Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,253
- 44,595
Nyongeza ya Maoni: Inabidi nisichoke kuelewesha ndugu zetu hawa ambao kwa namna fulani hawataki kuukubali ukweli hata kama unawakodolea macho. Tatizo kubwa la kuelewa kilichotokea Zanzibar ni kuwa chaguzi hizi mbili zimefanyika kwa wakati mmoja na mahali pamoja na hivyo ukiwaambia kuwa hazihusiani haiingii akilini. Lakini wataelewa tu kama vile tulivyoahidi watazinduka tu. Hili siyo suala la kutaka CCM ishinde au Shein ashinde; ni suala la kuwa sahihi tu. NImewahi kusema huko nyuma chuki peke yake haitoshi kuchochea mabadiliko kwani tatizo kubwa la chuki ni kupofusha. Ukishamchukia mtu humsikilizi, huoni na wala huelewi.
Sasa kuna watu wameamua kwa sababu ya chuki tu hawataki tena kutumia akili zao kwa sababu wakifanya hivyo wanaweza kubadili mawazo. Lakini hili si tatizo, itabidi tuwasaidie ndugu zetu washinde hiyo hisia kwa wakati huu ili wasije kujikuta wanakata tamaa ya mabadiliko ya kweli.
Sasa kama chaguzi hili mbili zingekuwa zimefanyia siku tofauti ingekuwaje?
1. ZEC kama wakala wa NEC kwenye kura za Urais na Wabunge wa Muungano ingesimamia uchaguzi siku ile ile uchaguzi wa JMT unafanyika.
2. Wananchi wa Zanzibar wangeenda kupiga kura za Urais na Ubunge wa JMT kama Watanzania wengine; wangekuwa na maboksi mawili ya kura zao; na wangeenda wakapiga kura kama Watanzania wengine.
3. Uchaguzi wao ungeanza na kufungwa kama Tanzania nzima na matokeo yake yangekusanywa na kujumlishwa kama Tanzani ailivyo, yale ya Mbunge yangetangazwa huko huko Zanzibar kama ilivyo sehemu nyingine Tanzania na yale ya Rais yangejumlishwa huko huko na kutangazwa na kisha kutumwa NEC siyo makao makuu ya ZEC.
4. KUra zake zingehesabiwa kama kura nyingine na jumla yake ingeingizwa kama jumla ya kura za kitaifa; hivyo kwa mfano wetu wa leo Magufuli na Lowassa wangepata kura zao kama walivyopata sasa.
5. Rais wa JMT angetangazwa kwa kujumlisha kura zote za Zanzibar na za Bara. Matatizo mengine yangeshughulikiwa kama ilivyo sehemu nyingine.
6. Hayo yote hapo juu yangefanyika kwa mujibu wa Katiba ya JMT na Sheria za Uchaguzi za JMT ambazo zinafanya kazi pia Zanzibar.
Halafu, Siku nyingine - sema mwezi mmoja badaye - wananchi wa Zanzibar wangeenda kupiga kura za kuchagua Rais wao, Wawakilishi na Masheha wao (sijui kama wanachaguliwa sasa au vipi).
1. ZEC ikiwa ni chombo cha Uchaguzi cha Zanzibar kingeandaa kila kitu kinachohusiana na uchaguzi huo bila kuhusiana, kushirikisha, kuomba kibali toka NEC.
2. Wananchi wa Zanzibar wangeenda kupiga kura bila kujali kura zao za Urais wa JMT au Ubunge wa JMT kwani kura hizo zilishapigwa na kuhesabiwa kwenye kura za uchaguzi ule mwingine.
3. Kura zingepigwa, kuhesabiwa na kutangazwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Uchaguzi za Zanzibar.
4. Washindi wangepatikana na kutangazwa kwa taratibu hizo hizo za Zanzibar. Tume ya Taifa ya Tanzania isingekuwa na kitu chochote cha kufanya huko Zanzibar, mambo yote ni ya Wazanzibari.
5. Kura hizi za uchaguzi wa Zanzibar HAZIINGIZWI, KUJUMLISHWA AU KWANAMNA YOYOTE KUHUSISHWA na zile kura za uchaguzi mwingine. Kwa maneno mengine hazihusiani kabisa na kura za Uchaguzi Mkuu. Hii ni pamoja na ukweli ni kuwa watu waliopiga kura kwenye chaguzi hizi mbili ni wale wale.
6. Kama kuna matatizo yangeshughulikiwa kwa mujibu wa taratibu hizo. Suala la kufuta matokeo na mamlaka nimelishazingumzia silirudii tena.
Sasa, ukiangalia vitu hivi unaweza kuona kuwa kumbe hizi chaguzi ni sambamba - parallel. Yaani zinaenda sambamba bila kukutana. Nimesema hapo kuwa sababu ya urahisi wa utendaji zimepangwa kufanyika pamoja lakini si LAZIMA zifanyike pamoja.
Swali kubwa ambalo wengi linawatatiza na hili pia ni kwa sababu ya kutokuelewa huo usambamba nilioueleza hapo juu ni kuwa - kwenye uchaguzi huu uliofanyika siku moja na kusimamiwa na watu wale wale inakuwaje mmoja unavurugwa na mwingine hauvurugwi?
Kama mtu amenielewa - ukiondoa mashabiki wa kisiasa tu - kuwa kimsingi chaguzi hizi haziingiliani. Tukishaelewa hili tunabakia na jambo moja tu ambalo wengi tayari tunakubaliana toka awali - haja ya kuhoji kama Mwenyekiti au Tume ina uwezo wa kisheria wa kufuta matokeo yote ya uchaguzi nakama inayo ni katika mazingira gani na kama mazingira hayo yapo katika hili. Sasa jibu la hili siyo maoni ya kila mtu; ni Mahakama. Sasa sijui niweke hili vipi.
Hata wenzetu Wamarekani ambao leo wanatulazimisha tuendelee na matokeo hawakufanya hivyo katika uchaguzi kati ya Gore na Bush miaka kadhaa nyuma. Wao wenyewe hawakusema mtu atangazwe mshindi tu walienda hadi Mahakama Kuu kabisa ya Marekani (Supreme Court). Na sisi tuna vyombo vya sheria kwanini tusitake kuvitumia kutatua tatizo la kisheria au kikatiba?
Jambo la mwisho kubwa ambalo nimelisikia likirudiwa rudiwa bila kuonesha watu wamefikiria sana ni kuwa ati wapiga kura wa chaguzi hizi mbili ni "wale wale". Sijui ni nani kaanzisha ulaghai huu mwingine ambao umeaminiwa hata na watu wasomi kabisa. Siyo kila mtu anayeishi Zanzibar ni Mzanzibari; na si kila Mtanzania ni Mzanzibari. Kila Mzanzibari ni Mtanzania. Hii ina maana kuwa wale wanaopiga kwenye kura za chaguzi zinazoendeshwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ni Wazanzibari tu na wanavitambulisho vyao vya ukaazi. Wanaopiga kura kwenye chaguzi za NEC ni Watanzania wote; yaani Wazanzibari na Watanzania wengine wenye ukaazi wa Bara kisheria. Kwa maneno mengine, Watanzania wengine ambao watapiga kura kumchagua Rais wa JMT na Wabunge hawatopiga kura kuchagua Rais wa Zanzibar na Wawakilishi kwa sababu wao siyo Wazanzibari. Ni kwa sababu hiyo pia idadi ya wapiga kura wa chaguzi hizi mbili siyo ile ile kwani uchaguzi wa NEC utakuwa na wapiga kura wenye kujumuisha Watanzania wote wakati ule wa ZEC utakuwa ni wa Wazanzibari tu.
Leo hii wanaofikiria kushabikia kwenda mitaani wajue tu kuwa Watanzania wapo wengi na wenye mawazo tofauti; sidhani kama na watu wa upande wa pili nao wakisema na wao waende mitaani basi tutalala vizuri. Hautakuwa mpambano wa wananchi na vyombo vya dola kama wengi wanavyofikiria; itakuwa ni wananchi dhidi ya wananchi. Ni lazima tujaribu kuepeussha hilo. Litakapotokea basi sote tujue limepaswa kutokea.
Jambo