Nyomi la Usaili wa Nafasi 40 TRA

Nyomi la Usaili wa Nafasi 40 TRA

Narudia tena, Chuo Kiku waende wenye Div One na Two tu. Wengine waende vyuo vya kati ili viwaandae kujiajiri.
Unaumwa wewe Elimu inayo tolewa ndiyo inayo waandaa watu wawe wa kuajiriwa tusubili jk labda ataleta mabadiliko udsm
 
Unaumwa wewe Elimu inayo tolewa ndiyo inayo waandaa watu wawe wa kuajiriwa tusubili jk labda ataleta mabadiliko udsm
Ni kweli naumwa. Lakini japo ungeelewa maana ya vyuo vya kati usingekurupuka. Tuliwahi kuwa na vyuo vya kati kama Mbeya Tech College (sasa MUST), DIT, na Arusha Tech. Vyuo hivi vilikuwa vinatoa cheti tu (Full Technician Certificate). Pia nazungumzia vyuo kama Veta. Vyuo vya aina hivi mfumo wake wa ufundishaji unaitwa 'competence-based', kwa maana unazingatia ujuzi na vitendo zaid kuliko nadharia. Chuo Kikuu ni sehemu ya kujifunza nadharia. Hivyo mtu aliyepata elimu ya chuo cha kati ni rahis kujiajiri.

Nadharia inatakiwa ifundishwe kwa mtu mwenye uelewa mkubwa, yaan aliyefaulu vizuri. elimu ya vitendo unaweza ukaelewa vizuri hata kata hujawahi kuingia darasani. Kosa tulilofanya ni kufikiri kila mtu anatakiwa kuwa na shahada. Hadi wenye Div.3 na 4 sasa unawakuta Chuo Kikuu. Wanafanya nini? Pole sana mkuu, yaelekea wewe ndo wale Div 3 na 4.
 
Hawa ni watu 23,653 wanataka kufanya interview katika ukumbi wa diamond jubilee, ili kutafuta nafasi za ajira katika shirika la mapato Tanzania (TRA), wakati waliokuwa wanahitajika ni watu 40 tu.View attachment 318663
huu ni ushahidi wa wazi kuwa ccm hakijaweza kubadili mfumo wa white collar job kwenye elimu yetu kutoka ukoloni,nchi inazalisha wasomi waajiriwa sasa kunafaida gani yakuwa namavyuo kama utitiri kuzalisha wataalamu waajiriwa
 
Narudia tena, Chuo Kiku waende wenye Div One na Two tu. Wengine waende vyuo vya kati ili viwaandae kujiajiri.
kwa hiyo kwako unaona "top cream" isijiajiri? badala ya kupambana elimu itolewayo na mazingira yawe ya kumuandaa muhitimu kujiajiri pia,,,!
 
Ajira za kuajiliwa ni tatizo sugu, inabidi vijana wafikilie upande wa pili kujiajiri na serikali nayo kwa upande wake hawana budi kubafilisha mitaala ili kijana amalizapo elimu yake awe na uwezo angalau hata wa kushona, ufundi mbalimbali nk
 
kwa hiyo kwako unaona "top cream" isijiajiri? badala ya kupambana elimu itolewayo na mazingira yawe ya kumuandaa muhitimu kujiajiri pia,,,!
Wewe mgumu kuelewa, unafaa kwenda chuo cha kati au Veta. Nitajaribu kukuelimisha tena. Mtu anayefundishwa nadharia anafundishwa kufikiria na anayefundishwa elimu ya vitendo anafundishwa kutenda. Kazi za kufikiri ni chache kuliko za kuetenda-duniani kote iko hivyo. Kwakuwa wanaofaulu vizuri ni wachache, na mahitaji ya nchi ni watu wa nadharia wachache na wenye uelewa mkubwa, basi wale tu waliofaulu vizuri ndo wasome nadharia.

Maana yake ni kwamba mhandisi mmoja abuni mashine rahisi kutumia na ya gharama nafuu ya kutengeneza-mfano matofari, sasa vijana wengi wenye elimu ya kati ndo waitumie mashine hiyo kutengeneza tofari. N i mgawanyo wa kazi tu. Hatuwezi wote kuwa wajasiliamali. Ni sawa uniambie kwanini mkulima alime Pamba, asitengeneze na shati!? Mgawanyo sahihi ni mkulima alime pamba na auze kwa mfanyabiashara, mfanyabiashara auze kwa kiwanda na kiwanda kifume nyuzi na vitambaa na kuuza halafu viwanda vya nguo vinunue vitambaa na nyuzi ili kutengeneza mashati/nguo.
 
bora nikomae na biashara kulikoni kupata hili jinamizi la ajira khaa..inauma saana umeteseka kusoma alafu unakuta ajira holaa...
 
Unaumwa wewe Elimu inayo tolewa ndiyo inayo waandaa watu wawe wa kuajiriwa tusubili jk labda ataleta mabadiliko udsm
Endelea kumsubiri jk akuletee mabadiliko UDSM TZ ilimshinda aje akuletee mabadiliko UDSM ??
 
Back
Top Bottom