Nyota ya Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salimu Mwalimu yang'ara

ILA msimuharibu, kwa kumpa sifa zisizo sake pekee. Mkutano huo alikuwa na wenzake. Walitumiza lengo Hilo wote. Bila CHADEMA, Mwalimu si kitu. Tunamuhitaji sana sana, lakini msimuharibu kwa sifa za ziada.
 
CHADEMA ina vijana wenye UWEZO (ki-fikra na kimaono) ambao wanaweza kuisaidia jamii tofauti na wale wa upande wa pili ambao wao ni wachekeshaji wa wafalme.
Kikubwa tunahitaji mikakati ya kisasa na mbinu za kisasa katika kushinda uchaguzi. Uchaguzi wa serikali za mitaa utatoa picha kamili.
 
Tatizo la CDM ni moja nalo ni ukabila na uanaharakati. Huyo bwana mdogo sasa hivi atapukutika. Kwa sababu wenzie ni biashara na ulaji tu.
 
Kifaa kipya cha UKAWA hicho; Go go go Salum Mwalimu; mabadiliko ya kweli; ufanisi wa ku-delete majizi ya CCM; yanahitaji vijana kama wewe; keep it up
 
Yap,dogo yupo njema sana,salute kwa viongozi wa chadema kwa kuwa na mpango mahususi wa kupika vijana kimya kimya na wanapoiva wanaingia frontline..."Wanasiasa wazuri huandaliwa...."By Freeman Mbowe,ni kwenye mazishi ya Regia Mtema....."...Naomba nitoe siri kwa leo,chadema tulikuwa tuna mwandaa kuja kuwa mwanasiasa,na tulikuwa tumesha mwandalia na jimbo,nalo ni Shinyanga mjini..."By Zitto Kabwe,ni kwenye mazishi ya Steven Kanumba.
 
SALUM Mwalimu, si jina geni kwa Watanzania wengi wanaofuatilia matukio yanayotokea hapa nchini na nje ya nchi mara kwa mara.

Jina hili ni la mwanahabari aliyejizolea umaarufu mkubwa akiwa katika kituo cha Luninga cha Chanel Ten, ambaye sasa anafanya kazi kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom ambako nako umahiri na uwezo wake wa kazi umemfanya kuwa na mchango katika kampuni hiyo.
Jina hili siku chache zilizopita limepata mvumo wa tofauti na ilivyozoleka baada kutangazwa kuwa miongoni mwa wanaowania ujumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema kutoka Zanzibar.
Tanzania Daima Jumatano, lilifanya mahojiano na Mwalim, kujua kilichomvutia Chadema na kuamua kuwania nafasi hiyo kubwa.
Mwalimu anasema alianza kuipenda Chadema mwaka 1998 wakati akisoma shule ya Sekondari ya Umbwe, wakati huo akiwa mwanafunzi mwenye kupenda kufuatilia siasa kupitia vyombo vya habari na wakati mwingine kupata nafasi ya kuhudhuria mikutano ya hadhara ya chama hicho.
"Nilipenda siasa tangu nilipokuwa shule na nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa mambo ya siasa,wakati huo nakumbuka pale Moshi Chadema ilikuwa ikivuma chini ya Mzee Ndesamburo na Mama Maulida Komu"
Anasema alivutiwa zaidi na chama hicho baada ya kuona vijana akiwemo Freeman Mbowe( akiwa mwenyekiti wa vijana na baadae mwenyekiti wa taifa ) wakipatiwa fursa ya kuongoza idara mbalimbali pamoja na kushiriki kikamilifu kwenye mikutano ya hadhara huku wakionesha uwezo mkubwa wa kisiasa na kukifanya chama hicho kupiga hatua kubwa.
Anaongeza alizidi kuvutiwa na siasa za Chadema pale baada ya kuona mwaka 1995 na 2000 wakiunga mkono wagombea urais kwa tiketi ya Chama cha NCCR – Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF) profesa Ibrahimu Lipumba.
Anasema anakumbuka mwaka 1995, chama hicho kilimuunga mkono mgombea wa NCCR-Mageuzi, Agustine Mrema, katika nafasi ya urais.
Anasema matukio hayo mawili yalimuonesha jinsi chama hicho kilivyo makini na kischokurupuka kwa lengo tu la kujipatia umaarufu bali kinaamini katika kujipanga na kufanya maamuzi yasiyoyakubahatisha.
Mwalimu anasema Mwaka 2005, Chadema kiliamua kumsimamisha Freeman Mbowe, katika nafasi ya urais ambapo alipata kura zisizopungua 600,000 na wabunge watano wa majimbo na sita wa viti maalum.
Anasema mwaka 2010 Dk. Willibrod Slaa, aliwania nafasi hiyo na kupata kura zaidi ya milioni mbili huku Chadema ikipata wabunge 23 wa majimbo na 24 viti maalum.
"Kimsingi Chadema inafanya mambo kwa umakini mkubwa zaidi ukiangalia machapisho yao, matamko, na kinavyokua siku hadi siku unaona ni kimbilio la wanyonge" anasema.
Anasema ameamua kuwania ujumbe wa CC, Zanzibar kwasababu anataka kukiimarisha chama hicho visiwani humo.
Mwalimu anasema kuimarika kwa Chadema Zanzibar, hakuna lengo la kuibomoa CUF bali ni kuongeza nguvu ya upinzani katika kupambana na CCM.
Mwalimu anasema umefika wakati kwa kampuni mbalimbali kutoa fursa kwa vijana kushiriki kwenye siasa ili taifa liweze kupata viongozi imara zaidi kwa wakati muafaka wakati akili na nguvu zao zikiwa zinachemka.
"Mfano mimi nafanya kazi Vodacom,lakini bado nina mapenzi na siasa nikiwa na shauku ya kulitumikia taifa langu, ninachokiangalia ni kulinda masilahi ya mwajiri wangu ikiwemo kuangalia nisitumie muda wangu wa kazi kwa mambo yangu ya siasa".
Anasema na kuongeza "Vijana wengi wanapenda na kutamani kuingia katika siasa.
Lakini changamoto kubwa imekuwa ni woga wa kulinda ajira zao, kama tutakuwa na mifumo imara yenye kuwawezesha vijana wanaopenda siasa kufanya hivyo pasi na kuleta madhara katika ajira zao na mashirika yakaelewa hivyo hakuna shaka kwamba taifa litapata vijana wengi wa fani mbalimbali katika kulitumikia taifa lao jambo ambalo naamini linawezekana."
Mwalimu anasema anajisikia bahati kufanya kazi Vodacom na kuanza safari yake ya kisiasa akitokea Vodacom kwani ni shirika ambalo anahisi linajali vipaji na uwezo wa wafanyakazi wake katika fani zao nje ya kazi.
Anasema wapo baadhi ya wanasiasa akiwemo William Ngeleja, Angela Kairuki ambao walikuwa watumishi wa Vodacom hadi pale walipopata ubunge na kuamua kuacha kazi kwa kutambua kuwa kazi ya ubunge ingewachukulia muda mwingi na wasingeweza kutumikia ajira hizo mbili kwa wakati mmoja.nae anaamini kuwa atapitia njia hiyo ya mafanikio.
Anasema uamuzi wa kuingia siasani hakuyakurupikia, imemchukua muda mwingi kujitathmini na kujipima na sasa anajiona kuwa anatosha kuwa kiongozi wa kisiasa wa kitaifa.
"Sio uamuzi mwepesi, wapo walionipongeza na kunitia moyo wa ujasiri na wapo ambao wamekuwa wana wasiwasi na uamuzi wangu huu na hasa kuhusu ajira yangu na maisha yangu ya baadae"
"mimi naamini kila alifanyalo binadamu tena kwa nia njema lina baraka za Mungu, kikubwa ninachokiomba kwa sasa ni Mungu kunijaalia nguvu, afya njema, hekima na busara za kuitumikia siasa kwa masilahi ya taifa langu."
Matukio kadhaa anayoayakumbuka ndani ya Chadema ni siku Mbowewakati huo akiwa mgombea Urais alipotumia kwa mara ya kwanza Helikopta (Chopa) kwa ajili ya kampeni zake.
"Nakumbuka hakuna aliyekuwa anaamini kwamba kweli Mbowe, angetumia usafiri huo kumalizia kampeni zake mwaka huo 2005, nakumbuka tukiwa Kamachumu, Muleba majira ya saa nne usiku hivi Mbowe aliongea na msafara mzima wa kampeni zake tukiwemo waandishi wa habari na kutuambia kuwa operesheni Chopa inaanza kesho na kuniteua mimi kuambatana nae katika usafiri huo, ilinichukua muda kuamini kile alichokuwa akitueleza."
"Siku iliyofuata ni kweli Chopa ilifika Kamachumu na Mimi na Mbowe tukaingia kwenye usafiri huo tukiongozwa na kepteni Denge, ilikuwa ni hatari kidogo lakini iliyochanganyika na furaha kwani wakati Mbowe akiweka rekodi ya kuwa mwanasiasa wa kwanza kutumia Helikopta kufanya kampeni za Urais na mimi (Mwalim) nikaweka rekodi ya kuwa Mwanahabari wa kwanza kuripoti mkutano wa kampeni kwa Chopa."
Mwalim analitaja tukio la pili analolikumbuka kuwa ni siku Chadema ilipozaliwa upya katika ukumbi wa PTA viwanja vya maonesho Sabasaba hiyo ikiwa mwaka 2006.
Lilikuwa ni tukio la kipekee ambalo nililishuhudia kwa macho yangu chama kikitoka kwenye rangi ya buluu bahari na kuanza kutumia rangi tatu yaani nyekundu,buluu na nyeupe.
Ni tukio lililomsisimua kila mmoja ukumbini. Anasema alipata bahati ya kushiriki kutoa maoni yake juu ya mabadiliko hayo makubwa ya chama ikiwemo bendera na kadi mpya za chama wiki kadhaa kabla ya uzinduzi, na hivyo kutoa maoni yake jambo ambalo anasema ilikuwa la heshima kubwa kwake.
Historia yake
Salum alizaliwa Novemba 24, 1979 katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja iliyopo Mjini Magharibi, Zanzibar.
Alipata elimu ya msingi katika skuli ya Mkunazini(zanzibar) na shule ya msingi Mlimwa (Dodoma) ambako ndiko nilipomalizia mwaka 1995.
Alianza kidato cha kwanza shule ya sekondari Dodoma (1996) mwaka huo huo akahamia shule ya sekondari Umbwe iliyopo Kibosho mkoa wa Kilimanjaro ambako nako alihama na kuhamia shule ya sekondari kibaha iliyoko kibaha mkoa wa Pwani mwaka 1998.
Mwaka 1999 alihitimu kidato cha nne. Akapata elimu ya sekondari ya juu katika shule ya sekondari Shycom iliyoko Shinyanga ambako alisomea masomo ya uchumi, biashara na uhasibu (2000-2002).
Alipata mafunzo ya uandishi wa habari na utangazaji ngazi ya cheti katika chuo cha uandishi wa habari Tanzania – TSJ (sasa ni shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma ya chuo kikuu cha dar es salaam SJMC – UDSM) hiyo ilikuwa mwaka 2002-2003.
Alijiunga na Chuo cha Usimamizi wa fedha ( IFM) kati ya mwaka 2004-2007 na kuhitimu Advance Diploma katika fani ya teknolojia ya habari (IT), kati ya mwaka 2008-2010 nilijiunga na SJMCUDSM kwa ajili ya masomo ya Postgraduate Diploma ya mawasiliano kwa umma na kati ya mwaka 2010-2012 nilipata elimu yangu ya shahada ya uzamili ya biashara za kimataifa (MBA-IB) katika chuo kikuu cha biashara cha India.
Ni mwanahabari na mtangazaji amefanya kazi katika kituo cha televisheni cha Channel Ten, kuanzia mwaka 2003 mwaka 201, alipojiunga na kampuni ya Vodacom katika nafasi ya Meneja Mawasiliano na baadae Meneja Uhusiano wa Nje.
Amekuwa Chadema kwa muda mrefu ameshiriki opresehni mbalimbali za chadema ikiwemo opresheni zote za chama kati ya mwaka 2005-2010 ikiwemo chaguzi ndogo, opereshini sangara, operesheni M4C, operesheni rasilimali, ziara za viongozi wa kitaifa, ziara ya mshikamano ya wenyeviti wa chadema, Nccr- Mageuzi na CUF.
Nimeshirki katika kuandaa vipindi mbalimbali vya televisheni vya chama. Amekuwa katika kikosi cha waandishi wa habari wa mgombea urais wa Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2005 na 2010. kati ya mwaka 2006 hadi sasa amekuwa mmoja wa washauri wa chama wa masuala ya habari makao makuu na mshirika wa mipango na mikakati ya kihabari ya chama makao makuu kwa lengo la kukieneza chama.











 
Badala ya kuchochea ufuasi wa mtu mmoja mmoja kma yeye, mbowe ameweza kuwabuavijana wengi wenye uwezo mkubwa wa kukijenga chama na kukipatia ufuasi wa kitaasisi


Umenena vizuri, Tunajenga taasisi wala siyo mtu.
Hayo wanafanya ccm, chadema hakuna aliye juu yake kama ccm na kingunge kaka.
Ukiboronga unabwaga haraka sana halafu wanapatikana wengine wanakufunika.
Waulize akina shonza
 
Kwa hiyo huyu Mwalim amepewa cheo kwa sababu ni mzanzibar na wala sio.kwa sababu ya uwezo wake wa uongozi? Kabla ya kuwa naibu katibu mkuu alikuwa nani kwenye chama?

Mkuu sometimes si vizuri kuongea kama huna facts on the ground, Mwalimu alikuwa groomed CDM muda mrefu sana toka akiwa channel 10, hata mwaka 2005 ni mmoja wa wana habari waliozunguka sana na kampeni za CDM, alikuwepo kwa kazi maalum, so usiende spidi tafuta kadi yake ya uanachama uangalie alikuwepo toka lini na kimkakati kafanya nini, he who alleges must prove.
 
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salmu Mwalimu amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa wapya wanao kubarika kwa haraka tena sana.

Kifupi anapendwa, sijui ana bahati ya kupendwa au chama chake. Lakini kila mkutano anaofanya watu wamekuwa wakimiminika sana na kupelekea kuvunja record ya Mwanasiasa kijana aliyewaingiza wanachama wapya wengi ndani ya chama cha siasa nchini, kupitia mkutano mmoja.

Tazama picha foleni ya watu wakinunua kadi za chama ili wawe wanachama.



View attachment 205191View attachment 205189



Hongera sana kaka tuna kufahamu tangu IFM, MUNGU Akuepushe na mabaya
 
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salmu Mwalimu amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa wapya wanao kubarika kwa haraka tena sana.

Kifupi anapendwa, sijui ana bahati ya kupendwa au chama chake. Lakini kila mkutano anaofanya watu wamekuwa wakimiminika sana na kupelekea kuvunja record ya Mwanasiasa kijana aliyewaingiza wanachama wapya wengi ndani ya chama cha siasa nchini, kupitia mkutano mmoja.

Tazama picha foleni ya watu wakinunua kadi za chama ili wawe wanachama.


View attachment 205191View attachment 205189

TULIANZA NA MUNGU , tUTAMALIZA NA MUNGU .
 
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salmu Mwalimu amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa wapya wanao kubarika kwa haraka tena sana.

Kifupi anapendwa, sijui ana bahati ya kupendwa au chama chake. Lakini kila mkutano anaofanya watu wamekuwa wakimiminika sana na kupelekea kuvunja record ya Mwanasiasa kijana aliyewaingiza wanachama wapya wengi ndani ya chama cha siasa nchini, kupitia mkutano mmoja.

Tazama picha foleni ya watu wakinunua kadi za chama ili wawe wanachama.


View attachment 205191View attachment 205189

Hizo siyo sura za Wazanzibari kabisa, hao wote ni wahamiaji al maaruf "machogo" huko Unguja.
 
Back
Top Bottom