Mkiliman
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 984
- 345
Kikao cha Bunge la Bajeti kikiwa kinaendelea siyo siri tena, mbunge anazungumzwa sana nje ya bunge maeneo yote ya viunga vya bunge mjini Dodoma na mitaani, pia katika vyombo vya habari ni jina la MWIGULU, ni shupavu, mwerevu, jasiri aliye na weredi wa kupangua hoja za wapinzania pasipo kupepesa macho.
Mwigulu ni hazina ya CCM na taifa la Tanzania kwa ujumla na yuko tayari kutetea maslahi ya nchi pasipo kuangalia udini wala ukabila. Mwigulu amekuwa ni mwiba mkali wa wabunge wa upinzania ambao walizoea kutoa kejeli kwa CCM na serikali yake; JIBU limepatikana dawa ya CDM ndani ya BUNGE ni MWIGULU. Hoja zake zimekuwa ni kufungua kaburi la kuizika CDM! Hongera Mwigulu Usirudi nyuma, tunakupongeza, Unaandaliwa mapokezi makubwa kuanzia MANYONI hadi Iramba kutokana na hoja zako zilizogeuka mwiba kwa CHADEMA
Akili zako ni sawa na bomba la maji machafu yanayotoka chooni, mfano wa bomba la kutoka Muhimbili Hospital.
Unatia aibu kuonyesha upumbavu wako hadharani. Unafikiri matusi au kejeli zake zinasaidia ujenzi wa taifa bora la watu wenye elimu, afya, kipato na ushindani bora?
Inaniwia vigumu sana kusadiki kiasi kikubwa cha umbumbu na uhanisi wa fikra na imani yako juu ya maneno na/ au kejeli azitoazo Mwigulu Nchemba dhidi ya wana wa nchi wenzako.
Ushauri wangu ni kuwa ni heri ya kutafakari njia za kuweka na kurejesha misingi bora ya taifa letu, badala ya kuleta mawazo finyu na hanisi kwa maslahi ya watu wachache.
INAKERA KUONA UPUMBAVU UNATAMALAKI BADALA YA UKWELI NA MAENDELEO.