafu kabsa
 
Mkuu kazi yao ndio hapo juu kwenye picha jinsi gani serikali inavyotia umasikini raia wake kwa kutumia dola tena.

Sitaki kuamini kama Askar we2 hawana Maadili vp mbna hauzungumzii nyumba za askari za uraiani zilizochomwa Nyambafu kabsa
 
Wananchi wakichoma nyumba, mahakama, magari, ofisi na kuharibu miundombinu mnashangilia tena kuhamasisha juu kuwa waendelee kuchoma. Ila ikisemwa polisi wamechoma mnawaandama polisi na kuwalaani kwa nguvu zote kana kwamba wakati nyumba inachomwa mlikuwa mnashuhudia na kuhakikisha kuwa kweli aliyechoma ni polisi.

Hujui usemalo!!
 
Maboso ni mapovu ya pombe, hasa ulanzi.... Yale magunia 18 si ya polisi? Lile fuvu halikuwa lao? Polisi wamekuwa majambazi siku hizi... Wanatumia madaraka yao vibaya

Ni kweli kabisa maboso ni mapovu ya pombe ya ulanzi ambayo watu kama wewe mnapenda kuyatumia na hivyo kujikuta mnatokwa tu na mapovu mdomoni kama ambavyo umedhihirisha hapa. Mie nazungumzia ishu ya mtwara wewe unaleta mambo ya Morogoro na Arusha.
 
Mie nahisi ni dalili njema za ukombozi ambazo hata baadhi ya watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaamua kukubaliana na mabadiliko hayo lakini ktk njia ambayo siyo rahisi wananchi na mtu mwingine kuamini kuwa kinachohitajika ni mabadiliko na wanatumia njia hii kutokana na sheria na taratibu zao za kazi(ngoja niwe wazi wanabaka,wanaua,wanachoma na kufanya kila aina ya uonevu ili wananchi wakasirike na wafanye maamuzi sahihi juu ya utawala mbovu uliopo)nani asiyejua matatizo waliyo nayo maaskali wetu?,wanalala ktk magofu,mishahala mibovu na wanafanya kazi ktk mazingira magumu kwani wao siyo watanzania hakuna ndugu zao wanaodhurika?ni swala la wakati tu ukifika tutaujua ukweli.:embarassed2:NI MTIZAMO WANGU
A%20S%20kiss.gif

Inahitaji watu wenye akili sana kulielewa hili, subiri Maboso aone hii hoja uone atakavyo kudhihaki!
 
Taratibu mkuu hebu acha kujichekesha ovyo mtindo huo hapa msibani kwa utakua hueleweki kabisa kwa mtu yeyote humu!!!!!!!!

Ni kweli kabisa maboso ni mapovu ya pombe ya ulanzi ambayo watu kama wewe mnapenda kuyatumia na hivyo kujikuta mnatokwa tu na mapovu mdomoni kama ambavyo umedhihirisha hapa. Mie nazungumzia ishu ya mtwara wewe unaleta mambo ya Morogoro na Arusha.
 
kinachonchekesha mimi kuna mijitu inaijibia serikal mambo yote wakat yenyewe ni milala hoi viraka mpaka matakoni bata nyie.
 
mbona wakuu hamzungumzii nyumba takribani &nbsp;20 za polisi waliojenga uraiani zilizochomwa moto baada ya kuporwa vitu vyote vya ndani siku ya tarehe 22 tuache unafiki<br>:

wewe ni polisi....wacha ujinga
 
Mkuu Maboso!...Mtazamo wako hauko sahihi katika mada hii. Sijambo linaloingia akilini kusikia polisi wa nchi ya kidemokrasia kama tanzania wana choma moto nyumba ya raia asiye na hatia, kubaka na kupiga risasi mwananchi kwa kisingizio cha kutuliza ghasia. Chaajabu zaidi ni pale walipochoma moto nyumba na kufanya ubakaji na uporaji baada ya tukio la vurugu kuwa limekwisha sitishwa!
Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya utendaji wa jeshi la polisi; ubambiliaji wa kesi, utesaji, ubabe na kutumiwa na chama cha mapinduzi katika uvunjaji wa sheria na ukandamizaji wa haki za binadamu lakini wakuu wa nchi hii kwakuwa wanafaidika na udhaifu huu wa jeshi wamekuwa wakitoa pongezi kwa askari hawa kama alivyofanya lukuvi ndani ya bunge. watu kama kamuhanda wanapata jeuri ya kufanya chochote bila hofu.
viongozi wa serikali na wanasiasa (hasa wa chama tawala) nao wamekuwa wakijifanyia lolote wanalotaka na hata kusababisha madhara; hakuna anayesikiliza na mwananchi amekata tamaa kwani hawajui wapeleke wapi malalamiko yao. Ipo mifano mingi lakini kwa uchache tukio la ghasia katika chuo cha uhasibu arusha, hotuba waziri muhongo iliyo jaa nyodo na kebehi hadi kusababisha vurugu mtwara, uingiliaji wa polisi katika maandamano ya amani ya vyama vya upinzani au wanaharakati na mengine mengi.
Jeshi la polisi linatakiwa kusukwa upya! lakini hili halita wezekana hadi chama goigoi cha mapinduzi na serikali yake dhaifu itakapo toka madarakani.
 
kama kweli wamechoma unazani hao watoto watakuwaje hata wakikua? Polisi na serikali tumieni akili kutatua matatizo nje ya hapo munaandaa bomu la ajabu sana hata ikiwezekana ugaidi maana roho zinakuwa zimesha nyanyaswa sana wakiwa dogo wakikua basi kabisa wanakuwa na element za liwalo na liwe
 
Hii nimeitoa IPPMEDIA:

A woman shows her house alleged to be burnt by Field Force police during the operation to calm the situation erupted after anti-gas transportation from Mtwara to Dar es Salaam clashed by riot police on Wednesday at Magomeni in Mtwara region. Situation in Mtwara is calm but remains tense.

View attachment 95077
jamani, la kuambiwa tuna changanya na akili zetu. Nyumba iliyochomwa inafanana hivi?! Mbona miti iliyosimamisha nyumba haina hata dalili za kuguswa na moto?! Hata udongo uliojenga nyumba hiyo hauna dalili za rangi ya moto! Tena Inaonesha haijawahi kukaliwa na familia husika. WaTZ kwa uongo 100/100. Cha kusikitisha hata wasomi Kama wewe!!!
 
Mkuu. Ni vizuri kusoma habari yote vizuri kama ulivyoaingalia hiyo picha. Kama umesoma habari yenyewe nimesema kwamba hii picha na habari nimeitoa kwenye tovuti ya IPPMEDIA. Sikuongeza neno moja zaidi kuhusu picha wala habari. Maneno yako ungepaswa kuyaelekeza kwa mwandishi wa habari hiyo.
 
na ndio hasa ilikuwa maana yangu. Huyu mwenye IPPMEDIA ni mkongwe kwenye industry ya uhabarishaji. ajue kwamba waTZ wanao uwezo wa kuchambua na kutafakari (kuchanganya na zetu)
 
Back
Top Bottom