Nyumba 6 zachomwa moto Kaunti ya Homa Bay kwa tuhuma za ushirikina

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,554
2,000
POLISI katika eneo la Ndhiwa, Kaunti ya Homa Bay walikuwa na wakati mgumu kutuliza wanakijiji waliochoma nyumba sita wakidai mwenyewe ni mchawi.

Wakazi wa kijiji cha Rachong’, Kata ya Kubuoch Magharibi, walimshambulia Mzee Gabriel Osaso, mwenye umri wa miaka 79, kwa madai kwamba alihusika katika kifo cha mwanafunzi wa Darasa la Kwanza mnamo Ijumaa.

Mzee Osaso alilaumiwa kuwa mchawi kwenye harakati za kutafuta mwili wa Veronicah Achieng’, aliyekuwa mwanafunzi katika Shule ya Msingi ya Ombo.

Mwanafunzi huyo anadaiwa kuuawa na mamba katika Mto Kuja.

Wanakijiji hao walisema mshukiwa alisikika akisema kwamba mwili wa marehemu haungepatikana baada yake kuufanyia mazingaombwe.

Chifu wa eneo hilo, Joseph Ogur alisema polisi walilazimika kumwokoa mzee huyo kutoka kwa umati huo ambao ulitaka kumdhuru.

Mnamo Jumapili, wanakijiji walichoma nyumba sita katika boma la mzee huyo na vitu vyote vilivyokuwa ndani.

Taifa Leo
 

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,375
2,000
Inaonekana Wakenya wamewekeza sana kwenye uchawi baada ya kuishiwa rasilimali kwenye nchi yao.
teh teh teh

Once a nyang'au, always a nyang'au.
 

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
10,783
2,000
Too sad,but wakenya mara nyingi uwa mnatuhumu TZ kwa ushirikina while huko kwenu umetamaraki!
Una uhakika? Navojua mimi utasikia cases za hapa na pale ila ushirikina huwa unakemewa sana Kenya na unaonekana kama ushamba wa hali ya juu. Nyie mpo kwenye level nyingine bana, kwanza viongozi wenu
ndio huwa mstari wa mbele. Eti utasikia bungeni bundi, ndege wa kawaida tu, anazua taharuki ya kufa mtu.
 

Mgagaa na Upwa

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
5,478
2,000
Una uhakika? Navojua mimi utasikia cases za hapa na pale ila ushirikina huwa unakemewa sana Kenya na unaonekana kama ushamba wa hali ya juu. Nyie mpo kwenye level nyingine bana, kwanza viongozi wenu
ndio huwa mstari wa mbele. Eti utasikia bungeni bundi, ndege wa kawaida tu, anazua taharuki ya kufa mtu.
hivi sio?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom