YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,994
Kikwete alipomaliza digrii yake ya uchumi chuo kikuu cha Dar es salaam 1975 hakuwa na nyodo kama ambavyo baadhi ya wasomi wetu wakipata digrii hukataa kwenda kufanya kazi maeneo yenye shida.Kikwete alikwenda bila kinyongo akijua kuwa hata wale wa Singida ni wananchi wanaohitaji pia kuhudumiwa na mtu mwenye digrii.
Pamoja na usomi wake aliamua kukitumikia chama ambacho kilikuwa hakilipi maslahi mazuri kama mashirika ya umma.Uvumilivu wake ulisaidia baadaye zile dua za wanyonge kama hao wa singida kumwezesha kufika mbali
Miaka ile angeweza kataa akapata kazi nzuri tu kwenye makampuni kibao yaliyokuwa Dar es salaaam
Angalia nyumba aliyokuwa akiishi msomi kama yeye wa miaka ile haina maji wala umeme.Kuna kijana yeyote wa UKAWA hata leo hii na kadgrii kake koko aweza kukaa maeneo kama haya? Angepewa nyumba kama hii BAVICHA mwenye kadgrii koko Jamii Forums yote ingejaa matusi ya kutukana serikali hadi basi.
Nimeamini kweli mvumilivu hula mbivu.Vijana jifunzeni kwa Kikwete sio ukipata kadgrii unakuwa limbukeni mwezi wa kwanza tu wa ajira unataka kukaa kwenye ghorofa kama ni mwalimu wa shule ya msingi unajitia siwezi kaa nyumba ya udongo.Hiyo nyumba aliyokaa Kikwete akiwa na digrii ni ya udongo sembuse nyie wengine na vi-certificate?