Nyuma ya pazia ya Operesheni Tokomeza

Nyuma ya pazia ya Operesheni Tokomeza

..... Endapo tume hiyo haitataja haya maovu niliyosimuliwa na mwanajeshi, nipo radhi kuvua nguo zangu zote na kutembea uchi mitaani. Ni bora kuwa chizi ili nisiendelee kuyaona haya maovu wanayotendewa raia wasiokuwa na hatia.
Ukifanya hivyo hautakuwa na tofauti na wale waliofanya unyama huo....kwani utakuwa hujasaidia lolote kuhakikisha waliofanya unyama huo wanaadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Nakushauri kusanya ushahidi wako wote uifadhi mahala salama tafuta namna ya kuhakikisha hiyo tume huru ya kiuchunguzi itakapoanza kazi unauwakilisha kwayo.
 
Yaani mleta mada mwenyewe hujaweza kuzitaja hizo dhuluma wakati unazijua.
 
Yaani mleta mada mwenyewe hujaweza kuzitaja hizo dhuluma wakati unazijua.

baadhi ya tuhuma tayari nimeishazitaja au unataka nitaje hata zile mbaya zaidi?
 
Kama shigo-ngo...

Ni kweli kabisa mkuu, tumezoea kusikia matukio ya kutisha kama haya kwenye hadithi za shigongo, lakini inasikitisha na inauma sana kusikia kwamba uovu huu umetendeka live katika ardhi ya Tanzania.
 
Ndugu yako ni mwanajeshi na yeye alikuwepo au alihusika kufanya unyama huo.

Ungemuuliza swali moja tu je alitumwa na waziri wa Maliasili Kagasheki au akili zao wao wenyewe?
 
Si utuambie tu kuwa waliamua kuhamishia ujangili toka kwa tembo kwenda kwa binadamu na sasa mmeacha kelele wameurudisha kwa tembo,kitaalam tunaita "re-allocation of ujangilitis" teh teh!
 
Kuna mambo mengi msiyoyajua kuhusu operesheni tokomeza. Leo nimekuwa nikiongea na kaka yangu, ambaye ni mmoja wa wanajeshi walioshiriki operesheni tokomeza, amenifumbua macho sana kuhusu unyama uliofanywa na wanajeshi kwa raia na mali zao, hasa mifugo. Kuna uovu mwingi na wa kutisha walioutenda ambao haujaripotiwa wala kuwewwa wazi na tume ya Lembeli kwa sababu ambazo hazijulikani kwa mtu yeyote mpaka sasa.

In fact, what has been revealed by Lembeli's inquiry commision is just a very small fraction of the tip of an iceberg. Ndugu zangu, maovu yaliyotendwa na wanajeshi hayasimuliki. Ngoja tusubiri tuone kama tume itakayoundwa kufanya uchunguzi wa kina itakuja na majawabu mapya kuhusu uovu wote uliotendeka. Endapo tume hiyo haitataja haya maovu niliyosimuliwa na mwanajeshi, nipo radhi kuvua nguo zangu zote na kutembea uchi mitaani. Ni bora kuwa chizi ili nisiendelee kuyaona haya maovu wanayotendewa raia wasiokuwa na hatia.

''...Ndugu zangu, maovu yaliyotendwa na wanajeshi hayasimuliki....''

Asante kwa taarifa kuwa hayasimuliki japokuwa kaka yako alikusimulia................
 
Yale unayo yatuhumu ndo hayo hayo unayoyafanya..
Kichwa cha habari kinasomeka tofauti na uliyosema.

Huyu jamaa amenichekesha sana.....Anasema hayasimuliki huku akidai kuwa kaka yake amemsimulia........
 
Mkuu,
Unachokisema ni sawa kwamba Majangili pia waliua wanajeshi ambao ni watanzania wenzetu wakiwa kazini, lakini labda nikuulize hivi;
Jangili kuua askari inaingia vipi mtu kuambiwa afanye mapenzi na mnyama? Inaingia vipi askari kumlazimisha baba kufanya mapenzi na mwanae? Je, hao watu waliounguzwa makalio ndiyo majangili?

Jamani hapana......... Tulipo siko!

Nashukuru kwa maelezo yako lakin naomba fahamu kuwa kila mtu akinyang'anywa kitu anachotumia na kupata faida lazima atasema yote kulinda mali zake.
Nakumbuka hii biashara inalipa sana na lazima wawalipe watu ili waseme ilifanyika vibaya na ikiwezekana hata isimamishwe ili wao wao wahusika waendelee kupata faida. Mimi kwa fikra zangu sidhani na siamini yanayosemwa juu ya uteswaji wa majangiri kuwa ni kweli ila ninachojua biashara hii ina watu wengi wakubwa wenye maslahi nayo! Hiv mfano aliyoko mbele akauliwa na wewe unatakiwa uendelee kupambana hiv utaendelea kwa kufurahi au nawe utakwazika? Lazima ujue kuwa kila upambanapo na adui hakuna kucheka na vita havina macho maana kama mpaka inafika hatua jangili anaua askari jua hiyo ni vita ya ujangili na wale wanaozuia ujangili
 
Hii ni TZ bwana,kila mtu anamamlaka juu ya mkulima na mfugaji, utasikia DC analazimisha mtu alime eka kadhaa utazani anamlishia mji wake, mbona wafanyakazi hawalazimishwi na DC kufanya kazi???
 
Back
Top Bottom