Nyomi ya coco beach ni balaa imevunja rekodi

menny terry

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
509
Reaction score
672
Wakuu,

Kama kawaida sichoki kuwaletea matukio mbalimbali na leo nilipita Coco beach! Aisee nyomi niliyoikuta huko imevunja record zote. Watu ni wengi sana aiseee. Watu wazima kwa watoto wadogo. Nadhani kuna haja Uongozi wa Coco beach kuweka vifaa mbalimbali vya kuokolea watu kama Ambulace na vifaa vya tiba haraka ili kuokoa maisha ya watu endapo changamoto yoyote itatokea.
Nawasilisha.

Kuna Mwingine Ameripoti Nyomi Kivukoni...Ferry kuwa Ilikuwa Balaa..

Nafikiri tushakuwa Wengi Dar na Sehemu Za Ku refresh ni Chache..!

Kipindi Cha Nyuma ...Makonda Alikuwa Mbunifu...Sasa Zamu Ya Mzee Makalla Sijui Atabuni nini Kuhusu Suala hili?
 
Hii ni coment ya yangu nimecomment kwenye uzi mwingine kama huu naipaste hapa.

Wengi wenye umri mdogo humu hamuwezi kujuwa lakini nawakikishia hili ni tatizo la ccm kuuza au kupora viwanja vya wazi.

Zamani hakukuwa na uzuraraji wa kiholela nje ya wilaya zenu na tarafa zenu palikuwa panajengwa mabanda (Circus) basi hapo burudani zote hupatikana, ngongoti, korokoro, muziki theater groups and likes ali mradi ni burudani tupu, watoto kwa wakubwa hakika walifurahi sana, na kulikuwa na mzunguko mkubwa wa pesa kwa biashara zote za vinywaji na vitafunwa, yani ilikuwa Disney land fulani.

Kuna kina sisi wengine tuliokuwa wapenzi wa sinema tulikwenda kuangalia movie Avalon cinema, Empire, New chocks, Odeon, Cameo, Drive in and so on,

Kwa mfano viwanja vya mnazi mmoja, buguruni chama, Temeke kata ya 14, kiwalani kata ya kipawa, mwenge, hizi sehemu kwa uchache zilikuwa na circus zao kama Disney land fulani hivi, lakini kwakuwa kuna kundi la walafi ccm wakateka nyala haya maeneo ya wazi either kujimilikisha au kuyauza na hatimaye huu utamaduni ukayeyuka jumla jijini Dar.

Ni hatari sana siku za sikukuu kundi moja kubwa lote kuelekea out sehemu moja kwa kukosekana public area za community kukutana.

Kwa tuliofuta matongotongo na kutembea nchi zenye viongozi wenye akili na maono kila kata ina community center hall na park tena saa nyingine park zaidi ya moja, wakati Dar hiyo paki iliyobaki ya mnazi mmoja na bado inafungwa, very fun aisee.

Inshort tatizo siyo waislamu, tatizo ni ccm.

Halafu kingine zamani siku za sikukuu ndio zilikuwa ndugu na familia kutembeleana na ndugu kujuwana lakini umaskini umeondowa upendo na sasa tunaishi kama manyani tu, hata mpenzi wako anakugeuza wewe ndio source of income na siyo tulizo la moyo tena
 
Bashite aliwahi buni kipi?!
 
Mkuu umesema jambo zuri sana,, kwenye nyomi Kama hio Kuna starehe gani tena Hapo zaidi yakuibiana tu manake mapanyaroad ndo wamechanganyikana humo humo mida yakusepa watu ndo huisoma namba...
 
Wakati wa sikukuu miaka hiyo ya nyuma Dar hakukuwa na shida ya usafiri ingawa familia nyingi hazikuwa na magari kwa sababu watu wengi walikuwa na sehemu za kusheherekea sikukuu maeneo yao hukohuko.

Tuliokuwa tunapenda kutoka tulitumia usafiri huu wa usafiri Dar Uda.

Hiyo ni Icarus kumbakumba.

E-2SPq8VQAIGb9s.jpg
 
Jana na juzi wanangu wananiambia "mama twende kwenye sikukuu" basi nawazuga zuga tu.
Maana wanaona heka heka watoto wenzao wamevaa wanaenda kutembea, nitawapeleka "kwenye sikukuu" jumamosi.
 
Wakati wa sikukuu miaka hiyo ya nyuma Dar hakukuwa na shida ya usafiri ingawa familia nyingi hazikuwa na magari kwa sababu watu wengi walikuwa na sehemu za kusheherekea sikukuu maeneo yao hukohuko.

Tuliokuwa tunapenda kutoka tulitumia usafiri huu wa usafiri Dar Uda.

Hiyo ni Icarus kumbakumba.

View attachment 2211893
Unakumbuka watu walikua wanatoka maeneo mbalimbali ya jiji, kwenda ndege bichi, na daladala za kukodi, huku zikepeperusha bendera za nchi mbalimbali hasa za nchi zilizoendelea.

Mwendo sasa, ni mwendo wa kasi, kurudi huko siku ya pili sasa kama umeenda peke yako shauri yako.
 
Waliluwa kifungoni, wametoka...hupenda kujazana kwenye pick up za mizigo kama suzuki cary na bajaji za mizigo
 
Back
Top Bottom