Nyuki kuingia ndani.

Nyuki kuingia ndani.

Libunda

Member
Joined
Sep 17, 2019
Posts
88
Reaction score
80
Wapendwa wiki mbili zilizopita,niliingiliwa na nyuki chumbani kwangu.Aisee sikuwahi ona nyuki wengi kiasi kile walikuwa wengi mno. Kwangu lilikuwa tukio la ajabu ambapo ndani sitting walikuwemo watoto lkn hawakuwang'ata hata mmoja. Nilishiia kuomba huku nikiomba ulinzi wake kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Wale nyuki waliingia kwenye kabati langu la nguo hata Sijui walipenyaje Hali ya kuwa nilifunga mlango wa kabati..Niliomba sana,sana na sana. Baada kusema Ameen nilinyanyuka nikafungua mlango wangu wa chumbani,Baada ya hapo nikaanza Tena kusali baadhi ya nyuki walianza kunizunguka lkn sikuacha kumuomba Mungu,na hawakuning'ata.

Baada ya hapo nikaenda Kwenye kabati na kumwambia Mungu, nafungua kabati hili kwa jina lako tukufu. Nikafungua..Nilichokiona juu ya kabati nyuki wametanda kote ni wengiiii Mungu Wangu yaan sijawahi ona nyuki namna Ile. Walikuwa wametulia tuli..Basi nikaacha kabati wazi,muda hiyo ni saa Saba mchana..Hawakutoka mpaka jioni..Lkn sikuwa na uoga Tena.

Sasa nauliza nyuki akiingia ndani Kuna ishara,ni kitu gani hicho wapendwa..
 
1. Je, Waliingia kupitia wapi? Dirishani au mlangoni?
2. Walitoka baada ya muda gani na walipitia wapi?
 
Wanasema nyuki kuingia ndani Ni bahati iliyo njema
 
1. Je, Waliingia kupitia wapi? Dirishani au mlangoni?
2. Walitoka baada ya muda gani na walipitia wapi?
Walipitia dirishani..Na usiku ulivyofika baadhi y majirani walikuja na kutuambia nyuki usiku hawaoni kwahy ni vyema tukawaua Ila asibakie ht mmoja..Niliingiwa na moyo wa Imani Baad ya kusema inabid wafe..Kwahy walipuliziwa sawa.
 
acha milango na madirisha wazi zima taa ndani washa za nje kisha tafuta majani yenye moshi mkali washa ndani

(hakikisha huwachomi ila moshi tu ndio utawafanya watoke nje wenyewe)

ni vizuri wakati huu ukihamishia familia jirani pia kwa mimi ambae nimewahi kuonana na hawa wadudu mara kadhaa ni kuwa hawapendi vurugu, ukitulia nao wanatulia.

kuhusu kufanya maombi si jambo baya lkn ningekushauri kutohusisha na mambo ya kishirikina ni kawaida nyuki kuhama hama na hasa kama sehemu walikuwapo wamesumbuliwa.

pia nyuki hupenda sehemu iliyojificha ndio maana wameingia kwa kabati hata wale wanaofuga ukiangalia mabanda yao yanakuwa na vitundu vidogo tu ambavyo ambavyo vinaruhusu kuingia na kutoka.

jioni njema na pole kwa usumbufu wa hao wadudu.
 
Mimi nilIkuwa nao ndani kabatini karibu kabisa na kitanda. Kwa kweli mambo yangu yalininyookea sana , ila tatizo nilikuwa nikienda kuchepuka nikirudi lazima nyuki mmoja aniume nikiwa nimelala kitandani. Kwa sababu ya ujana niliamua kuwalina asali na wakahamia. Miaka miwili iliyopita walikuja wakaingia kwenye tairi ya trekta dogo , niliacha kulitumia mpaka leo na la pili pia wameshaingia. Kwa kweli hera ya mboga na matumizi mengine napata na nyumbani kuna amani tele. Nakushauri ukae nao ila watoto wasizoee chumbani Utakuja kunishukuru baadae. Ila nyuki wanatabia ya kucheza nje ya mzinga kila mchana wala hilo lisikupe hofu. Ubarikiwe sana nyuki ni rafiki wa binadamu.
 
Nyuki wakikuingilia ndani unapaswa kufanya nini? Tuelimishane wakuu.

Pia kuwaua ulikuwa ni ukatili sana, nini kilipaswa kifanyike?
 
Labda walimfuata mtu ambae hayupo ndani wakatulia, piga sala tu watarudi kwa aliyewatuma.
 
kiasili ama kimila, kwetu nyuki walipokua wakiingia ndani, tulichukua maziwa fresh, kisha unayajaza mdomoni halafu unawapulizia na kuwaomba watoke nje...

ndani ya dakika 1 huoni nyuki.

kama huamini katika imani za kiafrika basi usikashifu...

kwetu ilisaidia sana zaidi hii ishu.

hata mifugo ilipokua ikipotea, tulifanya hivi na kuwaambia wazee. Unashangaa tu ghafla usiku wa manane mara paap mbuzi/kondoo hawa hapa. Hakuna fisi wala chui kugusa kitu

Back to Our roots
 
Wapendwa wiki mbili zilizopita,niliingiliwa na nyuki chumbani kwangu.Aisee sikuwah ona nyuki wengi kiasi kile walikuwa wengi mno..Kwangu lilikuwa tukio la ajabu ambapo ndani sitting walikuwemo watt lkn hawakuwang'ata ht mmoja..Nilishiia kuomba huku nikiomba ulinzi wake kutoka kwa Mwenyezi Mungu..Wale nyuki waliingia kwenye kabati langu la nguo ht Sijui walipenyaje Hali ya kuwa nilifunga mlango wa kabati..Niliomba sana,sana na sana..Baada kusema Ameen nilinyanyuka nikafungua mlango wangu wa chumbani,Baada ya hapo nikaanza Tena kusali baadhi ya nyuki walianza kunizunguka lkn sikuacha kumuomba Mungu,Na hawakuning'ata..Baada ya hapo nikaenda Kweny kabati na kumwambia Mungu,nafungua kabati hili kwa jina lako tukufu..Nikafungua..Nilichokiona juu ya kabati nyuki wametanda kote ni wengiiii Mungu Wang yaan sijawah ona nyuki namna Ile..Walikuwa wametulia tuli..Bhac nikaacha kabati wazi,muda hiyo ni saa Saba mchana..Hawakutoka mpk jioni..Lkn sikuwa na uoga Tena..Sasa nauliza nyuki akiingia ndani Kuna ishara,ni kitu gani hicho wapendwa..
Acha usanii wewe!!, Kwaiyo hapo sasa inaendea ujiite nabii, wakristo mna tabu!
 
huyo mr ndeka uliejipachika jina lake ni wako ama ulimuiba?
Kwan wew unafikiri hili jina ndo analo ndugu Yako TU huyo unayemfikiria au..Hata Sijui unazungumza nn..Haya majina ni ya ukoo na wako wengi Sasa cjui wew umemkariri nani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom