Nyongeza: Chaguzi zetu ni sambamba, siyo moja

Nyongeza: Chaguzi zetu ni sambamba, siyo moja

Kwa upande mwingine, tukubali maelezo ya UKAWA kwamba uvurugwaji wa Zanzibar umeathiri uchaguzi mzima! Lakini pia ni ukweli kwamba, linapokuja suala la uchaguzi wa JMT, ZEC wanakuwa ni kama wakala wa NEC kwa upande wa Zanzibar! Na ikiwa NEC anakuwa kama wakala huku akisimamia uchaguzi huo kwa kutumia sheria za NEC badala ya zile za NEC; kwa maana nyingine hapo Zanzibar inakuwa ni sawa na moja ya mikoa ya NEC inayopaswa kuendesha chaguzi zake strictly kwa kuangalia sheria za NEC and not otherwise.

Now the question is: Endapo uchaguzi ungeharibika mkoa mzima wa Mwanza ambao ni mkubwa kieneo na hata idadi ya watu ukilinganisha na Zanzibar! Je, matokeo yote ya Jamhuri ya Muungano yangefutwa kwa sababu tu matokeo ya Mwanza yamevurugika au yangefutwa ya Mwanza pekee? Kwenye uchaguzi wa 1995, Dar es salaam mambo yalienda mrama na kutokana na hilo ukarudiwa upya! Kwanini haukufutwa wa Tanzania mzima?

Ni kwanini kuharibika uchaguzi wa Zanzibar ndiko kuonekane kunapaswa kufutwa uchaguzi mzima wakati inapotokea sehemu zingine umeharibika; unarudiwa wa sehemu husika peke yake?

But in addition, hakuna kifungu chochote cha katiba kinachosema uhalali wa rais utakuwa pale tu kura zitahisisha pande mbili za muungano. Ibara ya 41 (6) Inasema: "Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote." Kwahiyo, hata kama itaonekana kura za Zanzibar zimeharibu, si tu kwamba kama ni kurudiwa inastahili urudiwe Zanzibar bali pia ikiwa majumuhisho yanaonesha kura za Zanzibar hazitaweza kuathiri matokeo ya urais wa Jamhuri (baada ya kuondoa zile za Znz) basi NEC inaweza kumtangaza. Hata hivyo, kwa kuwa tayari itakuwa kuna uchaguzi unapaswa kurudiwa sawa na ambavyo matokeo ya ubunge yasivyoweza kutangazwa ili kusubiri vituo vingine basi hapa napo, utangazwaji wa mshindi wa rais unaweza kusimamishwa kusubiria matokeo ya Zanzibar just for formalities. Ibara ya 42 (1) inasema:

42.-(1) "Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla ya kupita siku saba." Kwahiyo, labda NEC wasimtangaze mshindi mapema wakati tunasubiria matokeo ya Zanzibar! So, nini kifanyike wakati tunasubiria uchaguzi wa Zanzibar? Ibara ya 41 (3a) inaendelea: "Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula kiapo cha Rais."

Hadi sasa aliyechaguliwa kuwa Rais ni JK; kwahiyo ni kwamba aendelee kula kuku Ikulu wakati tunasubiria kura za Zanzibar zitengeneze majumuisho na hizi za bara lakini kung'ang'ania eti uchaguzi wote ufutwe kwa kigezo cha kuharibika uchaguzi wa Zanzibar ni kutaka kutafuta ushindi wa mezani!
Hapa unagoma kutambua kuwa mwanza sio sehemu ya muungano kama ilivyo zanzibar.

Unagoma kutambua kuwa mwanza haina katiba yake wala tume yake ya uchaguzi.Ni NEC ndo inahusika ambayo ndo hiyohiyo inahusika zanzibar juoitia mawakala ZEC.

Mfano wako wa mwanza unajaribu kuelewa kuwa hata ZEC basi wangefuta uchaguzi wa Pemba tu kwakuwa ndipo imegundua kuna dosari nyingi.Hapa ni kama unakubali kuwa dosari za ndani ya tume yenyewe wakati wa kutoa matokeo haziathiri uhalali wa kura kama zingekuwa halali.Kwahiyo msingi mkubwa wa kufutwa kwa uchaguzi ni dosari wakati wa kuoiga kura.Ingekuwa ni tume tu ndo kikwazo basi mwenyekiti wa tume angejiuzulu na raisi angeivunja tume bila kuathiri zoezi zima la upigaji kura.Yangefutwa matokeo yaliyotangazwa na tume iliyovunjwa.Tume mpya ingeendelea kutoa matokeo upya.

Moja ya dosari iliyotajwa na mwenyekiti ni idadi ya wapiga kura kuzidi daftari la wapiga kura.NEC ina daftari tofauti na ZEC huko Zanzibat au ni lilelile?
Kama ni hilohilo kwa nini NEC iendelee kuliona ni halali wakati ZEC ambao ni mawakala wao wamelioja haliwexi kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki?

Ni kweli ZEC haina mamlaka ya kufuta uchaguzi wa jamhuri ya muungano na wala hilo sio dai la wapenda demokrasia.Madai ni kwa nini NEC isifute uchaguzi wa jamhuri ya muungano kutokana na wakala wake ZEC kuonyesha kuwa haukuwa huru na haki huko kwenye eneo lake ikizingatiwa ni ZEC ndiyo wameendesha zoezi la uchaguzi wa raisi na wabunge wa muungano huko zanzibar?
 
Mungu ninayeini hutenda haki atashughilikia wanafiki kama ww mwanakijiji ww ni wa kutetea uhuni huu leo?!
 
Last edited by a moderator:
Eti chaguzi ni sambaba, lakini vyombo vinavyoendesha hizo chaguzi ni tofauti.

Hapo hapo, chombo kimoja kinaainisha dosari zilizopelekea kubatilishwa kwa matokeo/ uchaguzi wake lakini chombo kingine hakibatilishi matokeo ingawa wapiga kura ndo walewale.

Au ZEC walikuwa na wapiga kura wao na NEC nao walikuwa wa kwao na wa ZEC hawakupiga kura za NEC na wa NEC hawakupiga kura za ZEC?

Hahahahaa daaah.


ZEC ndiyo NEC kule Zanzibar!!!

ZEC ni wakala kikatiba wa NEC kule Zanzibar so NEC ya bara haipo Zenji isipokua ZEC ndo wanatenda kwa niaba ya NEC!!

Kwahiyo yote yaliyotokea yameratibiwa na ZEC na matokeo ya kura ZEC ndiyo inachakata then inatuma NEC bara!!!

Sasa huyu mkaanga sumu sijui anampotosha nani!!!
 
Cool Runnings, mbona unasema nilichosema. Siyo suala la SEif wala Lowassa hapa. Na definitely siyo suala la kina January wala kina sisi; ni suala la mahakama kwa sababu hapa kuna issue za kisheria na kwa ndani kabisa - kwa Zanzibar wenyewe - kuna suala la Kikatiba. Ila nikuhakikishie wakienda kwenye Mahakama Kuu yetu hili hata halitaenda mbali kwa sababu utengano wa chaguzi hizi mbili uko wazi mno. I stand to be corrected.
Mpaka sasa Watanzania wengi hatuna imani na mahakama?hizi mahakama ni za Ki CCM tu!!!!Dawa nzuri hapa ni rasimu ya Warioba tu
 
Mwanakijiji Du, i see yaani mzee mwenzangu umefikia hivi kweli. Invisible siku mkirudisha kitufe cha "like", mrejeshe na cha "unlike".

Usiseme tu hivi ndugu yangu; jenga hoja niulize nikiwa sina jibu la kukuridhisha nitakuambia. Watu wanavyonishangaa mimi na mimi nawashangaa wao kwanini hawaoni ninavyoona mimi.
 
Yawezekana gap alilopigwa Edo huku bara ni kubwa mno hivyo hata kama angechukua kura zote za Zanzibar bado asingemshinda Magufuli so NEC haioni umuhimu wa kuzisubiria kura za marudio za Zenji ambazo hata zikirudiwa haziathiri chochote kwenye hii jumlaa kuu ya bara.Kwani Zanzibar yote inawapiga kura wangapi?Lakini ukitumia common sense ni kwamba kuchanganya matokeo batili ya Zanzibar na haya ya huku bara utapata jumla kuu ambayo ni batili so kura zote zinakuwa batili.Unapochanganya kitimoto na nyama ya mbuzi na kuzipika kwa pamoja kwenye sufuria moja maana yake atakaye kula kipande cha nyama ya mbuzi atakuwa amekula kitimoto indirectly.
 
Mzee Mwanakijiji ni mtu anayejifanya anaelewa kumbe haelewi anachojifanya anaelewa. Ni sampuli za watu wanaoleta machafuko vichwani mwa watu wasioelewa
 
Mzee Mwanakijiji ni mtu anayejifanya anaelewa kumbe haelewi anachojifanya anaelewa. Ni sampuli za watu wanaoleta machafuko vichwani mwa watu wasioelewa

Usiseme tu alimradi umesema. Kama kuna kitu nimekisema ambacho si sahihi - kisheria au kihalisia - nisahihishe na niko tayari kubadili mawazo. Ndio kujulishana. Sijifanyi naelewa; nikielewa ninaelewa. Mtu akisema amemwagiwa maji ni ama amemwagiwa au la; huwezi kujifanya umemwagiwa maji wakati hujamwagiwa. Kuelewa ni kuelewa au kutokuelewa.
 
Hivi huko Zanzibar ZEC na NEC walikuwa na wasimamizi tofauti kabisa?

Yaani kila kituo kilikuwa na wasimamizi wa ZEC pamoja na wa NEC?


Hakuna wasimamizi wawili mkuu NEC ndiyo ZEC kule Zanzibar!!!
 
Moja ya dosari iliyotajwa na mwenyekiti ni idadi ya wapiga kura kuzidi daftari la wapiga kura.NEC ina daftari tofauti na ZEC huko Zanzibat au ni lilelile?

Kama ni hilohilo kwa nini NEC iendelee kuliona ni halali wakati ZEC ambao ni mawakala wao wamelioja haliwexi kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki?

Umejuaje ni daftari lile lile? Hivi unafikiri kila Mtanzania aliyeko Zanzibar anaweza kupiga kura za Rais wa Zanzibar na Wawakilishi? Mtu anawatofautishaje hawa kwenye hilo daftari lao kama ni moja?
 
Ballot papers zilizotumiwa Zanzibar zikoje?

Kuna za ZEC na za NEC?

Na je, hizo dosari zilizoainishwa na huyo mwenyekiti zilikuwepo tu kwenye uchaguzi wa ZEC na si NEC pia?

Like, really? Seriously?

Unajua hawa jamaa they are so stupid. They are so stupid to think that maybe we are all stupid [like they are].
They are so stupid to think they know everything and we know nothing.
 
ZEC ndiyo NEC kule Zanzibar!!!

ZEC ni wakala kikatiba wa NEC kule Zanzibar so NEC ya bara haipo Zenji isipokua ZEC ndo wanatenda kwa niaba ya NEC!!

Kwahiyo yote yaliyotokea yameratibiwa na ZEC na matokeo ya kura ZEC ndiyo inachakata then inatuma NEC bara!!!

Sasa huyu mkaanga sumu sijui anampotosha nani!!!

Anhaa...kwa hiyo watu waliosimamia uchaguzi wa rais wa jamhuri ya muungano ndo hao hao waliosimamia uchaguzi wa rais wa Zanzibar, siyo?

Na si kwamba kwenye kila kituo kulikuwepo na wasimamizi kutoka ZEC na wa kutoka NEC?
 
Hakuna wasimamizi wawili mkuu NEC ndiyo ZEC kule Zanzibar!!!

Lusungo sasa hamjitendei haki wenyewe; kuwa wakala wa chombo kingine haina maana umekuwa chombo kile kingine. Wakala wa kampuni ya ndege siyo kampuni ya ndege. Akikata tiketi anakata tiketi kwa niaba ya kampuni hiyo n.k. Ukipata matatizo na ndege hiyo guess unaenda wapi kulalamika - kwa kampuni siyo kwa wakala. ZEC inafanya kazi ya uwakala wa NEC. Sasa hili nalo inabidi lije kuondolewa kwa sababu mambo kama haya hayahitajiki; kwa sababu ya matatizo ya Zanzibar wanataka kutishia uchaguzi mzima wa Muungano bila sababu.
 
Hivi huko Zanzibar ZEC na NEC walikuwa na wasimamizi tofauti kabisa?

Yaani kila kituo kilikuwa na wasimamizi wa ZEC pamoja na wa NEC?

Wasimamizi ni wale wale kwakuwa ZEC ni agent wa NEC kwa upande wa Zanzibar hakuna wasimamizi tofauti waliotumwa na NEC, these people are insulting our intelligence.
 
Samahani.kwa swali.langu mwenyewe.ufaham anijibu hivi mwanakijiji yupo marekani kama mkimnizi ama??
 
Anhaa...kwa hiyo watu waliosimamia uchaguzi wa rais wa jamhuri ya muungano ndo hao hao waliosimamia uchaguzi wa rais wa Zanzibar, siyo?

Na si kwamba kwenye kila kituo kulikuwepo na wasimamizi kutoka ZEC na wa kutoka NEC?

NN, correct kabisa. Ila hapa naona watu wanahitimisha sana bila kuangalia kwa ukaribu kidogo. Uchaguzi wa NEC unaendeshwa kwa kanuni za NEC siyo ZEC. Kama umeona matokeo ya majimbo ya Zanzibar yameendelea kutoka kama kawaida kwa sababu masanduku yao tofauti, yanahesabiwa tofauti, na yanaripotiwa tofauti. Ndio maana nimesema hapo juu kuwa tatizo kubwa ni kufanya hizi chaguzi mbili zifanywe kwa wakati mmoja. Watu wale wale wangeweza kuendesha chaguzi hizi katika siku tofauti na wale kusingekuwa na tatizo.
 
Zec haijasema nini sababu ya kupigana kwa wajumbe wake
pia kimetokea nini mpaka sababu hizi tisa zikagunduliwa katikati ya usomaji wa matokeo?
Tamko la zec limekuja baada ya viongozi wastaafu kwenda znz hapa kunanini.
 
Samahani.kwa swali.langu mwenyewe.ufaham anijibu hivi mwanakijiji yupo marekani kama mkimnizi ama??

Na ikiwa ndiyo then what? Inahusiana vipi na ukweli wa hoja iliyopo. Wewe ulipo ni mkulima?
 
Lusungo sasa hamjitendei haki wenyewe; kuwa wakala wa chombo kingine haina maana umekuwa chombo kile kingine. Wakala wa kampuni ya ndege siyo kampuni ya ndege. Akikata tiketi anakata tiketi kwa niaba ya kampuni hiyo n.k. Ukipata matatizo na ndege hiyo guess unaenda wapi kulalamika - kwa kampuni siyo kwa wakala. ZEC inafanya kazi ya uwakala wa NEC. Sasa hili nalo inabidi lije kuondolewa kwa sababu mambo kama haya hayahitajiki; kwa sababu ya matatizo ya Zanzibar wanataka kutishia uchaguzi mzima wa Muungano bila sababu.
Sasa wakala wa hiyo ndege akinikatia tiketi ya kihuni nani wa kulaumiwa? Shirika la ndege au wakala?
 
Back
Top Bottom