Tiba ya ugonjwa wa Pumu ya ngozi

mukeyamasaifake

New Member
Mar 12, 2024
4
1
Habari za muda wakuu!!!

Jmani naomba msaada kwa anaejua dawa ya kienyeji ya PUMU ya ngozi.

Mwanangu anasumbuliwa sana nahuu ugonjwa, nimeshampeleka MUHIMBILI, EKENYWA, REGENYCY na tukapewa dawa na mafuta ya kupaka ya EPIMAX JUNIOR. Anapona kwa muda ila baadae inaanza tena.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu.
 
1.
Tumia asali ya nyuki wadogo kumpakaa kutwa mara 2 hii ilimponya mwanangu.
2. kuna sabuni inaitwa potassium permanganate
Unakuwa unamwogesha nayo kwenye pharmacy nyingi inapatikana hii
Kila la kher mkuu
 
Pole sana Mkuu, mimi mke wangu anayo ya kwenye mikono nimehangaika naye mpaka nikachoka. Mwisho akaambiwa asiwe anashika maji kwa muda mrefu labda wakati anaoga tuu, hivyo hawezi kufua, kuosha vyombo wala kudeki. Aakifanya hivyo mikono inakuwa poa lakini akigusa maji kwa muda mrefu mikono inawasha na kutoa vipele vidogo vidogo na ngozi anakatika kwa sababu ya ukavu hivyo kufanya mikono iwe na vidonda vingi
 
Pole sana. Muhimu zingatia masharti uliyopewa na ma Dr. Kwani huo ni ugonjwa wa kurithi/generational.
Hakikisha anakuwa mkavu mwilini pia avae soksi za pure cotton
 
Habari za muda wakuu!!!

Jmani naomba msaada kwa anaejua dawa ya kienyeji ya PUMU ya ngozi.

Mwanangu anasumbuliwa sana nahuu ugonjwa, nimeshampeleka MUHIMBILI, EKENYWA, REGENYCY na tukapewa dawa na mafuta ya kupaka ya EPIMAX JUNIOR. Anapona kwa muda ila baadae inaanza tena.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu.

1. Epuka kumpa parachichi! Linaufanya unakuwa active sana!
2. Mie wanangu wawili wamekuwa wanatumia virgin coconut oil (mafuta ya nazi yanakamuliwa bila kuchemshwa). Haya yamesaidia sana kwenye kuilaza maana huwa haiishi!!
3. Mikoa ya kaskazini (hasa Moshi) wana dawa ya asili ilisaidia kuituliza sana kiasi ukiwaona huwezi jua kama wana hio tatizo.

Nitaiulizia, ikipatikana nitakupa namba zao DM kama unajali kuhusu dawa za asili lakini.
 
Pole kwa mtoto, kama unaweza kupata ndemwai tumia hiyo kumpaka na kumpa kunywa asubuhi na jioni apate kuondokwa na hayo maradhi,maana inatibu pumu aina zote
 
Back
Top Bottom