Nyumba iliyochomwa na FFU Mtwara

Nyumba iliyochomwa na FFU Mtwara

mbona wakuu hamzungumzii nyumba takribani &nbsp;20 za polisi waliojenga uraiani zilizochomwa moto baada ya kuporwa vitu vyote vya ndani siku ya tarehe 22 tuache unafiki<br>:
 
Yote kwa yote askali police either kwa maksudi au kwa umbumbumbu wao wameingia kunako mtego wa watawala bila kujua .Nasasa kwakuwa wanaajiri ajiri tu hata wezi kwani askar wa sasa hawana maadili
 
SERIKALI INAPOCHOMA NYUMBA ZA RAIA WAKE, KUBAKA WAKE KWA MABINTI, KUCHINJA VIJANA KWA WAJAWAZITO LINDI NA MTWARA SHAURI YA MAONI YAO WANANCHI SASA TUKIMBILIE WAPI

Jamani watazameni masiki wenzangu na mimi hawa kosa lao tu ni kule KUDIRIKI KUTOA MAONI YAO na sasa nyumba tu ya udongo unalazimika kuwatoka jumla hivi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sasa WaTanzania tunatarajia matokeo ya aina gani kwa hicho kitoto hapo pichani anayelazimika kulala kwenye baridi porini kwa kuwa tu CCM na Rais Kikwete wachoma nyumba yao,

Je, tunatarajia kitu gani tukija kukutana na yule binti pale akijiuza Mtaa wa Ohio Dar usiku kwa kuwa tu serikali yake imevuruga kabisa misingi ya pato la familia?

Je, WaTanzania tunalo jibu gani endapo huyo mama hapo juu atakaposhindwa maisha kijijini kwa kuwa tu maoni yao tu kwa mradi wa gesi utakua umemfanya mumewe atolewe roho na Nchimbi na kisha akajichagulia kuja jijiji kujaribu bahati yake katika Umachinga wa Mama Nitilie pembeni mwa barara pale Ilala Boma????????



25th May 2013 12:25 Woman-May25-2013.jpg

I had vehemently supported JK and sometimes admired his leardership style. I used to defend him personally in this forum. I never liked CCM in my life at all.
For the past six months i happen to distrust him and for these incidents happening in Mtwara, what is the difference between him and Assad? I live upcountry but think what this family posseses after 50 years of independent and think their future life after the incident!
It give senses for what they are fighting for!.
 
Ni wakati mwafaka kwa NEC-CHADEMA kutuma ujumbe wa walau watu saba (Makamanda Marando, Prof Safari, Chiku Abwao, Mawazo wa Bukoba, Zitto, Ben Saanane, Makamu Mwenyekiti wetu Zanzibar na John Mnyika) kwenda Lindi na Mtwara kutathmini hali ilivyo kwa wananchi wenzetu wa kusini kisha kurejesha ripoti Makao Makuu ili watu tujue tunaamua kuchukua hatua gani juu ya sakata la gesi once and for all.

Udhalilishwaji wa familia mbalimbali huko kusini ikiwemo hii familia tuliojulishwa na mpiga picha wa IPP Media ni ushahidi tosha kwamba tusipochukua hatua hizi za haraka basi kama chama tutakua tumewasaliti mno wenzetu hawa ambao hivi sasa ni WAHANGA WA MAONI juu ya mradi wa gesi ya Kikwete na Wa-China wake.
 
Ni wakati mwafaka kwa NEC-CHADEMA kutuma ujumbe wa walau watu saba (Makamanda Marando, Prof Safari, Chiku Abwao, Mawazo wa Bukoba, Zitto, Ben Saanane, Makamu Mwenyekiti wetu Zanzibar na John Mnyika) kwenda Lindi na Mtwara kutathmini hali ilivyo kwa wananchi wenzetu wa kusini kisha kurejesha ripoti Makao Makuu ili watu tujue tunaamua kuchukua hatua gani juu ya sakata la gesi once and for all.

Udhalilishwaji wa familia mbalimbali huko kusini ikiwemo hii familia tuliojulishwa na mpiga picha wa IPP Media ni ushahidi tosha kwamba tusipochukua hatua hizi za haraka basi kama chama tutakua tumewasaliti mno wenzetu hawa ambao hivi sasa ni WAHANGA WA MAONI juu ya mradi wa gesi ya Kikwete na Wa-China wake.

Mimi simo?!!!.. Na TAYADI!...
 
It gives me pleasure to note that a number of home and international rights bodies are already on the ground in their largest number ever to get a feel of the pinch, infringment of universal rights and the degree to which the state-managed attrocities on Southerners may have taken to the hour in terms of criminal acts like:

1) Deliberate torching of homestead and private property carried out by state mechineries,

2) Indiscriminate and most dehumanising sexual assaults going on in Mtwara,

3) The much feared cold-blood killings of disenting voices already branded as 'righleaders' down there.

4) State targeting of specific groups in Mtwara because of their political affiliation to CHADEMA, CUF and othe opposition parties,

5) ... etc


Swali lenye thamani ya zaidi ya dola milioni moja kwa kila mmoja kwa nafasi yake katika taifa letu ni:

Je pindi unaposikia ya kwamba serikali inayosadikiwa kuwekwa madarakani kwa manufaa ya wapiga kura inapogeuka adui na kuchoma nyumba za raia wake, kubaka wake kwa mabinti, kuchinja vijana kwa wajawazito kwa mizinga ya kijeshi Lindi na Mtwara shauri tu ya kutoa maoni yao, wananchi sasa tukimbilie wapi???????????
 
Hii nimeitoa IPPMEDIA:

A woman shows her house alleged to be burnt by Field Force police during the operation to calm the situation erupted after anti-gas transportation from Mtwara to Dar es Salaam clashed by riot police on Wednesday at Magomeni in Mtwara region. Situation in Mtwara is calm but remains tense.

View attachment 95077

Casuality of war
 
Wakuu 'FundiMchundo', 'Dingswayo', 'Mtwaraboy' pamoja na 'Gesi-Mtwara'; hebu tusaidieni basi picha ya yule MAMA MJAMZITO anayedaiwa kubakwa kwanza kisha kufiatuliwa rundo la mi-risasi tumboni pale Magomeni-Mtwara juzi - ni muhimu sana picha hii wakuu.
 
Wakuu 'FundiMchundo', 'Dingswayo', 'Mtwaraboy' pamoja na 'Gesi-Mtwara'; hebu tusaidieni basi picha ya yule MAMA MJAMZITO anayedaiwa kubakwa kwanza kisha kufiatuliwa rundo la mi-risasi tumboni pale Magomeni-Mtwara juzi - ni muhimu sana picha hii wakuu.

picha za Mwangosi Kijokisimba kazunguka nayo Dunia nzima kumchafua Jakaya, aliporudi nyumbani Kaingia Rais wa China na akahutubia Dunia kutokea Tanzania na sasa 1 st July Barack Hussein Obama anaingia kwa Jakaya kushuhudia maendeleo yasiyo mithilika!
 
Wananchi wakichoma nyumba, mahakama, magari, ofisi na kuharibu miundombinu mnashangilia tena kuhamasisha juu kuwa waendelee kuchoma. Ila ikisemwa polisi wamechoma mnawaandama polisi na kuwalaani kwa nguvu zote kana kwamba wakati nyumba inachomwa mlikuwa mnashuhudia na kuhakikisha kuwa kweli aliyechoma ni polisi.

Ingekuwa unajua wajibu wa polisi kwa jamii usingeandika huu upuuzi wako humu
 
Kuna watu wanatafuta...mahakama za kimataifa na watazipata tu..
 
Nilipokuwa mwela tulikuwa tunakosa nafasi ya kuyatumia mafunzo yetu
Siku hizi kila kukicha vijana wanatumia mafunzo vilivyo
Huu umbea wa kuweka picha ya nyumba iliyoungua na kusema imechomwa moto na ffu ni upumbavu tu
 
Wananchi wakichoma nyumba, mahakama, magari, ofisi na kuharibu miundombinu mnashangilia tena kuhamasisha juu kuwa waendelee kuchoma. Ila ikisemwa polisi wamechoma mnawaandama polisi na kuwalaani kwa nguvu zote kana kwamba wakati nyumba inachomwa mlikuwa mnashuhudia na kuhakikisha kuwa kweli aliyechoma ni polisi.

Kumbe ile sera ya jino kwa jino bado mnayo!?
 
Mkuu Songoro,

Hebu twende taratibu kidogo hapa;

Siku zote kwao wanafalsafa katika karakana zao aina ya zana ambazo watu hawa hujihifadhia huwa si lingine zaidi tu ya maneno na maana yake inayopatikana zaidi na kwa juu zaidi ya jinsi akili za kawaida zilivyozoea kwa neno husika.

Naam, ni kutokana na tabia hii ya wanasafa mbali mbali kama vile Socrates, Conficious, Mwalimu Nyerere na wengine chungu nzima duniani ndio maana wao hutajwa sana kama vile WATU WENYE MAHABA MAZITO NA KITU 'NENO' kwa kuwa ndio chombo pekee kwao kutendea kazi zao za kila mara.

Hapo chini kidogo naona umeweza kutumia baadhi ya 'FIKRA' na hata 'MANENO' mazito mazito ama kiajali au kwa kukusudia, katika kukuwezesha kuleta mezani hoja yako jukwaani. Sasa naona ni bora tukaenenda fungu kwa fungu katika kujiridhisha nini fikra na maneno hayo yatakua yamebeba kwetu sote na wala si kwako pekee.

Maneno nitakayozungumzia humu ni pamoja na hayo kwenye wino mwekundu uliokolea sana hapo chini:

1) Kijokisimba 'kazunguka' ...


= Hii ina maana unazungumzia pengine binadamu fulani mahala ila sina uhakika juu ya hilo maana kama ni kitu Jina basi nakuhakikishia ya kwamba nalisikia kwa mara ya kwanza kwako wewe hapa ila kote Tanzania hakuna jina kama hilo.

2) 'Kumchafua' ...


= kwa maana rahisi tu hilo neno hapo juu linatupa maana ile ya ama 'KUTIA UCHAFU', 'KUFANYA KUINGIA UCHAFU' au 'KUMSILIBIA MTU UCHAFU AMBAO HAKUA NAO TANGU MWANZO'.

Sasa kidogo inaleta shida kuelewa ulichoinuia kueleza hapa, pengine maana yako ni moja kati ya haya;

(i) kulikua na mtu fulani mbaya sana aliyejichukulia kazi ya kutangaza kuwa Daudi Mwangosi aliuawa wakati tariifa ulizonazo wewe ni kwamba jamaa ni buheri wa afya sana tu tena hapa hapa ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Kama kweli hilo ndilo ulilomaanisha na kweli mwendawazimu mwingine aliaanza tu kuzunguka dunia kuzungumzia kitu kilicho kinyume hicho unachotuaminisha humu basi mimi hapa niwe wa kwanza kukuomba radhi kwa niaba yake na kuungana na wewe katika kumkeme vikali kweli kweli humu.

3) Kutembelewa na Majina Mazito duniani kama vile jiPing na Obama...

= Hapa nako nakutana na jambo; safari hii wala si neno tena bali ni 'FIKRA' kwamba uzito wa ugeni katika nyumba yetu ama ina maana kwamba:

(i) Nyumba yetu ni sumaku sana kutembelewa na kila jina zito duniani hata kukitokea mtu 'KUCHAFULIWA' au hata kiukweli yeye awe kweli ni 'MCHAFU KIASILIA' lakini ugeni wa aina fulani haitojizua tu kuendelea kupiga hodi kwake.

(ii) Nako pia haujaweka wazi kwa katika ugeni tunaoendelea kuupata nchini ama kutoka Ughabuni huko au hata maeneo yetu haya haya ya Bara la Africa - yule ambaye amekua akitembelewa huwa 'NI MTU FULANI KWA JINA LAKE YEYE' au ugeni wa aina uliotaja huwa ni 'KWA JINA LA TAIFA LETU LA TANZANIA'?

(iii) Jambo lingine linalojitokeza ni kule kutafuta kutuweka katika mkondo wa kutaka kuaminisha ya kwamba 'UBORA WA VIONGOZI NA UONGOZI WAO KWETU HAPA NCHINI SIKU HIZI HUPIMWA NA AINA YA UGENI' unaojitokeza milangoni mwao. Kidogo hapo nako sina uhakika mpaka pale utakapotuweka wazi zaidi juu ya hilo.

(iv) Kwingineko katika ile orodha ndefu ya Haki za Msingi za Binadamu kote duniani (UN Human Rights Code) kidogo nilidiriki kutumia japo kamojawapo tu pale kwenye bandiko namba 33 humu ndipo Mkuu Songoro ukapata kutibuka, kuchefuka na hata kushindwa uvumilivu wowote juu ya 'HAKI YANGU NA YA WATANZANIA WOTE KUPATA TAARIFA SAHIHI TENA NDANI YA MUDA MWAFAKA'.

Hadi hapo kidogo mara baada ya kusoma hoja yako, licha ya kukupa heko na wewe KUTUMIA HAKI YAKO YA KUTOA MAONI hata pale nisipopendezwa za kile unachokisema, nilibaki nimeduwazwa kwamba pengine ki-undani ulikua unaonelea ya kwamba sisi wananchi:

(a) ama hatuna haja na taarifa juu ya nini kinachoendelea Mtwara kwa wananchi wenzetu isipokua wenye haki hiyo ni serikali pekee; au

(b) pengine wenzako tulipotoka mahala kuomba kufahamu MAZINGIRA YA KIFO CHA YULE MAMA MJAMZITO kule Mtwara lakini bila ya kuomba kwanza RUKSA mahala hivi?

Hadi hapo Mwenyekiti Buchanan, naomba kuketi ili nikampishe mjumbe mwenzetu 'Mkuu Songoro' naye sasa achukue kipaza sauti ili kuweka wazi jukwaa lako wazi hatua kwa hatua kwa kujibu hoja hizo hapo juu.

Asante Ndg Mwenyekiti.


picha za Mwangosi (1) Kijokisimba kazunguka nayo Dunia nzima (2) kumchafua Jakaya, aliporudi nyumbani Kaingia (3) Rais wa China na akahutubia Dunia kutokea Tanzania na sasa 1 st July Barack Hussein Obama anaingia kwa Jakaya kushuhudia maendeleo yasiyo mithilika!
 
Back
Top Bottom