Nyota yako leo Juni 27/2025

Nyota yako leo Juni 27/2025

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
NYOTA YAKO LEO IJUMAA JUNI 27/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KI
IMG-20250627-WA0038(1).jpg
NYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Ili kukamilisha mipango yako ni lazima ukutane na mtu mmoja mkubwa akiwa yupo hapa au yupo mbali akusaidie kuondokana na yanayokusibu vinginevyo hakuna mafanikio katika jambo lolote.

•Mahusiano yako yatakuwa na utulivu na leo utasikilizwa zaidi na mwenzako jitahidi kutumia zaidi busara kuliko nguvu inaweza kukujengea kinyongo kibaya kwa mwenzako na ukashindwa kufanya mengine ya kimaendeleo kutokana na kinyongo chake.

★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Leo hata kama ukikubaliana na mtu yoyote jambo lolote ujue atakwambia usubiri kwanza au atakucheleweshea mahitaji yako kuwa na subira na tumia hekima utafanikiwa.

•Kazi zako zitaenda kwa uzito uzito na makelele lakini mwisho itakuwa vizuri na manufaa yataonekana.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Pamoja na kwamba leo itakuwa siku nzuri kwa kila jambo lako utakalolifanya unashauriwa kuwa usianzishe mambo mapya endeleza yale ya zamani na utafanikiwa tu.

•Safari zako ni nzuri ila usiwahi utapata maudhi maudhi lakini utafika salama.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Leo kuna uwezekano wa urafiki wako kuvurugika unashauriwa kuwa makini katika kuchagua marafiki wengine watakutaka wewe ili kupata kitu na sio marafiki wa kweli.

•Utapokea taarifa nzuri sana leo na mambo mazuri yatakutokea haja zako nyingi zitatimia na utafanikiwa.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Leo jaribu sana kuwa karibu na watu wa dini ili uweze kubarikiwa mambo yako Fanya ibada kwa mujibu wa imani yako na toa sadaka kwa watoto yatima maskini na wajane na utafanikiwa.

•Safari zako ni nzuri na zina kheri nyingi kwako moyo ukikataa kutoka ghairi panga siku nyingine na lolote unalolitilia shaka ni kweli lizingatie lina umuhimu kwako hata ukijikwaa usichukulie rahisi ipo maana yake.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Leo usipokuwa makini unaweza kupoteza vitu vya thamani kubwa kuwa makini katika mambo yako hasa nyie ambao mnaotumia usafiri wa umma katika kufanya safari zenu za hapa na pale.

•Mahusiano yako yapo vizuri ila mtu mpya uliyenae kwa sasa yupo kwako kimaana kimaslahi hana madhara ya nuksi kwako au matatizo dhidi yako ila usimuamini sana unaweza kulia msimu ambae yeye ndio anakucheka.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Leo jihadhari sana kujumuika na vikundi visivyofaa hasa nyakati za jioni kama una matatizo yanayokusumbua jaribu sana kuwasiliana na wataalamu ili wakusaidie kuondokana na matatizo hayo hata kupata ushauri.

•Safari zako ni nzito leo na utaona ugumu mwingi pia safari inaweza kufa hivyo ikiwezekana ghairi au chelewa zaidi kutoka.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Leo inaonekanakana kuwa mambo yako yapo hatarini kuharibiwa na watu wengine hasa wale ambao wako katika serikali au katika dini Unatakiwa kuwa mpole kuwa muda huu ili kupisha dhahama hiyo iondoke.

•Mahusiano yako yataingia doa mpaka utatamani yasiwepo tu yaishe ili uishi kwa amani zaidi hii inatokana na uadui wa nje unaoonekana kufuatilia zaidi maisha yako ndio unaamua kupitia humo.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo jaribu kuwa muangalifu na mtu yoyote ambaye utashirikiana nae katika jambo lolote wengine watataka kukuingiza katika mambo ambayo yatakuletea balaa kubwa na hasara kuwa makini sana.

•Maradhi madogo madogo ya hapa na pale yatakusumbua na yanaputa usipate khofu.

Safari zako leo sio nzuri tulia nyumbani.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Tumia muda huu kukamilisha mambo yako uliyokuwa umepanga kuyafanya Fanya safari kutana na wadau wa biashara zako na tekeleza wajibu wako kazini Mambo mazuri yanakuja.

•Mahusiano yako yamejaa giza kwa sasa na usijihusishe na mahusiano yasiyoeleweka au yanayotumia nguvu zako kubwa yatakuletea athari mbaya mwilini.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Leo ni siku mbaya kwako kuna uwezekano wa wewe kupata balaa katika mambo yako jaribu sana kuwa muangalifu katika kila jambo ambalo umepanaga kulifanya au la si hivyo unaweza kuharibikiwa pakubwa.

•Utapokea habari mbaya leo aidha ya msiba wa mtu unayemfahamu au maarufu au mambo ya kutisha au kuona tukio baya la huzuni stahmili ni mambo ya kawaida na yanapita tu.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Leo jitahidi kukutana na wakubwa zako wakusaidie kukupa ushauri bila hivyo itakuwa vigumu kwako kutatua matatizo yako yanayokukabili hasa yale yanayohusiana na mapenzi na ndoa.

•Kazi zako zitaenda kwa uzito sana na ili zifanikiwe lazima utumie nguvu kuhakikisha kufanikiwa kwake.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
 
Leo niliwaza kutoka nyumbani nipite kwenye vitongoji vyote kuwaeleza nautaka udiwani sasa hapo kaka mchawi kwenye nyota yangu umesema nitulie nyumbani basi wacha nifanye hivyo .

Aisee niandalie kombora la kutisha niwatishe wajinga wote watakaochukua fomu ya udiwani katani kwangu maana rasmi nautaka udiwani mkuu dogoli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom