Nyoka wa Makengeza anakuja tena!

Nyoka wa Makengeza anakuja tena!

Umekurupuka! Jifunze kuandika dogo kabla ya kuleta pumba zako humu.

Zuzu wewe.
 
hizi mida za menyu hizi watu wanawaza misosi tu, na stori zinakua za misosi kama hii
 
Wewe yajimboni kwake yanakuhusu nini ungeeleza kwanza hali ilivyo jimboni kwako.
 
Vipi hali za raia vipi elimu vipi afya jimboni kwake maana anayoyafanya wakati wa uchaguzi ni balsa
Naona anachinja ng'ombe 10 pilau ya kufa mtu wali ni kupiga misosi tu akishinda ndio usiseme nasikia watu wanashiba wenyewe
Anachaguliwa kwa maendeleo au ni kwa nyama na pilau?
Tusaidiane mnaolijua jimbo lake
Si anajua kuwa wale watu ni ngazi ya kwenda sehemu akapige deal kama kawaida yao?
 
Anachaguliwa kwa kuleta maendeleo. Anaungana na wananchi wake ktk kuboresha elimu afya na miundo mbinu. Wananchi wanapochangia maendeleo anawaunga mkono. Vijiji vyake vyingi vimepata umeme na vilivyobakia vipi ktk mpango wa kupata umeme. Karibu bariadi ili ujionee
 
Nitakaribia mkuu
 
Unamaanisha nini kuchorwa kwa jimbo la Bariadi Mjini? Unaongea kishabiki na kidaku daku sana mpaka hueleweki. Jikaze uongee vizuri ueleweke mkuu. Huyo Simba ana makazi hapo Bariadi au alivamia tu?

Hahahahaaaa,
naona umeachwa solemba na tashtiti.
Elimu elimu elimu. Usipende kurupuka utakasirika bure.
 
Hahahahaaaa,
naona umeachwa solemba na tashtiti.
Elimu elimu elimu. Usipende kurupuka utakasirika bure.
Unaelewa nini kuhusu tashtiti (satire) wewe? Matumizi mazuri ya tashtiti hayahitaji hoja kinzani na maelezo meengi yasiyoeleweka. Tashtiti nzuri inakupeleka moja kwa moja kwenye hoja ya msingi tena mara nyingi kwa lugha nyepesi na yenye kufurahisha (ucheshi) halafu ukifika mwisho unagundua kuwa kumbe kinachosemwa na hata kuchekwa ndicho-sicho.

Hapo juu hakuna cha tashtiti wala nini bali ni uandishi wa kizembe tu na uvivu wa kupangilia hoja kindakindaki. But again you are right: Elimu, elimu, elimu. Safari yetu kama taifa bado ni ndefu kwani hata wa.ji.nga wanafikiri kuwa ni werevu. Pathetic!
 
Unaelewa nini kuhusu tashtiti (satire) wewe?

Naijua vizuri...

Hapo juu hakuna cha tashtiti wala nini bali ni uandishi wa kizembe tu na uvivu wa kupangilia hoja kindakindaki.

Hahaa, ww si ndio ulijifanya umeielewa tashtiti bhana, kumbe hukuielewa, so elimu zaidi unahitaji, haswa ya tashtiti.
 
joka lazima lipige deal ndefu ya mabilioni awamu hii,naliaminia sana,wafuasi wake tunasubiri kushangilia ushindi mwingine:redface:
 
Unamaanisha nini kuchorwa kwa jimbo la Bariadi Mjini? Unaongea kishabiki na kidaku daku sana mpaka hueleweki. Jikaze uongee vizuri ueleweke mkuu. Huyo Simba ana makazi hapo Bariadi au alivamia tu?
Wewe utakuwa unatokea Mwakibuga, kwa washamba wa kukomba na chai. Kwani Joka kipindi anakuja BR alikuwa na makazi? Kwa taarifa yako Joka bila Ubunge usingemuona Bariadi. Ni Sharobaro wa nguvu, suti zake huagiza kutoka London. Kitu kingine joka 'ameshikwa' sana na mke wake Komando Suzy,joka hafurukuti kama ilivyokuwa kwa Rais Kibaki. Hata neno kuchora hujui maana zake?!!!
 
Unaelewa nini kuhusu tashtiti (satire) wewe? Matumizi mazuri ya tashtiti hayahitaji hoja kinzani na maelezo meengi yasiyoeleweka. Tashtiti nzuri inakupeleka moja kwa moja kwenye hoja ya msingi tena mara nyingi kwa lugha nyepesi na yenye kufurahisha (ucheshi) halafu ukifika mwisho unagundua kuwa kumbe kinachosemwa na hata kuchekwa ndicho-sicho.

Hapo juu hakuna cha tashtiti wala nini bali ni uandishi wa kizembe tu na uvivu wa kupangilia hoja kindakindaki. But again you are right: Elimu, elimu, elimu. Safari yetu kama taifa bado ni ndefu kwani hata wa.ji.nga wanafikiri kuwa ni werevu. Pathetic!
Kwa hiyo mpaka ucheke wewe ndio itakuwa satire? Who was your language teacher, Ong'wise?
 
Mkuu huyo nyoka wa makengeza aje tu mjengoni tunamsubiri kwa hamu sana. Ila mwaka huu awe makini vinginevyo atarithi eidha chumba cha Yona au MRAMBA pale Segerea ndiyo maana Magufuli alimkwepa kumnadi.

Mkuu umeliona joka leo? Lilikuwa limejaa,limevimba kitini, linazungusha makengeza kusaka harufu ya ngawira. Good start joka. Wakimbize, kuja washituke...
 
Jaman hii thread inanivunja mbavu zangu aisee.
.
.
.
.
.
Joka linaponiacha hoi ni pale likipora ngawira linawazuia kulipeleka kamati za maadili hata mahakaman linaizuia mahakama kuendesha kesi yake. Yaan hili jamaa sijui linatumia sheria gani maana akina kikwete wakaishia kuchekacheka tu, Magufuli na ununda wake akalinadi japo hata kwa unafik.. Viva joka
 
Unaelewa nini kuhusu tashtiti (satire) wewe?

Naijua vizuri...

Hapo juu hakuna cha tashtiti wala nini bali ni uandishi wa kizembe tu na uvivu wa kupangilia hoja kindakindaki.

Hahaa, ww si ndio ulijifanya umeielewa tashtiti bhana, kumbe hukuielewa, so elimu zaidi unahitaji, haswa ya tashtiti.
Sawa mkuu. Mimi ndiyo sikuielewa tashtiti. Yaani nguvu za kuendelea kuhojiana zimeniishia ghafla. Have a nice day!
 
Kwa hiyo mpaka ucheke wewe ndio itakuwa satire? Who was your language teacher, Ong'wise?
Ukisoma tena maelezo yangu hapo juu utanielewa tu. As to my language teacher - tunamalizia kitabu kinachoitwa "Tashtiti Katika Fasihi ya Kiswahili" na kitachapishwa na Mkuki na Nyota Publishers mwaka kesho. Humo kuna makala nzuri za mabingwa wa fasihi wakiwemo Kezilahabi, Senkoro pamoja na Ngugi. Ninazo makala mbili humo moja comparative na akina Charles Dickens, George Orwell etc kwa muktadha wa Juvenalian satire. That's my language teacher sir!
 
Wewe utakuwa unatokea Mwakibuga, kwa washamba wa kukomba na chai. Kwani Joka kipindi anakuja BR alikuwa na makazi? Kwa taarifa yako Joka bila Ubunge usingemuona Bariadi. Ni Sharobaro wa nguvu, suti zake huagiza kutoka London. Kitu kingine joka 'ameshikwa' sana na mke wake Komando Suzy,joka hafurukuti kama ilivyokuwa kwa Rais Kibaki. Hata neno kuchora hujui maana zake?!!!
Vipi tena mkuu? Hii si mada yako wewe? Mimi niliuliza tu kistaarabu kwani sijui. Sasa mambo ya Mwakibuga yanatoka wapi tena?

By the way huko Mwakibuga ni wapi? Wewe una ubora gani kuliko hao watu wa Mwakibuga unaowaita washamba? Kama wanakomba chai, si ni uhuru wao? Wewe ni nani mpaka uwapangie maisha yao?

Usharobaro wa Joka Makengeza na makorokocho mengine mi hayanihusu. That's his personal life. Nilikuwa namuulizia Ngwilimi kwani nilikuwa na imani kubwa pengine angeweza kushinda.

Safari nyingine ukianzisha mada be humble na wajibu wachangiaji wako kistaarabu tu na siyo kutunisha misuli yako ya dharau bila sababu. Wabeja!
 
Back
Top Bottom