Nyumba 84 zinatarajiwa kupigwa mnada, baada ya wakopaji wa mikopo benki kuzitumia kama dhamana na kushindwa kurejesha fedha

Walikua wanakopa halafu wanacheza na watumishi wa mabenki kufutiwa mikopo na madeni kama wamemaliza.
System imebadilika hayo mambo hayapo kwa sasa.

Pia mabenki husikiliza mteja ,unapokwama kibiashara unawasiliana nao kuwaeleza changamoto ulizonazo ,nao hu extend mkopo, na utatakiwa kupunguziwa kiwango cha marejesho,sasa kipi kigumu?,ziuzwe tu ,kama walikopa halafu wakajificha shauri yao
Bank zingefirisika wewe, umesoma hadi darasa la ngapi mkuu? Katika vitu ambavyo hata ukidanganya utaabika basi ni namba, pesa ni namba. Ukimkopesha mtu halafu jifanya karudisha ilihali hajarudisha, account haita badirika, itasoma -ve and then kama ni biashara itafirisika na kama ni duka kenji zitaanza kuonekana.
 
Yule mama aliyedai katapeliwa nyumba na nmb walishamrudishia? Naona rc happi alilivalia njuga
 
Dar watu wanakopa sana
Kwa mujibu wa tangazo lililotoka Jumanne ya wiki iliyopita kwenye moja ya magazeti ya wiki, nyumba hizo zitapigwa mnada kwa awamu tofauti kuanzia mwezi huu hadi Julai baada ya wahusika kushindwa kurejesha mikopo waliyochukua kwenye benki ya NMB.

Tangazo hilo ambalo lilitolewa na kampuni ya udalali ya Nsombo & Company (NC), limeainisha majina ya wadaiwa, mali ilipo na tarehe ya mnada utakapofanyika.

“Kwa idhini tuliyopewa na Benki ya NMB Makao Makuu tutauza nyumba za wadaiwa katika mikoa mbalimbali,” lilieleza tangazo hilo.

Pia tangazo hilo lilisema mnada huo utafanyika mahali zilizopo mali hizo kwa tarehe na muda kama ulivyoainishwa kwenye tangazo hilo kati ya Jumapili ya mwezi huu hadi Julai 13.

Tangazo hilo limeweka hadharani majina ya wakopaji hao na dhamana walizoziweka wakati wa ukopaji.

Katika kipindi cha mwaka jana kampuni mbalimbali za udalali kwa nyakati tofauti zilitangaza uuzaji wa nyumba za wakopaji kwenye benki tofauti ambao walishindwa kurejesha mikopo wanayodaiwa.

Mwezi Aprili Benki ya EFC ya jijini Dar es Salaam, ilitangaza mnada wa nyumba 43, viwanja na magari yaliyowekwa rehani na watu waliochukua mikopo kwenye benki hiyo na kushindwa kuirejesha.

Kwa mujibu wa matangazo yaliyochapishwa Aprili 20, mwaka huu kwenye magazeti mawili tofauti, mnada huo ulijumuisha mali hizo ambazo zilinunuliwa au kuwekwa dhamana kama mkopo kwa wananchi hao.

Benki hiyo ilitoa kazi ya kuendesha mnada huo kwa kampuni za udalali ambazo hata hivyo, zilipopigiwa simu ili kutoa ufafanuzi wa mnada utakavyoendeshwa, hazikuwa tayari kueleza.

Katika tangazo lililochapishwa kwenye moja ya magazeti hayo, lilionyesha wateja 24 walikopa fedha kati ya Sh. milioni 30 hadi milioni 343 na kuweka rehani hati za nyumba na kadi za magari.

Tangazo hilo lilibainisha kuwa nyumba hizo ziko maeneo ya Kunduchi, Mbweni, Ukonga, Manzese, Temeke, Mivumoni, Buza, Mbagala, Kiwalani na Segerea.

Katika tangazo lingine, jumla ya wadaiwa 19 wenye mikopo kati ya Sh. milioni 25 hadi 120, walioweka dhamana ya nyumba, zilitangazwa kuuzwa kwa mnada wa hadhara.

Novemba 2, kampuni ya udalali ilitangaza uuzaji wa nyumba 21 baada ya wahusika kushindwa kurejesha mikopo waliyochukua kwenye benki ya NBC.

Mwaka jana, Mwenyekiti wa Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Stanley Kevela, alisema wamekuwa wakiuza nyumba za wateja walioshindwa kulipa mikopo ya benki kadhaa, kukusanya madeni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

“Tuna kazi ya kukusanya madeni na kuuza nyumba za wateja walioshindwa kulipa mikopo benki zaidi ya 10, kama NBC, KCB, Barclays na CRDB. Tunauza nyumba Mwanza, Morogoro, Zanzibar na maeneo mengine.

Nyumba ya aliyewahi kuwa Waziri wa serikali ya awamu ya tatu na nne, Dk. Batilda Burian, iliwekwa sokoni baada ya kudaiwa kushindwa kurejesha mkopo anaodaiwa benki.

Nyumba hiyo ilikuwa ipigwe mnada Juni 9, mwaka jana, kwa niaba ya Benki ya Equity Tanzania baada ya Dk. Batilda aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kushindwa kulipa deni.

Lakini baadaye Kampuni ya udalali ya Magwembe iliyotangaza kuuza nyumba hiyo ilisema haikuuzwa kwa sababu mwenyewe amejitokeza na kuikomboa.

“Mmiliki aliongea na benki akalipa kiasi cha fedha na wakakubaliana kuongezewa muda zaidi wa kulipa deni ili nyumba hiyo isipigwe mnada kama tulivyokuwa tumepewa kazi na benki,” alisema ofisa mmoja wa kampuni ya udalali.

Juni mwaka jana, nyumba 85 na magari zaidi ya 10 ya wakopaji wa benki nne nchini, ziliwekwa katika mnada wa hadhara baada ya wakopaji kushindwa kurejesha mikopo waliochukua kwa dhamana ya mali hizo.

Kwa mujibu wa matangazo ya kampuni za udalali ndani ya siku 57 tangu Aprili 20, mwaka huu, na kampuni zilizopewa kazi ya kuendesha mnada kwa niaba ya benki hizo, wakopaji hao walipewa muda wa siku saba kulipa madeni yao vinginevyo mali zao zitauzwa kwa mnada wa hadhara.

Katika tangazo la Mei 23, mwaka jana nyumba 21 na magari sita yalitangazwa kupigwa mnada na nyumba nyingine 20 na magari manne zilitangazwa kwenye tangazo lingine.

Chanzo: IPP
 
Uchumi unakua kwa 7%
 
Kipindi kile hadi vijijni zilijengwa nyumba mpya na bati la 'Msouth' sasa hivi zinauzwa zilizojengwa
Itasaidia sana watu kuwa na nidhamu ya pesa, sio kukopa na kununua gari ya kutembelea badala ya kuwekeza kwenye viwanda vidogo na kulipa hilo deni kwa uzalishaji
 
Ikope biashara iuzwe nyumba ya kuishi ujinga huu tunautoaga wapi? Kama uliweza kujenga bila mkopo sasa unaiwekaje nyumba zamana ya mkopo?
 
Kuna jamaa yangu mkopo keshamaliza hati ya nyumba wamegoma kumrudishia wanasema ni mteja mzuri anarejesha kwa wakati wamkopeshe tena nayeye hataki
 
Awamu ya nne hakuna nyumba iliyowahi kupigwa mnada na benki, kwakweli uchumi umeyumba sana.

Hata dala dala watu wanarudisha magari kwa kukosa abiria.
Its not about uchumi! Unajua watu walikuwa wananunua na kujenga kwa hela gani. Hebu tafakari halafu urudi na evidence zako hapa!
 
Back
Top Bottom